Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Wewe tunakufahamu. Huna Uchungu huo bali unatafuta UMAARUFU KWA NGUVU KWELI. Ulishindwa DARUSO sasa unataka uraiani. Umaarufu hautafutwi hivyo. Jiangalie mdogo wangu Abert, UTAPOROMOKA!

Duuuuuuuuuuuh kazi kweli kweli!
 
Originally Posted by MsandoAlberto:


Albert!!!!!!!!!!!!!!!!!!! unatuabisha......... Huo ndo uadilifu wa wapi? Au uadilifu Wa ki-malice malice!!!!!

Nimekosea wapi Kuntukuntu? Iweke wazi na mimi nitajibu kwa hoja.

Kwa kusema nawaaibisha peke yake haitoshi. Kwamba kwa kusimamia sheria mimi sio muadilifu na ni malice unakosea. Sasa malice inatoka wapi? Kwamba nataka nichaguliwe viti maalumu au niwe mjumbe wa Halmashauri hizo?

Jenga hoja nitakuelewa na nitakujibu.

Humu ndani nimeona kuna baadhi yenu mnapenda sana nidhamu ya woga. CCM wanakuja na amani na utulivu, nyinyi mnakuja na uadilifu na heshima.

That is not Albert Msando. Its not me.
 
Hao ni Makamanda wa Chadema... Ila naona hawajui nini wanachotaka toka Chadema, iwapo wapo tayali kuona Chadema nayo inapindisha sheria! Hii ni aibu kwa wanaosema wanataka mabadiliko!

Hapana wale ni wana CCM siamini kama ni wanachadema!

Waberoya, salaam.

Jana nimepishana na Hiace njiani imeandikwa kwenye kioo "waberoya". Nikajiuliza hili jina maana yake nini? Hilo tuache.

Humu ndani utapima ni kazi kiasi gani inahitajika kufanyika kuikomboa hii nchi. Watu wanapinga ili mradi wapinge. wapo wanaoamini kazi ya kuitoa CCM madarakani ni rahisi na kuna watu wataifanya kazi hiyo kwa niaba yao.

Mtu anakurupuka, anashindwa kuona the objective, strategy and outcome of a move! Bado anajiita mwanachadema. Ni mwanachadema gani hajui kujipanga wala kutekeleza malengo? watu kama hawa ni mzigo kwa chama na nakuahidi wote wataondoka kama hawatabadilika.

Chadema ni chama kinachojengwa kwa jasho la damu. Watu tunajitolea muda na nguvu zetu ili chama kikue. Na tutaendelea hivyo hivyo. Hakuna siasa za kubembelezana na kupakana mafuta. Kwenye ukweli nitasema na nitasema. Huo ndio uanachama wangu. Sihitaji kupendwa kwa kuficha uzembe, uovu, wizi, dhuluma wala udhaifu. Iwe CCM, iwe CDM, iwe CUF, awe Raisi awe waziri sitamuonea aibu wala kumuogopa.

Mtu anashindwa kujibu hoja nyepesi tu, je sheria zilifuatwa? na sheria nimeziweka hapo. anakurupuka na hoja dhaifu, eti ugomvi na Grace. Huo ni uzushi na uwongo wenye nia ya kupotezea hoja.

Mkuu nakuelewa na watu kama wewe wana support yangu yoote, nataka mabadiliko na mapinduzi sitaki kufuata mkumbo sitaki kuuza utu wangu. Lengo lako na mipango yako ndio haswa vinavyohitajika this time! watu badala ya kupinga basi kwa hoja wanalesta issue za UDSM! na kuleta uongo kibao, mpaka amaridong analazimisha eti wewe ni mimi, nikacheka sana, amekuwa kama makamba kwa matendo yake!!

Lengo lao ni nini?? Msando I believe hata Grace hajawatuma ni kujikomba na wivu tu ndio unaowamaliza!!

Waberoya ni kwa kiswahili kinatokana na neno la kiingereza Berean ((Beh- REE - un), ambao kwenye biblia ni wale 'wachunguza maandiko na wauliza maswali' Berean ni watu waliotoka mji mmoja unaitwa Berea (angalia ramani) uliko Greece karibu na bahari ya meditaranean kwenye biblia wanapatikana ( MATENDO 17:10-12)

berean1.jpg





cheers! keep on smiling and moving

mapambano yanaendelea!
 
Msando,


Naomba unifahamishe yafuatayo kwani mimi sina utaalamu na Sheria,

Je hawa wabunge si walipewa barua na vyama vyao kuwasili katika jimbo flani kama mwakilishi wa jimbo hilo ? Na katika kutafuta tafsiri kwa nini wasishtakiwe wale tu waliopindisha maana/tafsiri ya sheria husika?

Hauni kwamba kwa kuwashtaki hawa wabunge ,watakuja na ushahidi wa barua walizopewa na vyama vyao nahivyo ukahitajika kufungua kesi nyingine ambayo itawahusu waliopindisha tafsiri na hivyo kumislead the whole system .

Je wabunge kama wa CDM wana kosa gani ilhali baada ya Mwanasheria mkuu wa serikali kupindisha tafsiri,na kwa sababu mwanasheria huyo yupo kwenye nafasi ya kutoa tafsiri sahihi..basi wao kama wadau wa siasa wakaamu kumteua Mh Kiwelu na Owenya kwa jimbo la hai na Anna komu jimbo la arusha mjini ?


Ni hayo tu.

Noel,

Nakushukuru kwa kutaka kujua.

Kwanza kabisa 'kushtaki' usitafsiri kama kushtaki mtu kwa kutenda kosa. Wabunge hao hawana kosa ila kitakachozungumzwa mahakamani kinagusa haki yao ya ujumbe kwenye hizo halmashauri ambazo vyama vyao vimewapa barua.

Ni lazima wawe ni party to the application ili haki itendeke. Kama wanaweza kutoa uthibitisho (sio barua) kwamba wameteuliwa kuwa Wabunge na chombo ambacho kimo ndani ya Halmashauri husika basi mahakama itatamka wazi kwa ni halali wao kuwa wajumbe kwenye Halmashauri hiyo. Hili litasaidia kuondoa vurugu na mvutano uliopo Arusha mpaka sasa.
 
Mkuu Engineer, Nakuheshimu sana ila hapa Hujajenga Bali unabomoa, Msando na Grace ni Diwani na Mbunge wa CDM sasa kutumia Maneno kama haya kwa Grace katika Thread iliyoletwa kwa Nia Nzuri na Msando sidhani kama Umetumia Busara yako Vyema

Mtu wa kwanza kumpigia simu na kumjulisha nia yangu njema alikuwa ni Mh. Grace. Anafahamu vizuri sana kwanini nimeamua kusimamia hili. Maneno ya kuchonganisha hayana nafasi kwa sasa na Chadema itaendelea kuwa imara na salama.

Pamoja daima.
 
Tafadhali, ukikurupuka wala huwezi kupata umaarufu unaotemea. Ngoja tuone mwisho wako. Wengi waliojifanya kuapply for general interest kama unavyotaka kufanya wameishia kufirisika kisiasa. Tunajua na wewe itakuwa hivyo!
 
Tafadhali, ukikurupuka wala huwezi kupata umaarufu unaotemea. Ngoja tuone mwisho wako. Wengi waliojifanya kuapply for general interest kama unavyotaka kufanya wameishia kufirisika kisiasa. Tunajua na wewe itakuwa hivyo!

Siwezi kukurupuka. Hiyo sheria umeisoma na iko wazi. Unadhani ni sahihi uchaguliwe Tanga uende ukawakilishe Arusha kwa sababu tu unafanya kazi Arusha?

Na unavyosema 'tunajua' ni wewe na nani Kibunda?

Mwisho, kwa nini usiseme nini kifanyike badala ya kunifundisha woga? Kuhusu kufilisika nitarudia kauli yangu 'masikini hafilisiki'.

Na kusema ukweli sio kutaka umaarufu. Hapa wengi mnakereka kwa sababu ni jambo ambalo litagusa interest za Chama chetu pia. Ingekuwa nimesema namshtaki Mary Chitanda peke yake msingechukua muda kuelewa nini ninachofanya. Mngefurahia moja kwa moja. Hiyo ni kufuata mkumbo. Safari inaendelea.
 
mhhh wewe muheshimiwa diwani priority zao zikoje.?

katika masuala issue za kisheria zinazohitaji attention kichama na kijamii hilo ni la muhimu?
Au hilo ni rahisi
kushinda
Au hilo la hao kina dada na kina mama ni rahisi kukujengea
publicty

Kabla sijakuunga mkono lakini nitapenda kujua kama kabla ya hii nafsi yako imewai kukutuma tena kuwashitaki watu gani wengine kwa manufaa ya Umma au Chama na watanzania


mapaka hapa naona wakati ni jambo sahihi but priority zako ziko wrong na zina kama kamsukumo ka ubinafsi
 
mhhh wewe muheshimiwa diwani priority zao zikoje.?

katika masuala issue za kisheria zinazohitaji attention kichama na kijamii hilo ni la muhimu?
Au hilo ni rahisi kushinda
Au hilo la hao kina dada na kina mama ni rahisi kukujengea publicty

Kabla sijakuunga mkono lakini nitapenda kujua kama kabla ya hii nafsi yako imewai kukutuma tena kuwashitaki watu gani wengine kwa manufaa ya Umma au Chama na watanzania

mapaka hapa naona wakati ni jambo sahihi but priority zako ziko wrong na zina kama kamsukumo ka ubinafsi

Zing,

Mpaka sasa Arusha madiwani wa CDM wamegomea mikutano ya Halmashauri. Bado suala la Mh. Mary Chitanda halijamalizika na maandamano hayajaleta suluhu mpaka sasa. Je tuendelee kusubiri au tupange maandamano mengine? Na kama viongozi wa mkoa wanaendelea na mipango mingine kwa nini nisije na njia mbadala ambayo pia itasaidia kuondoa kasoro iliyopo?

Ni makosa kwa Mary Chitanda kuendelea kuingia kwenye mikutano ya Halmashauri Arusha kama mjumbe. Lakini itakuwa makosa vile vile kwa Grace na Lucy kuendelea kuingia Hai unless wathibitishe kwamba wao wameteuliwa na Kamati Kuu ya Taifa na siyo chombo kilichopo ndani ya eneo la Halmashauri.

Hili ni suala langu binafsi na sioni aibu wala tatizo kulisimamia. Ni lini mtu anatakiwa aanze kutetea au kukemea yale ambayo hayako sawa? Je nilitakiwa nifungue kesi ngapi kabla ya kuwa Diwani?

Tatizo hamtaki kuuliza kabla ya kupost mawazo yenu. Unachofikiria ni kwamba nimewaonea hao wabunge. Kwa hiyo unataka waendelee kuwa wajumbe ili iweje? Na wananachi waliowachagua wanawakilishwa na nani?

Kwa mfano, Arusha kuna wabunge wa viti maalumu watatu wa CCM na wawili wa CDM plus Mbunge wa kuchaguliwa Godbless Lema. Jumla ni wabunge watano (5) kwenye Halmashauri moja!! Hii ni Halmashauri au Bunge dogo la Arusha. Hivi hapa ni nini kinachofanyika? Hai kuna wabunge wawili wa viti maalumu na Mbunge mmoja wa kuchaguliwa Freeman Mbowe. Kuna usawa wa uwakilishi hapa? Wewe unaona ni sawa na kusema kwangu si sawa unaona ni ubinafsi na kutaka umaarufu. Hizo zinazotumika ni fedha za wananchi. Matatizo ambayo hayatatuliwi ni ya wananchi. Acha iwe hivyo. Nitasema.

Karibu tena.
 
Here are the court documents.
 

Attachments

  • Affidavit - Lucy & Grace.docx
    13.8 KB · Views: 61
  • Affidavit - Mary Chitanda.docx
    13.5 KB · Views: 53
  • Certifcate of Urgency.docx
    13.2 KB · Views: 49
  • Certificate of Urgency - Lucy & Grace.docx
    13.3 KB · Views: 84
  • Chamber Summons - Mary Chitanda.docx
    15 KB · Views: 296
  • Chamber Summons - Lucy & Grace Moshi.docx
    13.8 KB · Views: 54
MY TAKE; KAMA KINACHOKUONGOZA KUTENDA HAYA NI MOYO THEN THINK TWICE, MIND YOU ''MOYO NI MDANGANYIFU SANA''(according to the scriptures kitabu cha Mithali japosikumbuki verses) Nakuombea hekima, utashi na busara katika kuitekeleza azma yako.

Freedom is backed up by the essense of God in whatever we do and not self esteem that is backed up by revenge and being appreciated by fellow men. Kila la Kheri
 
MY TAKE; KAMA KINACHOKUONGOZA KUTENDA HAYA NI MOYO THEN THINK TWICE, MIND YOU ''MOYO NI MDANGANYIFU SANA''(according to the scriptures kitabu cha Mithali japosikumbuki verses) Nakuombea hekima, utashi na busara katika kuitekeleza azma yako.

Freedom is backed up by the essense of God in whatever we do and not self esteem that is backed up by revenge and being appreciated by fellow men. Kila la Kheri

Proverbs 4:23

New international Version "Above all else, guard your heart, for it is the wellspring of life".

From English Standard Version "Keep thy heart with all diligence; for out of it are the issues of life"

And Navigator;

Luke 6:45 The good man brings good things out of the good stored up in his heart, and the evil man brings evil things out of the evil stored up in his heart. For out of the overflow of his heart his mouth speaks.

That is the heart.
 
"shitaki mwanasheria mkuu wa serikali wewe", hapo tutakuunga mkono kwa dhati-vinginevyo utakuwa unaruka mzizi wa tatizo wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Zing,


Hili ni suala langu binafsi na sioni aibu wala tatizo kulisimamia. Ni lini mtu anatakiwa aanze kutetea au kukemea yale ambayo hayako sawa? Je nilitakiwa nifungue kesi ngapi kabla ya kuwa Diwani?

Tatizo hamtaki kuuliza kabla ya kupost mawazo yenu. Unachofikiria ni kwamba nimewaonea hao wabunge. Kwa hiyo unataka waendelee kuwa wajumbe ili iweje? Na wananachi waliowachagua wanawakilishwa na nani?
...........

Mwanasheria unaweza kunukuu wapi nimesema umewaonea.

Nilichokuuliza mimi ni priority zako kama katika mambo ya msingi kabisa hilo ni la priorty kwako kwa chama au kwa wananchi.

Pili nikasema isije ikawa ni jambo la haki lakini lina msukumo wa ubinafsi zaidi ndani yake. ndio maana umelipa kipaumbele.

Ulitaka tukuulize nini mkuu ili uhisi kuwa umeeleweka. Mimi nimekupata umeandika kila kitu.

Quote me right nimeandika hivi

mapaka hapa naona wakati ni jambo sahihi but priority zako ziko wrong na zina kama kamsukumo ka ubinafsi
 
HII MADA SAFI SANA NIMEIPENDA ENDEELEEENI MSIVUNJE SHERIA TAFADHALI endelea mwanasheria na injinia wako kamueni tuko tunawasoma hapa .
 
Si suala la umaarufu wala nini, kama wana CDM wanalalamikia Mary Chatanda kushiriki katika baraza la madiwani Arusha kama Mbunge wa kuteuliwa basi waunge mkono kesi hii, ili haki itendeke na si kupinga eti kwa sababu watapoteza Halmashauri ya HAI endapo MSANDO atashinda katika kesi husika. Kama unachukia uonevu chukia pia kuonea, kama unachukia kubaguliwa chukia pia kubagua. Tusiwe tunakasirika na kulalama pale CDM inapoonewa lakini inapoonea tukae kimya. Tusimamie haki na si kusimamia chama.

TAADHALI KWA WAKILI MSANDOALBERTO (wewe ni mwanasiasa wengine sisi ni wanaharakati hatuna chama bali tunasupport chama tunacho amini kitaleta mabadiliko yanayotakiwa hapa nchini) Kumbuka CCM wanampango wa kuvunja Baraza la Madiwani Katika JIJI la ARUSHA na kuunda TUME, hivyo kesi yako hutomkomoa MARY CHATANDA WALA CCM, lakini kwa Upande wa HAI mjini ukishinda kesi utakikomoa chama chako na wanachama wenzako LUCY OWENYA na LUCY KIWELU. Je utaweza kupambana kama ZITTO ndani ya chama? yaani wewe uwe upande mwingine na CDM upande mwingine katika mapambano hayo? Jifunze kwa yanayomkuta ZITTO lakini ukiwa tayari kwa lolote GO ON.
 
Nakuunga mkono alberto, watu hawaeliwi unachokigania kwa sasa ila baada ya matokeo ya kesi wataelewa, so far watu wameshindwa kukudefeat kwa wamebaki kutoa mitusi, wakijifanya ni wana cdm kumbe wengine ni ccm. Kila la kheri kaka
 
"shitaki mwanasheria mkuu wa serikali wewe", hapo tutakuunga mkono kwa dhati-vinginevyo utakuwa unaruka mzizi wa tatizo wewe!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Nsimba, wote wanakuwa parties to the case. So na yeye ni mmoja wao.
 
Grace Kiwelu sio mLucy Kiwelu,rekebisha hiyo mwanaharakati mwenzangu teheeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom