Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 24, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu WanaJF,

  Hatimaye nafsi yangu imekuwa huru. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu huku nikiumia moyoni nafsi yangu sasa imekuwa huru na niko tayari kufanya lile ambalo naamini halitawapendeza wengi lakini ni sahihi kwa maslahi ya Taifa letu.

  Mimi kama Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea na Diwani kwa tiketi ya CHADEMA nimekuwa na wakati mgumu kufanya au kufikia uamuzi huu.

  Kwanza, kabisa ni mategemeo ya wengi kwamba kama Diwani wa Chadema ni lazima nifuate utaratibu ndani ya Chama. Nategemewa kusema au kufikiria vile chama au wanachama wengine wanavyofikiria. Hapana.

  Pili, nategemewa kwamba nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakisaidia chama kukua na kupendwa zaidi (njia zile ambazo wengine wanaona ndizo sahihi ikiwa ni pamoja na kutosema ukweli au kukemea uovu ili mradi chama kitanufaika).

  Tatu, nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakidhoofisha chama cha mapinduzi (CCM). Hata kama ni kwa uonevu au kwa kupindisha ukweli (mara nyingi kinachosemwa dhidi ya CCM ni ukweli na ni mara chache sana watasingiziwa au kuonewa).

  Nne, kama Mwanasheria na Wakili nimtetee na kumlinda mteja wangu. Hilo nitafanya daima.

  Lakini katika hili, nitafanya vile ambavyo nafsi yangu inanituma kufanya na kwa faida ya nchi yangu. Pia vile vile kulinda heshima na fani ya sheria mbele ya jamii.

  Nimeamua kuwashitaki Waheshimiwa Wabunge wafuatao;

  1. Mh. Grace Kiwhelu - Viti Maalum (Moshi Vijijini) - CHADEMA.

  2. Mh. Lucy Owenya - Viti Maalum (Moshi Mjini) - CHADEMA.

  3. Mh. Mary Chitanda - Viti Maalum (Tanga) - CCM.

  Pia katika kesi hizo nimemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Waheshimiwa Wabunge hawa ni wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Halmashauri ya Manispaa Arusha.

  Ni ukweli usiopingika kwamba Waheshimiwa hawa ni wateule wa vyombo (organs) vya vyama vya siasa i.e. CHADEMA na CCM. Vyombo hivyo UWT na BAWACHA vilivyowateua haviko ndani ya Halmashauri husika. i.e Hai na Arusha. Vyombo hivyo viko nje ya Halmashauri hizo hivyo hawastahili kuwa wajumbe.

  Sheria husika kuhusu Wabunge wa Viti Maalumu kwa Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa Sheria Namba 7 ya 1987 inasema hivi (kifungu cha 35(e):

  35. Constitution of district councils

  (1) Every district council shall consist of–

  (a) members elected one from each ward in the area of the district council;

  (b) three members appointed by the Minister;

  (c) the Member or Members of Parliament representing constituencies within the area of the district council in the Assembly; and

  (d) such number of women members who are qualified to be elected to the council, being not less than one third of all the members referred to in paragraphs (a), (b) and (c) to be proposed by the political parties represented in the Council in such numbers as shall be proportional to the number of the members of those parties elected to the Council, who the electoral authority shall declare to have been elected into the Council;

  (e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

  Kwa kiswahili naweza kusema Kifungu hicho cha sheria kinasema hivi;

  Mbunge mwingine yoyote ambaye uteuzi wake umeanzia kwenye vyombo vya vyama vya siasa ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya.

  kwa upande wa mamlaka za Majiji sheria husika ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 13 ya Mwaka 2006 kifungu cha 17 ambacho kinaongeza kifungu kidogo (d) kwenye kifungu cha 19 cha Sheria Namba 7/1982 kwamba;

  (d) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

  Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno; nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili.

  Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda Arusha. Alitumia siasa kutoa tafsiri hiyo huku akijua wazi kwamba anakosea.

  Mwanasheria Mkuu alikosea zaidi pale alipoamua kuchukua jukumu la kutoa tafsiri ya sheria badala ya kuiachia mahakama itoe tafsiri hiyo. Sheria zote mbili za Serikali za Mitaa (Namba 7 na 8 za Mwaka 1982) zimetoa utaratibu wa kufuatwa endapo kutakuwa na maswali kuhusu uhalali wa mtu kuwa mjumbe kwenye Halmashauri. Sheria inasema hivi:

  43. Decision of questions as to membership of council

  (1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

  (a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

  (b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

  (c) a person claiming to have been a candidate at the election;

  (d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

  (e) the Attorney-General.

  Mwanasheria Mkuu anatajwa kama mmoja wapo wa watu wanoweza kupeleka maombi mbele ya Hakimu Mkazi ili atoe uamuzi kuhusu uhalali wa ujumbe wa mtu. Hakufanya hivyo badala yake watu wamekufa, mali zimeharibika na wengi wameumizwa. Pia serikali inaingia gharama kuendesha kesi dhidi ya walioandamana.

  Ni sababu zipi zilimfanya Mwanasheria Mkuu asilione hili? Kwa nini alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu Mary Chitanda? tangu uchaguzi ulipomalizika, mvutano ulipojitokeza tarehe 17/12/2010 mpaka tarehe 5/01/2011 Mwanasheria Mkuu hakuwa amepata jibu la nini kifanyike kutatua Mgogoro wa kama Mary Chitanda ni mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha au la?

  Kwa kusoma vifungu hivyo vya sheria hata mtoto wa mwaka wa kwanza wa stashahada ya sheria (Certificate of Law) angeweza kutoa tafsiri sahihi ya Mbunge wa Viti Maalumu anatakiwa aingie kwenye Halmashauri ipi. Ni Halmashauri ile ambayo chombo kilichomchagua kipo. Kama alichaguliwa na UWT Tanga basi anaingia halmashauri ile ambayo UWT Tanga ipo. Kama alichaguliwa na BAWACHA (Baraza la Wanawake Chadema) anaingia pale ambapo baraza hilo lipo. Na sio Halmashauri yoyote nchini!

  Natambua Mods wanaweza kuamua hii mada iende kwenye Jukwaa la Sheria. Napinga mada hii kupelekwa huko kwa sababu siasa ndio ilitumika kufikia tafsiri hiyo na athari zilizojitokeza ni za kisiasa zaidi. Sheria iko wazi.

  CHADEMA waliamua kutumia njia ya Maandamano kupinga kile kilichoonekana ni dhuluma ya wazi na uvunjaji wa sheria mchana kweupe. Walitaka kuonyesha umma ni jinsi gani baadhi ya watu wako tayari kukanyaga sheria za nchi ilimradi tu matakwa yao yatimie. Kilichofuata ni kupigwa nakutawanya kwa nguvu kubwa bila sababu. Labda sababu ilikuwa ni kuficha ukweli.

  Naamini kwamba Mungu ana njia nyingi za kutufanya tuone ukweli na sasa muda umefika. Ni muda wa mahakama kuiangalia Sheria inasemaje na kutoa tafsiri sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa.

  Hili nitalisimamia na kulipigania. Hata kama Chama changu kitaguswa kwa msimamo wangu niko tayari kutetea ukweli na sheria za nchi. Hicho ndicho kiapo changu mbele ya Jaji Mkuu mwaka 2007. Siwezi kukivunja nitakuwa kama wao.

  HITIMISHO.

  1. Waheshimiwa Grace Kiwhelu, Lucy Owenya na Mary Chitanda SI wajumbe halali wa Halmashauri za Hai na Arusha.

  2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (pamoja na Katibu wa Bunge na Tume ya Uchaguzi) walitoa tafsiri ambayo si sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda, Grace Kiwhelu na Lucy Owenya kama wajumbe wa Halmashauri hizo.

  Siasa imetuponza. Maamuzi ambayo yalitolewa kisiasa ili kufanikisha nia na malengo ya kisiasa yamesababisha watu watatu (3) wamepoteza maisha, mali zimeharibiwa na wengi wamebaki vilema.

  Hakukuwa na sababu ya polisi kuzuia maandamano ya amani yaliyopangwa na CHADEMA. Hiyo ilikuwa ni njia ya kuficha uovu ambao sasa utajulikana. Uzembe na ubinafsi vinaimaliza hii nchi.

  Wote tusimame imara na kutetea ukweli. Tuungane kwa pamoja kuwasaidia wananchi wetu masikini ambao sisi wasomi tunachokisema wanakiamini hata kama tunawadanganya.

  MwanaJF yeyote anakaribishwa kuungana nami kama mlalamikaji katika kesi hizo mbili za kuweka kumbukumbu sawa. Kesi dhidi ya Wah. Grace Kihwelu na Lucy Owenya zinafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kesi dhidi ya Mh. Mary Chitanda inafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

  Nawasilisha taarifa.
   
 2. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Unajisumbua bure....we utaona tu, hukumu itatolewa June 2015 ikiwa umebaki mwezi mmoja vipindivyao vya ujumbe huo haramu unaouona wewe uishe.
  Anyway, sikukatishi tamaa..jaribu!
   
 3. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni mwanaume,mkweli kwa jamii na kwa nafsi yako.tunataka watu wanaosimamia haki si wanaotetea maovu na kuyafanya kwa maslahi ya vyama vyao.kila la kheri!!
   
 4. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kesi za kisiasa hasa za kupinga matokea na kuweka mapingamiz huwa haziishi kama unataka ushahid muulize Mh John myika na kesi yake dhid ya Keenja ilimalizika lin? hii nchi tuna mihimil mitatu katika maandish tu .
  mahakama,bunge na rais vyote ni mali ya kikundi cha wezi wale wale CCM.
   
 5. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tutapambana, naamini kwamba itawezekana. Nitakukumbusha tukifanikiwa. Hatuna cha kupoteza kwa kufanya MK. Ujumbe utakuwa umefika na ukweli utajulikana hata kama ni baada ya miaka mingi.
   
 6. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kesi hii ni kutafuta tafsiri sahihi ya sheria. Tutaipigia kelele mpaka itasikilizwa.

  Kwa nini tunakata tamaa? serikali ni yetu, mahakama ni zetu na bunge ni letu. Kwa nini tunakubali kuonewa? Kwa nini tunakubali kudhulumiwa? Kwa nini? Mimi nimesema basi na ifike mwisho. Katika mazingira hayo magumu nitasema na kupaza sauti daima. haki itatendeka!
   
 7. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Najua CHADEMA iliamua kuwapeleka Owenya na wengine Hai baada ya kuona uhuni wa CCM kwa Arusha. Binafsi nakushauri ulie na tafsiri potofu ya mwanasheria mkuu wa serikali. Baada ya kushinda hiyo kesi basi mambo mengine yataenda sawa maana yatarekebishwa tu!

  Naamini Chadema haina tatizo katika hilo ila tatizo ni hiyo tafsiri ya mwanasheria mkuu wa serikali. Fungua mashitaka ya kikatiba au vinginevyo uonavyo bila kuwapotezea muda waheshimiwa wabunge wetu wa Chadema! Am not a lawyer by the way lakini nimeshauri kama raia tu!
   
 8. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,650
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Hatuna budi kuheshimu utawala wa sheria na demokrasia.
  Makosa ni muhimu yarekebishwe ili yasijirudie,hata kama chama chako kimefaidika kupitia makosa hayo hayo!
   
 9. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NINA WASIWASI NA UANACHAMA WAKO

  wewe ni mamluki wa ROSTAM umetumwa kuja kupoteza malengo yetu ya maandamano nchi nzima,SHINDWA
   
 10. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tihii tihiii...ni kweli broda but when the truth prevails uongo utakuja jitenga tuu.
  broda nenda kashtaki.
   
 11. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Malengo ya CHADEMA ni kupindisha sheria, kukiuka sheria na kuvunja sheria? Nani anatakiwa kutilia mashaka uanachama wa mwenzake? Ningetegemea kama mwanachadema uwe mstari wa mbele kupigania haki na ukweli. Kilichotokea Arusha hakivumiliki na lazima kipingwe kwa nguvu zote.

  zaidi, soma maelezo yangu na utoe tafsiri yako. Au toa msimamo wako. Msimamo wangu uko wazi. Wabunge hao sio wajumbe wa halmashauri hizo. Nitausimamia msimamo wangu na uanachama wanguu utabaki.

  Mwisho, unaandamana nchi nzima ili iweje kama hutaki haki itendeke? wewe ni mwanachama wa kipekee kabisa. Ukishaandamana halafu? Kwa hiyo kwa sababu tumepanga kuandamana basi tusitafute haki mahakamani? Sitakushangaa. Ukisoma nilichosema utaelimika na kuelewa nini cha kufanya.
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Uliapa 2007? Bado kuruta tu!
   
 13. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wewe tunakufahamu. Huna Uchungu huo bali unatafuta UMAARUFU KWA NGUVU KWELI. Ulishindwa DARUSO sasa unataka uraiani. Umaarufu hautafutwi hivyo. Jiangalie mdogo wangu Abert, UTAPOROMOKA!
   
 14. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #14
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Si kweli, ataporomoka kwa sababu umesema? yeye ni Diwani, ebu waambie ukoo wako wajipange popote walipo simikeni Diwani mmoja tu uone kama ni kazi rahisi!

  Tunamjua Msando ana uhuru wa mawazo popote alipo, we know this

  Go Msando Go!!
   
 15. M

  MushyNoel Senior Member

  #15
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msando,

  Naomba unifahamishe yafuatayo kwani mimi sina utaalamu na Sheria,

  Je hawa wabunge si walipewa barua na vyama vyao kuwasili katika jimbo flani kama mwakilishi wa jimbo hilo ? Na katika kutafuta tafsiri kwa nini wasishtakiwe wale tu waliopindisha maana/tafsiri ya sheria husika?

  Hauni kwamba kwa kuwashtaki hawa wabunge ,watakuja na ushahidi wa barua walizopewa na vyama vyao nahivyo ukahitajika kufungua kesi nyingine ambayo itawahusu waliopindisha tafsiri na hivyo kumislead the whole system .

  Je wabunge kama wa CDM wana kosa gani ilhali baada ya Mwanasheria mkuu wa serikali kupindisha tafsiri,na kwa sababu mwanasheria huyo yupo kwenye nafasi ya kutoa tafsiri sahihi..basi wao kama wadau wa siasa wakaamu kumteua Mh Kiwelu na Owenya kwa jimbo la hai na Anna komu jimbo la arusha mjini ?

  Ni hayo tu.
   
 16. n

  nyantella JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Thanx Albert for being honest to yourself in seeking justice. how about adding the Mayorship crisis in Arusha kwenye kesi hiyo ili tujue mbivu na mbichi? otherwise I personnly wish you all the best!!
   
 17. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SASA NA WEWE ALBERT SI ULIKUWA MASHUHURI TUU DARUSO NA UMEPATA UANASHERIA HIVI JUZI JUZI SASA ILIKUWAJE UKAGOMBEE UDIWANI AISEE KUNA NINI HUKO MBONA NA RAFIKI YAK=NGUI KITURURU NAE ALIKUWA ANAGOMBEA UDIWANI HAPA UBUNGO??

  LAKINI KAMA UNA ISSUE NA GRACE ISOLVE KWANZA ITAONEKANA UNA BIFU LA KIMAPENZI MAN,
  ILA MWANASHERIA WAKILI DIWANI DUU ,MBONA UNAINGILIA KAZI ZA WATU MI NAONA MADIWANI WANGEKUWA MADIWANI TUU NA WANASHERIA TUFANYE KAZI YETU YA KUWACHEK SIOHUMO HUMO TENA AU NI NJAAA

  SASA HILI LA KIWELU AISEE UNA KAZI

  pole sana bwana ila ungemuomba msamaha kwanza
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kashaijabutege, si lazima uanzie ukuruta kabla ya kuwa Kanali (hapana sitaki ukanali maana unawajua makanali, Brigedier)
   
 19. K

  Kuntukuntu Member

  #19
  Feb 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Originally Posted by MsandoAlberto:
  Ndugu zangu WanaJF,

  Hatimaye nafsi yangu imekuwa huru. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu huku nikiumia moyoni nafsi yangu sasa imekuwa huru na niko tayari kufanya lile ambalo naamini halitawapendeza wengi lakini ni sahihi kwa maslahi ya Taifa letu.

  Mimi kama Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea na Diwani kwa tiketi ya CHADEMA nimekuwa na wakati mgumu kufanya au kufikia uamuzi huu.

  Kwanza, kabisa ni mategemeo ya wengi kwamba kama Diwani wa Chadema ni lazima nifuate utaratibu ndani ya Chama. Nategemewa kusema au kufikiria vile chama au wanachama wengine wanavyofikiria. Hapana.

  Pili, nategemewa kwamba nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakisaidia chama kukua na kupendwa zaidi (njia zile ambazo wengine wanaona ndizo sahihi ikiwa ni pamoja na kutosema ukweli au kukemea uovu ili mradi chama kitanufaika).

  Tatu, nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakidhoofisha chama cha mapinduzi (CCM). Hata kama ni kwa uonevu au kwa kupindisha ukweli (mara nyingi kinachosemwa dhidi ya CCM ni ukweli na ni mara chache sana watasingiziwa au kuonewa).

  Nne, kama Mwanasheria na Wakili nimtetee na kumlinda mteja wangu. Hilo nitafanya daima.

  Lakini katika hili, nitafanya vile ambavyo nafsi yangu inanituma kufanya na kwa faida ya nchi yangu. Pia vile vile kulinda heshima na fani ya sheria mbele ya jamii.

  Nimeamua kuwashitaki Waheshimiwa Wabunge wafuatao;

  1. Mh. Grace Kiwhelu - Viti Maalum (Moshi Vijijini) - CHADEMA.

  2. Mh. Lucy Owenya - Viti Maalum (Moshi Mjini) - CHADEMA.

  3. Mh. Mary Chitanda - Viti Maalum (Tanga) - CCM.

  Pia katika kesi hizo nimemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

  Waheshimiwa Wabunge hawa ni wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Halmashauri ya Manispaa Arusha.

  Ni ukweli usiopingika kwamba Waheshimiwa hawa ni wateule wa vyombo (organs) vya vyama vya siasa i.e. CHADEMA na CCM. Vyombo hivyo UWT na BAWACHA vilivyowateua haviko ndani ya Halmashauri husika. i.e Hai na Arusha. Vyombo hivyo viko nje ya Halmashauri hizo hivyo hawastahili kuwa wajumbe.

  Sheria husika kuhusu Wabunge wa Viti Maalumu kwa Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa Sheria Namba 7 ya 1987 inasema hivi (kifungu cha 35(e):

  35. Constitution of district councils

  (1) Every district council shall consist of–

  (a) members elected one from each ward in the area of the district council;

  (b) three members appointed by the Minister;

  (c) the Member or Members of Parliament representing constituencies within the area of the district council in the Assembly; and

  (d) such number of women members who are qualified to be elected to the council, being not less than one third of all the members referred to in paragraphs (a), (b) and (c) to be proposed by the political parties represented in the Council in such numbers as shall be proportional to the number of the members of those parties elected to the Council, who the electoral authority shall declare to have been elected into the Council;

  (e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

  Kwa kiswahili naweza kusema Kifungu hicho cha sheria kinasema hivi;

  Mbunge mwingine yoyote ambaye uteuzi wake umeanzia kwenye vyombo vya vyama vya siasa ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya.

  kwa upande wa mamlaka za Majiji sheria husika ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 13 ya Mwaka 2006 kifungu cha 17 ambacho kinaongeza kifungu kidogo (d) kwenye kifungu cha 19 cha Sheria Namba 7/1982 kwamba;

  (d) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

  Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno; nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili.

  Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda Arusha. Alitumia siasa kutoa tafsiri hiyo huku akijua wazi kwamba anakosea.

  Mwanasheria Mkuu alikosea zaidi pale alipoamua kuchukua jukumu la kutoa tafsiri ya sheria badala ya kuiachia mahakama itoe tafsiri hiyo. Sheria zote mbili za Serikali za Mitaa (Namba 7 na 8 za Mwaka 1982) zimetoa utaratibu wa kufuatwa endapo kutakuwa na maswali kuhusu uhalali wa mtu kuwa mjumbe kwenye Halmashauri. Sheria inasema hivi:

  43. Decision of questions as to membership of council

  (1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

  (a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

  (b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

  (c) a person claiming to have been a candidate at the election;

  (d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

  (e) the Attorney-General.

  Mwanasheria Mkuu anatajwa kama mmoja wapo wa watu wanoweza kupeleka maombi mbele ya Hakimu Mkazi ili atoe uamuzi kuhusu uhalali wa ujumbe wa mtu. Hakufanya hivyo badala yake watu wamekufa, mali zimeharibika na wengi wameumizwa. Pia serikali inaingia gharama kuendesha kesi dhidi ya walioandamana.

  Ni sababu zipi zilimfanya Mwanasheria Mkuu asilione hili? Kwa nini alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu Mary Chitanda? tangu uchaguzi ulipomalizika, mvutano ulipojitokeza tarehe 17/12/2010 mpaka tarehe 5/01/2011 Mwanasheria Mkuu hakuwa amepata jibu la nini kifanyike kutatua Mgogoro wa kama Mary Chitanda ni mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha au la?

  Kwa kusoma vifungu hivyo vya sheria hata mtoto wa mwaka wa kwanza wa stashahada ya sheria (Certificate of Law) angeweza kutoa tafsiri sahihi ya Mbunge wa Viti Maalumu anatakiwa aingie kwenye Halmashauri ipi. Ni Halmashauri ile ambayo chombo kilichomchagua kipo. Kama alichaguliwa na UWT Tanga basi anaingia halmashauri ile ambayo UWT Tanga ipo. Kama alichaguliwa na BAWACHA (Baraza la Wanawake Chadema) anaingia pale ambapo baraza hilo lipo. Na sio Halmashauri yoyote nchini!

  Natambua Mods wanaweza kuamua hii mada iende kwenye Jukwaa la Sheria. Napinga mada hii kupelekwa huko kwa sababu siasa ndio ilitumika kufikia tafsiri hiyo na athari zilizojitokeza ni za kisiasa zaidi. Sheria iko wazi.

  CHADEMA waliamua kutumia njia ya Maandamano kupinga kile kilichoonekana ni dhuluma ya wazi na uvunjaji wa sheria mchana kweupe. Walitaka kuonyesha umma ni jinsi gani baadhi ya watu wako tayari kukanyaga sheria za nchi ilimradi tu matakwa yao yatimie. Kilichofuata ni kupigwa nakutawanya kwa nguvu kubwa bila sababu. Labda sababu ilikuwa ni kuficha ukweli.

  Naamini kwamba Mungu ana njia nyingi za kutufanya tuone ukweli na sasa muda umefika. Ni muda wa mahakama kuiangalia Sheria inasemaje na kutoa tafsiri sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa.

  Hili nitalisimamia na kulipigania. Hata kama Chama changu kitaguswa kwa msimamo wangu niko tayari kutetea ukweli na sheria za nchi. Hicho ndicho kiapo changu mbele ya Jaji Mkuu mwaka 2007. Siwezi kukivunja nitakuwa kama wao.

  HITIMISHO.

  1. Waheshimiwa Grace Kiwhelu, Lucy Owenya na Mary Chitanda SI wajumbe halali wa Halmashauri za Hai na Arusha.

  2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (pamoja na Katibu wa Bunge na Tume ya Uchaguzi) walitoa tafsiri ambayo si sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda, Grace Kiwhelu na Lucy Owenya kama wajumbe wa Halmashauri hizo.

  Siasa imetuponza. Maamuzi ambayo yalitolewa kisiasa ili kufanikisha nia na malengo ya kisiasa yamesababisha watu watatu (3) wamepoteza maisha, mali zimeharibiwa na wengi wamebaki vilema.

  Hakukuwa na sababu ya polisi kuzuia maandamano ya amani yaliyopangwa na CHADEMA. Hiyo ilikuwa ni njia ya kuficha uovu ambao sasa utajulikana. Uzembe na ubinafsi vinaimaliza hii nchi.

  Wote tusimame imara na kutetea ukweli. Tuungane kwa pamoja kuwasaidia wananchi wetu masikini ambao sisi wasomi tunachokisema wanakiamini hata kama tunawadanganya.

  MwanaJF yeyote anakaribishwa kuungana nami kama mlalamikaji katika kesi hizo mbili za kuweka kumbukumbu sawa. Kesi dhidi ya Wah. Grace Kihwelu na Lucy Owenya zinafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kesi dhidi ya Mh. Mary Chitanda inafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

  Nawasilisha taarifa.
  Thanx Albert for being honest to yourself in seeking justice. how about adding the Mayorship crisis in Arusha kwenye kesi hiyo ili tujue mbivu na mbichi? otherwise I personnly wish you all the best!!
  Reply Report Post Thanks *

  Albert!!!!!!!!!!!!!!!!!!! unatuabisha......... Huo ndo uadilifu wa wapi? Au uadilifu Wa ki-malice malice!!!!!
   
 20. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa Mkeshaji, natakiwa kufanya nini?

  Kukubali kwamba Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri sahihi?

  Nikubali kwamba wabunge wa viti maalumu wanaweza kuingia kwenye Halmashauri yoyote nchini?

  Kwamba sheria niliyokuwekea hapo juu si sheria na hakuna haja ya kuiheshimu?

  Kama nisipokubali hayo nitakuwa maarufu so let me be. Kama kwa kupinga dhuluma nitapoteza umaarufu acha upotee.

  I will stand and say what i believe to be the truth.

  Karibu tena.
   
Loading...