Albert Msando
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 1,019
- 171
- Thread starter
- #41
Si suala la umaarufu wala nini, kama wana CDM wanalalamikia Mary Chatanda kushiriki katika baraza la madiwani Arusha kama Mbunge wa kuteuliwa basi waunge mkono kesi hii, ili haki itendeke na si kupinga eti kwa sababu watapoteza Halmashauri ya HAI endapo MSANDO atashinda katika kesi husika. Kama unachukia uonevu chukia pia kuonea, kama unachukia kubaguliwa chukia pia kubagua. Tusiwe tunakasirika na kulalama pale CDM inapoonewa lakini inapoonea tukae kimya. Tusimamie haki na si kusimamia chama.
TAADHALI KWA WAKILI MSANDOALBERTO (wewe ni mwanasiasa wengine sisi ni wanaharakati hatuna chama bali tunasupport chama tunacho amini kitaleta mabadiliko yanayotakiwa hapa nchini) Kumbuka CCM wanampango wa kuvunja Baraza la Madiwani Katika JIJI la ARUSHA na kuunda TUME, hivyo kesi yako hutomkomoa MARY CHATANDA WALA CCM, lakini kwa Upande wa HAI mjini ukishinda kesi utakikomoa chama chako na wanachama wenzako LUCY OWENYA na LUCY KIWELU. Je utaweza kupambana kama ZITTO ndani ya chama? yaani wewe uwe upande mwingine na CDM upande mwingine katika mapambano hayo? Jifunze kwa yanayomkuta ZITTO lakini ukiwa tayari kwa lolote GO ON.
My brother, kama ni mabadiliko hayawezi kuja kwa maneno peke yake. Lazima maamuzi magumu yafanyike na atakayepinga anipinge kwa hoja. Sitarudi nyuma hata kidogo. Mawazo yangu yatabaki kuwa huru na sitaruhusu nitumbukie kwenye dimbwi la mkumbo au ufuasi. Chadema itajengwa kwa mawazo huru na siasa ambazo zi za kufuata mkumbo.
Niseme neno, kwa Mahakama kutoa uamuzi kwamba Wabunge hao sio wajumbe haimaanishi kwamba CDM au CCM vitapoteza halmashauri walizoshinda. Sheria iko wazi kwamba kitakachotokea ni wale kutokuendelea na ujumbe wao lakini maamuzi yaliyopitishwa wakiwemo hayatakuwa batili unless kwa sababu nyingine kama vile kutokuwepo kwa quorum etc.
Kuna watu ambao wanachukulia kwamba Halmashauri ya Hai itapotea. Si kweli. Mwenyekiti wa Halmashauri akishachaguliwa anaendelea kuwa mwenyekiti kwa miaka mitano. Huo ndio uwoga unaowaingia watu kiasi kwamba wako tayari kuvunja sheria ili mradi Halmashauri ibaki kwetu. Hata kama ingekuwa tunapoteza Halmashauri isingekuwa sahihi kuvunja sheria kisa halmashauri. Tutakuwa na tofauti gani na CCM ambao wako tayari kuua ili mradi ukweli usijulikane? Wako tayari kuua ili mradi Meya awe wa kwao?
Chadema hatuko hivyo na hatutakuwa hivyo. Wanaokurupuka humu ndani aidha si wanachadema au ni wanachadema ambao hawana uelewa wa kutosha na wanafuata mkumbo. Tutawanyoosha tu.