Nawashtaki Grace Kiwhelu, Lucy Owenya, Mary Chitanda na Mwanasheria Mkuu

Msando kuwa mkweli kwanini napokutajia namalok sokoine umuongeze hautaki , au umeshapiga mahesabu kesi uliyoivungua kupinga matokeo ya moshi vijijini una nafasi kubwa ya kushinda sasa unataka kiwelu arudi moshi vijijini ili uchaguzi ukirudiwa ujihakikishie ushindi kwa sababu uchaguzi uliopita ulibwagwa kwa kura moja:A S 13:

Carefree,

Umenimind bure kamanda. Sijakataa kumuongeza Namalok. Kabla sijakujibu nilikuwa namtafuta Mbunge wa Arusha ili niconfirm kuhusu Namalok kwani sijasikia wakimlalamikia mpaka ulipsema wewe. Kama umeona nilikugongea ka thanks muda fulani niliposoma post yako.

Kuhusu Mohi vijijini unajua kabisa walichofanya ila tutaona mwisho wake.
 
Ndugu zangu WanaJF,

Hatimaye nafsi yangu imekuwa huru. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu huku nikiumia moyoni nafsi yangu sasa imekuwa huru na niko tayari kufanya lile ambalo naamini halitawapendeza wengi lakini ni sahihi kwa maslahi ya Taifa letu.

Mimi kama Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea na Diwani kwa tiketi ya CHADEMA nimekuwa na wakati mgumu kufanya au kufikia uamuzi huu.

Kwanza, kabisa ni mategemeo ya wengi kwamba kama Diwani wa Chadema ni lazima nifuate utaratibu ndani ya Chama. Nategemewa kusema au kufikiria vile chama au wanachama wengine wanavyofikiria. Hapana.

Pili, nategemewa kwamba nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakisaidia chama kukua na kupendwa zaidi (njia zile ambazo wengine wanaona ndizo sahihi ikiwa ni pamoja na kutosema ukweli au kukemea uovu ili mradi chama kitanufaika).

Tatu, nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakidhoofisha chama cha mapinduzi (CCM). Hata kama ni kwa uonevu au kwa kupindisha ukweli (mara nyingi kinachosemwa dhidi ya CCM ni ukweli na ni mara chache sana watasingiziwa au kuonewa).

Nne, kama Mwanasheria na Wakili nimtetee na kumlinda mteja wangu. Hilo nitafanya daima.

Lakini katika hili, nitafanya vile ambavyo nafsi yangu inanituma kufanya na kwa faida ya nchi yangu. Pia vile vile kulinda heshima na fani ya sheria mbele ya jamii.

Nimeamua kuwashitaki Waheshimiwa Wabunge wafuatao;

1. Mh. Grace Kiwhelu - Viti Maalum (Moshi Vijijini) - CHADEMA.

2. Mh. Lucy Owenya - Viti Maalum (Moshi Mjini) - CHADEMA.

3. Mh. Mary Chitanda - Viti Maalum (Tanga) - CCM.

Pia katika kesi hizo nimemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Waheshimiwa Wabunge hawa ni wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Halmashauri ya Manispaa Arusha.

Ni ukweli usiopingika kwamba Waheshimiwa hawa ni wateule wa vyombo (organs) vya vyama vya siasa i.e. CHADEMA na CCM. Vyombo hivyo UWT na BAWACHA vilivyowateua haviko ndani ya Halmashauri husika. i.e Hai na Arusha. Vyombo hivyo viko nje ya Halmashauri hizo hivyo hawastahili kuwa wajumbe.

Sheria husika kuhusu Wabunge wa Viti Maalumu kwa Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa Sheria Namba 7 ya 1987 inasema hivi (kifungu cha 35(e):

35. Constitution of district councils

(1) Every district council shall consist of–

(a) members elected one from each ward in the area of the district council;

(b) three members appointed by the Minister;

(c) the Member or Members of Parliament representing constituencies within the area of the district council in the Assembly; and

(d) such number of women members who are qualified to be elected to the council, being not less than one third of all the members referred to in paragraphs (a), (b) and (c) to be proposed by the political parties represented in the Council in such numbers as shall be proportional to the number of the members of those parties elected to the Council, who the electoral authority shall declare to have been elected into the Council;

(e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Kwa kiswahili naweza kusema Kifungu hicho cha sheria kinasema hivi;

Mbunge mwingine yoyote ambaye uteuzi wake umeanzia kwenye vyombo vya vyama vya siasa ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya.

kwa upande wa mamlaka za Majiji sheria husika ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 13 ya Mwaka 2006 kifungu cha 17 ambacho kinaongeza kifungu kidogo (d) kwenye kifungu cha 19 cha Sheria Namba 7/1982 kwamba;

(d) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno; nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili.

Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda Arusha. Alitumia siasa kutoa tafsiri hiyo huku akijua wazi kwamba anakosea.

Mwanasheria Mkuu alikosea zaidi pale alipoamua kuchukua jukumu la kutoa tafsiri ya sheria badala ya kuiachia mahakama itoe tafsiri hiyo. Sheria zote mbili za Serikali za Mitaa (Namba 7 na 8 za Mwaka 1982) zimetoa utaratibu wa kufuatwa endapo kutakuwa na maswali kuhusu uhalali wa mtu kuwa mjumbe kwenye Halmashauri. Sheria inasema hivi:

43. Decision of questions as to membership of council

(1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

(a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

(b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

(c) a person claiming to have been a candidate at the election;

(d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

(e) the Attorney-General.

Mwanasheria Mkuu anatajwa kama mmoja wapo wa watu wanoweza kupeleka maombi mbele ya Hakimu Mkazi ili atoe uamuzi kuhusu uhalali wa ujumbe wa mtu. Hakufanya hivyo badala yake watu wamekufa, mali zimeharibika na wengi wameumizwa. Pia serikali inaingia gharama kuendesha kesi dhidi ya walioandamana.

Ni sababu zipi zilimfanya Mwanasheria Mkuu asilione hili? Kwa nini alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu Mary Chitanda? tangu uchaguzi ulipomalizika, mvutano ulipojitokeza tarehe 17/12/2010 mpaka tarehe 5/01/2011 Mwanasheria Mkuu hakuwa amepata jibu la nini kifanyike kutatua Mgogoro wa kama Mary Chitanda ni mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha au la?

Kwa kusoma vifungu hivyo vya sheria hata mtoto wa mwaka wa kwanza wa stashahada ya sheria (Certificate of Law) angeweza kutoa tafsiri sahihi ya Mbunge wa Viti Maalumu anatakiwa aingie kwenye Halmashauri ipi. Ni Halmashauri ile ambayo chombo kilichomchagua kipo. Kama alichaguliwa na UWT Tanga basi anaingia halmashauri ile ambayo UWT Tanga ipo. Kama alichaguliwa na BAWACHA (Baraza la Wanawake Chadema) anaingia pale ambapo baraza hilo lipo. Na sio Halmashauri yoyote nchini!

Natambua Mods wanaweza kuamua hii mada iende kwenye Jukwaa la Sheria. Napinga mada hii kupelekwa huko kwa sababu siasa ndio ilitumika kufikia tafsiri hiyo na athari zilizojitokeza ni za kisiasa zaidi. Sheria iko wazi.

CHADEMA waliamua kutumia njia ya Maandamano kupinga kile kilichoonekana ni dhuluma ya wazi na uvunjaji wa sheria mchana kweupe. Walitaka kuonyesha umma ni jinsi gani baadhi ya watu wako tayari kukanyaga sheria za nchi ilimradi tu matakwa yao yatimie. Kilichofuata ni kupigwa nakutawanya kwa nguvu kubwa bila sababu. Labda sababu ilikuwa ni kuficha ukweli.

Naamini kwamba Mungu ana njia nyingi za kutufanya tuone ukweli na sasa muda umefika. Ni muda wa mahakama kuiangalia Sheria inasemaje na kutoa tafsiri sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa.

Hili nitalisimamia na kulipigania. Hata kama Chama changu kitaguswa kwa msimamo wangu niko tayari kutetea ukweli na sheria za nchi. Hicho ndicho kiapo changu mbele ya Jaji Mkuu mwaka 2007. Siwezi kukivunja nitakuwa kama wao.

HITIMISHO.

1. Waheshimiwa Grace Kiwhelu, Lucy Owenya na Mary Chitanda SI wajumbe halali wa Halmashauri za Hai na Arusha.

2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (pamoja na Katibu wa Bunge na Tume ya Uchaguzi) walitoa tafsiri ambayo si sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda, Grace Kiwhelu na Lucy Owenya kama wajumbe wa Halmashauri hizo.

Siasa imetuponza. Maamuzi ambayo yalitolewa kisiasa ili kufanikisha nia na malengo ya kisiasa yamesababisha watu watatu (3) wamepoteza maisha, mali zimeharibiwa na wengi wamebaki vilema.

Hakukuwa na sababu ya polisi kuzuia maandamano ya amani yaliyopangwa na CHADEMA. Hiyo ilikuwa ni njia ya kuficha uovu ambao sasa utajulikana. Uzembe na ubinafsi vinaimaliza hii nchi.

Wote tusimame imara na kutetea ukweli. Tuungane kwa pamoja kuwasaidia wananchi wetu masikini ambao sisi wasomi tunachokisema wanakiamini hata kama tunawadanganya.

MwanaJF yeyote anakaribishwa kuungana nami kama mlalamikaji katika kesi hizo mbili za kuweka kumbukumbu sawa. Kesi dhidi ya Wah. Grace Kihwelu na Lucy Owenya zinafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kesi dhidi ya Mh. Mary Chitanda inafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
kwanza bwana mdogo mheshimiwa wakili nkupongeza kwa kuukwaa udiwani kupitia chama chadema nitawasiliana na wewe muda si mrefu natumai safari yako tokea pale mwananyamala ss ukiwa na mhshimiwa fulani aliyeko mjengoni kwa sasa imeanza nawe siku moja utatua usiofie mchakachue hy waziri sasa umekomaa kisiasa ruksa mapambano, hoja zako ni nzito lakini wanachadema wenzio watakuelewa kweli lakini sheria haina rafiki wala undugu naunga mkono hoja.
 
Carefree,

Umenimind bure kamanda. Sijakataa kumuongeza Namalok. Kabla sijakujibu nilikuwa namtafuta Mbunge wa Arusha ili niconfirm kuhusu Namalok kwani sijasikia wakimlalamikia mpaka ulipsema wewe. Kama umeona nilikugongea ka thanks muda fulani niliposoma post yako.

Kuhusu Mohi vijijini unajua kabisa walichofanya ila tutaona mwisho wake.
Hili ndiyo walinza kulilalamikia madiwani cdm na wabunge. wakaeleweshwe... Eti diwani wa kuteuliwa yuko huru kuchangua manispaa inaelekea waliliziaka na maelezo hayo ndipo likajitokea swala na Mary Chitanda kwa maelezo yako itabidi ufanye inabidi umjulishe maana hakuwa mkazi wa Arusha kwa zaidi ya miaka 5...
 
Sasa maandamano yale yamemaliza vip mgogoro wa Umeya wa Arusha? Je unaweza kukiri sasa kuwa ku-opt kufanya maandamano badala ya kwenda makamani haukuwa uamuzi sahihi kwa mazingira ya suala husika?

Jibu la swali lako,
click this link:
Maandamano ya chadema yanayoendelea sasa ambayo yameanza jana huko Mwanza, leo yapo Geita na yanatarajia kuendelea maeneo mengine nchini yamemaliza matatizo yanayotajwa kubeba ujumbe wa maandamano hayo? Ufisadi, Dowans, Mgawo wa Umeme na Maisha magumu kwa watanzania yamekwisha? Au unatarajia yataisha ndani ya siku tisa za maandamano hayo?
Think!
 
Sio wazo baya na pia mimi si mwanasheria lakini;

CCM walitumia udhaifu wa sheria kumpeleka Marry Arusha; Kwa tafsiri ya Mwanasheria Mkuu Chadema pia watumia udhaifu huo huo;

Ningekuwa mimi nadhani kwanza ninge mshitaki Mwanasheria Mkuu kwa Kesi ya Kikatiba kwa kutaka Marekebisho yatakayoekeleza kwa Kina Scope nzima ya wabunge wa viti maalumu;
Kuwashitaki Wabunge wenyewe ambao wao waliagizwa na vyama vyao kwa barua na sidhani kama walikuwa na option nadhani utanakosa uzito, labda ungewashitaki CCM na Chadema kwa kutumia sheria vibaya

Lingine kubwa: Sina hakika kama pia umepata kushauriana na viongozi wako wa CDM mkoa au Taifa pengine na maoni yao; Mara nyingine mtu anaweza hasifanikiwe sana kwa sababu tu ya methodogy unayotumia.

Zaidi ya hapo kila la kheri

Mkuu thanks kwa kuliona hilo hapo kwenye red.
Wale wote waliokuwa wananibeza kama watafuatilia michango yangu ndani ya thread hii (achilia mbali majibu ya mabezo), hiki ndicho nilichokuwa nasisitiza mimi. Bahati mbaya sikukiandika katika tone wanayoitaka walionibeza. Mwishowe niliishia kubezwa na kutopatiwa majawabu sahihi kwa nilichouliza/kushauri. Yote kwa yote nasimama kwenye hilo.
 
Msando, inawezekana Dhamira yako ni kumDisqualify Chitanda kwa kuona kuna Nguvu zaidi za Hoja za Kisheria, kule Kuwashtaki kina Kihwelu na Owenya ikawa ni just a Tactical Legal Ploy to Camouflage your Actual intent. Unfortunately, you are Most probably Doomed to be Entangled in The Confusing Quamire of Lumpen Party Politics. Hivi kweli Watu walifanywa waandamane Hadi Kufa kwa ajili ya Tafsiri tu ya Origin ya Uteuzi wa Chitanda?! Definitely Origin ya uteuzi ni Pale Uteuzi wenyewe Ulipofanyika, km Milipuko ya Mabomu ya G/Mboto ni yale Maghala ya Jeshi na Sio yalikotengenezwa Mabomu yenyewe. Masuala ya ndani ya Chama juu ya Namna ya kufikia uteuzi wao, its their Business, Sheria nadhani itaangalia zaidi Chombo kilichofanya Uteuzi huo. Na si Wote walianza mchakato hio Ngazi za Mkoa, Km Mama Anna Abdallah hakupigiwa kura za Uteuzi popote Bali ameteuliwa Moja kwa Moja na NEC, sasa Nae kwa Tafsiri yako ataingia kwenye Halmashauri ya Wilaya ipi? Naweza kupewa mwanga Zaidi?
 
Carefree,

Umenimind bure kamanda. Sijakataa kumuongeza Namalok. Kabla sijakujibu nilikuwa namtafuta Mbunge wa Arusha ili niconfirm kuhusu Namalok kwani sijasikia wakimlalamikia mpaka ulipsema wewe. Kama umeona nilikugongea ka thanks muda fulani niliposoma post yako.

Kuhusu Mohi vijijini unajua kabisa walichofanya ila tutaona mwisho wake.

Msendo ur the Man, i had a dought lakini umeweza ku i clear it, pls GO, hata sijui kwa nini unazidi kupoteza muda pls GO
 
Nilisema kwenye hii thread ni mtazamaji. Bado natazama.

Anna Moulid Komu vipi mbona hajashitakiwa
 
Malengo ya CHADEMA ni kupindisha sheria, kukiuka sheria na kuvunja sheria? Nani anatakiwa kutilia mashaka uanachama wa mwenzake? Ningetegemea kama mwanachadema uwe mstari wa mbele kupigania haki na ukweli. Kilichotokea Arusha hakivumiliki na lazima kipingwe kwa nguvu zote.

zaidi, soma maelezo yangu na utoe tafsiri yako. Au toa msimamo wako. Msimamo wangu uko wazi. Wabunge hao sio wajumbe wa halmashauri hizo. Nitausimamia msimamo wangu na uanachama wanguu utabaki.

Mwisho, unaandamana nchi nzima ili iweje kama hutaki haki itendeke? wewe ni mwanachama wa kipekee kabisa. Ukishaandamana halafu? Kwa hiyo kwa sababu tumepanga kuandamana basi tusitafute haki mahakamani? Sitakushangaa. Ukisoma nilichosema utaelimika na kuelewa nini cha kufanya.

hAPA HATUZUNGUMZII UANACHAMA NI SHERIA INASEMAJE? ENDELEA MKUU TUMEKUELEWA VIZURI SANA NA FIKRA ZAKO ZIDUMU, USIACHE WAHUNI WACHACHE WAFINYANGE SHERIA UKU UKIJUA SHERIA.
 
MsandoAlberto

Nimekusoma tafadhali sana endelea na nia yako njema.
 
mkuu ngongo .... ulitujuza kwamba wale madiwani waliofukuzwa CDM watafungua kesi .... hebu tujuze wamefikia wapi na mkondo wa sheria
 
Ndugu zangu WanaJF,

Hatimaye nafsi yangu imekuwa huru. Baada ya kutafakari kwa muda mrefu huku nikiumia moyoni nafsi yangu sasa imekuwa huru na niko tayari kufanya lile ambalo naamini halitawapendeza wengi lakini ni sahihi kwa maslahi ya Taifa letu.

Mimi kama Mwanasheria na Wakili wa Kujitegemea na Diwani kwa tiketi ya CHADEMA nimekuwa na wakati mgumu kufanya au kufikia uamuzi huu.

Kwanza, kabisa ni mategemeo ya wengi kwamba kama Diwani wa Chadema ni lazima nifuate utaratibu ndani ya Chama. Nategemewa kusema au kufikiria vile chama au wanachama wengine wanavyofikiria. Hapana.

Pili, nategemewa kwamba nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakisaidia chama kukua na kupendwa zaidi (njia zile ambazo wengine wanaona ndizo sahihi ikiwa ni pamoja na kutosema ukweli au kukemea uovu ili mradi chama kitanufaika).

Tatu, nitende na niseme yale ambayo kwa njia moja au nyingine yatakidhoofisha chama cha mapinduzi (CCM). Hata kama ni kwa uonevu au kwa kupindisha ukweli (mara nyingi kinachosemwa dhidi ya CCM ni ukweli na ni mara chache sana watasingiziwa au kuonewa).

Nne, kama Mwanasheria na Wakili nimtetee na kumlinda mteja wangu. Hilo nitafanya daima.

Lakini katika hili, nitafanya vile ambavyo nafsi yangu inanituma kufanya na kwa faida ya nchi yangu. Pia vile vile kulinda heshima na fani ya sheria mbele ya jamii.

Nimeamua kuwashitaki Waheshimiwa Wabunge wafuatao;

1. Mh. Grace Kiwhelu - Viti Maalum (Moshi Vijijini) - CHADEMA.

2. Mh. Lucy Owenya - Viti Maalum (Moshi Mjini) - CHADEMA.

3. Mh. Mary Chitanda - Viti Maalum (Tanga) - CCM.

Pia katika kesi hizo nimemuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Waheshimiwa Wabunge hawa ni wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai na Halmashauri ya Manispaa Arusha.

Ni ukweli usiopingika kwamba Waheshimiwa hawa ni wateule wa vyombo (organs) vya vyama vya siasa i.e. CHADEMA na CCM. Vyombo hivyo UWT na BAWACHA vilivyowateua haviko ndani ya Halmashauri husika. i.e Hai na Arusha. Vyombo hivyo viko nje ya Halmashauri hizo hivyo hawastahili kuwa wajumbe.

Sheria husika kuhusu Wabunge wa Viti Maalumu kwa Halmashauri za Wilaya kwa mujibu wa Sheria Namba 7 ya 1987 inasema hivi (kifungu cha 35(e):

35. Constitution of district councils

(1) Every district council shall consist of–

(a) members elected one from each ward in the area of the district council;

(b) three members appointed by the Minister;

(c) the Member or Members of Parliament representing constituencies within the area of the district council in the Assembly; and

(d) such number of women members who are qualified to be elected to the council, being not less than one third of all the members referred to in paragraphs (a), (b) and (c) to be proposed by the political parties represented in the Council in such numbers as shall be proportional to the number of the members of those parties elected to the Council, who the electoral authority shall declare to have been elected into the Council;

(e) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Kwa kiswahili naweza kusema Kifungu hicho cha sheria kinasema hivi;

Mbunge mwingine yoyote ambaye uteuzi wake umeanzia kwenye vyombo vya vyama vya siasa ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya.

kwa upande wa mamlaka za Majiji sheria husika ni Sheria Namba 8 ya Mwaka 1982 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 13 ya Mwaka 2006 kifungu cha 17 ambacho kinaongeza kifungu kidogo (d) kwenye kifungu cha 19 cha Sheria Namba 7/1982 kwamba;

(d) any other member of parliament whose nomination originated from organs of political parties within the area of jurisdiction of the district council.

Hiyo ndiyo sheria na tafsiri nyingine yoyote SIO SAHIHI kutokana na uelewa wangu. Kwa mtu ambaye sio msomi wa sheria tafuta maana ya maneno; nomination, origin, organ, political party, within, area of jurisdiction, district council. Halafu unganisha upate sentensi kamili.

Mwanasheria Mkuu alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda Arusha. Alitumia siasa kutoa tafsiri hiyo huku akijua wazi kwamba anakosea.

Mwanasheria Mkuu alikosea zaidi pale alipoamua kuchukua jukumu la kutoa tafsiri ya sheria badala ya kuiachia mahakama itoe tafsiri hiyo. Sheria zote mbili za Serikali za Mitaa (Namba 7 na 8 za Mwaka 1982) zimetoa utaratibu wa kufuatwa endapo kutakuwa na maswali kuhusu uhalali wa mtu kuwa mjumbe kwenye Halmashauri. Sheria inasema hivi:

43. Decision of questions as to membership of council

(1) All questions arising as to whether a person has been lawfully elected a member or not, or the right of any person to be or remain a member of a district council, shall be determined by a court of a Resident Magistrate upon the application of or election petition presented by, any one or more of the following persons, namely–

(a) a person who lawfully voted or had a right to vote at the election to which the application or election petition relates;

(b) a person claiming to have had a right to be nominated or elected at an election;

(c) a person claiming to have been a candidate at the election;

(d) a person claiming to have a right to be or remain a member of a district council;

(e) the Attorney-General.

Mwanasheria Mkuu anatajwa kama mmoja wapo wa watu wanoweza kupeleka maombi mbele ya Hakimu Mkazi ili atoe uamuzi kuhusu uhalali wa ujumbe wa mtu. Hakufanya hivyo badala yake watu wamekufa, mali zimeharibika na wengi wameumizwa. Pia serikali inaingia gharama kuendesha kesi dhidi ya walioandamana.

Ni sababu zipi zilimfanya Mwanasheria Mkuu asilione hili? Kwa nini alitoa tafsiri isiyo sahihi kuhusu Mary Chitanda? tangu uchaguzi ulipomalizika, mvutano ulipojitokeza tarehe 17/12/2010 mpaka tarehe 5/01/2011 Mwanasheria Mkuu hakuwa amepata jibu la nini kifanyike kutatua Mgogoro wa kama Mary Chitanda ni mjumbe wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha au la?

Kwa kusoma vifungu hivyo vya sheria hata mtoto wa mwaka wa kwanza wa stashahada ya sheria (Certificate of Law) angeweza kutoa tafsiri sahihi ya Mbunge wa Viti Maalumu anatakiwa aingie kwenye Halmashauri ipi. Ni Halmashauri ile ambayo chombo kilichomchagua kipo. Kama alichaguliwa na UWT Tanga basi anaingia halmashauri ile ambayo UWT Tanga ipo. Kama alichaguliwa na BAWACHA (Baraza la Wanawake Chadema) anaingia pale ambapo baraza hilo lipo. Na sio Halmashauri yoyote nchini!

Natambua Mods wanaweza kuamua hii mada iende kwenye Jukwaa la Sheria. Napinga mada hii kupelekwa huko kwa sababu siasa ndio ilitumika kufikia tafsiri hiyo na athari zilizojitokeza ni za kisiasa zaidi. Sheria iko wazi.

CHADEMA waliamua kutumia njia ya Maandamano kupinga kile kilichoonekana ni dhuluma ya wazi na uvunjaji wa sheria mchana kweupe. Walitaka kuonyesha umma ni jinsi gani baadhi ya watu wako tayari kukanyaga sheria za nchi ilimradi tu matakwa yao yatimie. Kilichofuata ni kupigwa nakutawanya kwa nguvu kubwa bila sababu. Labda sababu ilikuwa ni kuficha ukweli.

Naamini kwamba Mungu ana njia nyingi za kutufanya tuone ukweli na sasa muda umefika. Ni muda wa mahakama kuiangalia Sheria inasemaje na kutoa tafsiri sahihi ili kuweka kumbukumbu sawa.

Hili nitalisimamia na kulipigania. Hata kama Chama changu kitaguswa kwa msimamo wangu niko tayari kutetea ukweli na sheria za nchi. Hicho ndicho kiapo changu mbele ya Jaji Mkuu mwaka 2007. Siwezi kukivunja nitakuwa kama wao.

HITIMISHO.

1. Waheshimiwa Grace Kiwhelu, Lucy Owenya na Mary Chitanda SI wajumbe halali wa Halmashauri za Hai na Arusha.

2. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (pamoja na Katibu wa Bunge na Tume ya Uchaguzi) walitoa tafsiri ambayo si sahihi kuhusu uhalali wa Mary Chitanda, Grace Kiwhelu na Lucy Owenya kama wajumbe wa Halmashauri hizo.

Siasa imetuponza. Maamuzi ambayo yalitolewa kisiasa ili kufanikisha nia na malengo ya kisiasa yamesababisha watu watatu (3) wamepoteza maisha, mali zimeharibiwa na wengi wamebaki vilema.

Hakukuwa na sababu ya polisi kuzuia maandamano ya amani yaliyopangwa na CHADEMA. Hiyo ilikuwa ni njia ya kuficha uovu ambao sasa utajulikana. Uzembe na ubinafsi vinaimaliza hii nchi.

Wote tusimame imara na kutetea ukweli. Tuungane kwa pamoja kuwasaidia wananchi wetu masikini ambao sisi wasomi tunachokisema wanakiamini hata kama tunawadanganya.

MwanaJF yeyote anakaribishwa kuungana nami kama mlalamikaji katika kesi hizo mbili za kuweka kumbukumbu sawa. Kesi dhidi ya Wah. Grace Kihwelu na Lucy Owenya zinafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kesi dhidi ya Mh. Mary Chitanda inafunguliwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Nawasilisha taarifa.
Go sunny go for a JUST COURSE!!
 
Najua CHADEMA iliamua kuwapeleka Owenya na wengine Hai baada ya kuona uhuni wa CCM kwa Arusha. Binafsi nakushauri ulie na tafsiri potofu ya mwanasheria mkuu wa serikali. Baada ya kushinda hiyo kesi basi mambo mengine yataenda sawa maana yatarekebishwa tu!

Naamini Chadema haina tatizo katika hilo ila tatizo ni hiyo tafsiri ya mwanasheria mkuu wa serikali. Fungua mashitaka ya kikatiba au vinginevyo uonavyo bila kuwapotezea muda waheshimiwa wabunge wetu wa Chadema! Am not a lawyer by the way lakini nimeshauri kama raia tu!

Wasu,uko sahihi kabisa! Kwanza Huyu diwani mwanasheria hinyo basi alie na Warema ambaye ndo mtafsiri mkuu wa sheria za nchi na tunajua kuwa alifanyaivo ili kumlinda Chitanda aliyevuruga ule uchaguzi wa meya wa SISIEM wa H/shauri ya ARUSHA!
 
<br />
<br />

Mahakama ilitoa uamuzi na kutupilia mbali kwa kisingizio kwamba muda wa kufungua madai umepita. Sipo Arusha ila nitajitahidi kuweka maamuzi ya mahakama hapa kwa taarifa.
 
Msando,
This is good for your career, push it up, dont give up. Haya mambo ya Udiwani na CDM ni ya msimu tu, nadhani umeyaona majibu ya wanachama wenzio. Siasa upepo waweza kuhama na CDM ikawa kama TLP , NCCR au CUF. Nani alijua Cuf watakuja kuwa hivi?
So jenga jina kwenye professional yako, siasa egesha tu kiaina.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom