Nawashangaa wanaoichukia CCM!! Hebu soma hapa.

Nawashangaa wanaoichukia CCM!! Hebu soma hapa.

Malyenge

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
6,658
Reaction score
3,664
Imekuwa ni kawaida sana kwa kizazi cha sasa kilichozaliwakati yqa mwaka 1990 na kuja huku mbele miaka ya 2000. Imekuwa ni kawaida sanakusikia mabezo mengi tu kwamba CCM ni chama kisichofaa kuongoza. Ni kawaidausikia kwamba mwaka 2015 CCM ndo itakuwa mwisho wake. Imekuwa ni kawaida sanakusikia watu wakiombea na hata kuomba dua mbaya (na si dua nzuri) kwamba CCM kipate mikosi ilikionekane hakifai mbele za watu.
CCM kimekuwa kikibebeshwa lawama na mizigo kisichostahilikuibeba……Chama Cha Mapinduzi ni chama kinachotawala yaani ni chamakilichoshinda na kuunda serikali. Kazi ya Chama Cha Mapinduzi ni kutengenezasera ili zitekelezwe na serikali. Kinapotengeneza sera kwa mfano, sera yaajira, kasha anayezisimamia sera hizo ni serikali (serikali ni pamoja na watuwasio na mrengo wa chama chochote ama walio na mrengo wa chama tawala na vyamavya upinzani). Sera za Chama Cha Mapinduzi hazibagui maana CCM kinaamini “Binadamu wote ni sawa na Kila Mtuanastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake…..”
Sasa utaona mtu aliyepewa mamlaka ya kuismamia utoaji waajira akafanya hivyo lakini kwa upendeleo wa kikabila ama kindugu lawama zotezinakwenda kwa CCM!!!!!Ama mtu akapewa taasisi aiendeshe lakini akawa na tamaa (greed)akafuja mali taasisi ikafa lawama zinakwenda CCM!!! Ama utakuta serikali inakamata wahujumuuchumi inawapeleka mahakamani kesiinaunguruma miaka kadhaa lakini watu wanaachiwa huru serikali inakata rufaawatu hawataki ikate rufaa. Hatimaye kesi inashindwa kuendelea kwa sababu yakelele za watu lakini lawama zinakwenda Chama Cha Mapinduzi!!!!!!!
CCM kinatengeneza sera za kujenga miundo mbinu ili wananchiwake wapate maendeleo yao lakini utakuta watu badala ya kutumia miundo mbinuhiyo katika kujiletea maendeleo watu wanatumia simu kutukanana ama kutukanawengine na hasa viongozi wakuu wanaosimamia nchi na hasa walioleta maendeleohayo ya miundombinu ya mawasiliano. Lakini lawama zote zinakwenda CCM!!!!
Watu walikuwa wanatumia masaa kumi na mbili kutoka Bukobakwenda Mutukula kiasi cha kilometa 80 tu lakini sasa wanatumia dakika 80 lakinilawama zinakwenda CCM!!! Watu walikuwa wanatumia usiku kucha kuanzia saa kumina moja jioni kwenda Tanga lakini sasa hivi ni masaa manne na nusu hadi matanotu lakini bado lawama zinakwenda CCM!!!! Zamani nchi ilikuwa giza tupu hasanyakati za usiku lakini sasa nchi inang’aa na mataa usiku (mataa ya TANESCO,SOLA, TOCHI NA TAA ZA KICHINA NK). Mpaka muuza mkaa antumia taa!!!! Lakinilawama zote zinakwenda CCM!!!!!
Sera za nchi zilizowekwa na CCM kwamba kila raia mwenye umriunaokubalika kisheria anayohaki ya kupiga na kupigiwa kura lakini watuwanashindwa kuelewa haki hiyo. Wanajichanganya kwamba haki ya kupigiwa kuramaana yake kushinda uchaguzi!!! Wakishindwa lawama zinakwenda CCM wakatiwaliopiga kura si wanachama wa CCM pekee……..
Watanzania tukumbuke tulikotoka…….Tuwaelimishe vijana wasasa wasiojua dhiki na taabu za maisha…Wanaodhani haki yako unaweza kuipata kwakutukana watu……Mimi niwaulize hata hao baba za watoto hao (au hata watu wazima)wanaoshabikia anguko la CHAMAkilicholeta maendeleo haya tuliyo nayo sasa. Kwamba motto wako akija leo hiiakakuomba pesa ya shule kwa nguvu na matusi juu, je utampa? Na hata kama utampautampa ukiwa na furaha moyoni? Au motto wako aje kukulaumu wewe mzazi kwambaumesababisha umaskini katika familia wakati huohuo anataka umwandikishe awemrithi wa mali zako……..!!!! Inaingia akilini kweli????
Msitulazimishe kujiunga na vyama vyenye tabia hiiniliyoitaja hapa juu na wala si lazima wote tuwe mashabiki wa vyama vya siasa,Maana siasa haikufanyi ufaulu Engineering, Information Technology, Accountancy,Sociology ama taaluma zinginezo bali taaluma itabaki kuwa taaluma na siasaitabaki kuwa siasa. Wengine hawahitaji kuwa wanasiasa….Wanataka kuwa raia wakawaida wajiajiri na wajiajiri. Sera za ajira na kujiajiri ziko wazi na walaserikali ya CCM haijazizuia ama kubagua watu. Kama una mtaji wako mwagamabilioni yako ujenge viwanda na CCM inatakulinda kwa sera zake. Ukikutana navikwazo inabidi kujiuliza ni wapi umekwama na si kuanza kulaumu.
Ni wapi CCM inakataza wawekezaji wazawa wasiwekeze?
Ni wapi CCM inakataza wafuasi wa vyama vya upinzaniwasiajiriwe?
Ni wapi CCM inazuia wananchi kujiunga na vyama vya siasa?
Ni wapi CCM inazuia vyama vya upinzani vitakaposhikamadaraka visitumie ikulu ya magogoni?
Ni wapi CCM inaiamuru serikali iwanyonge wapinzani?
Ni wapi CCM ikitukanwa imekwisha kwenda mahakamani?
Ni wapi chama cha upinzani duniani kilishawahi kushindauchaguzi kwa sera za ukanda?
 
We mtoa mada, kama wewe unaipenda CCM usishangae pia watu kuichukia CCM. Pia kitu ambacho kilikuwa wazi na kimesemwa mara nyingi sana kwamba ushindi wa CCM ni wamashaka, watu hawakutaka kuelewa, lakini sasa ni dhahiri ukimsikiliza lipumba jinsi alivyo kibeba chama kisicho bebeka pamoja na msaada wa tume ya kura.
Pia kama mwenyekiti alitumia pesa ya EPA kushinda uchaguzi sasa unataka tukiseme chama gani au mtu gani?
na kila kitu kinafika wakati watu wana kichoka, out of fashion, hili swala hauwezi kulazimisha inabidi kuwa mpole.
Tunashukuru kwa yote CCM iliyo tufanyia na sasa hatuna budi kusema inatosha na tunataka madiliko.
cha maana wakubali kutoka kwa amani ili tuendelee kuwaheshimu...
 
Nawachukia kwa sababu hii hapa.

Kula hujala na Kamshahara kenyewe unakolipwa ka pesa ya madafu halafu unaleta mbwembwe za kudandia gari eti unawawahi chadema...utaja kufa bure jinga wewe!!!

Kwa hiyo vyama vya upinzani havitakuwa na FFU na vitaruhusu mambo ya kipuuzipuuzi tu yaendelee!!!!!!!!
 
Hii ni sawa na kutushangaa kwa nini hatumpendi mkeo au mumeo!!!!!!!vyovyote alivyo hata kama ana sura mbaya kiasi gani kwako utamuona ni Mr or Miss world'
 
Ukichunguza, pia hao unaowaona wako CCM hawakipendi, sema wameona ni kijiwe cha kupigia dili, na kuwa na uhakika wakuto shitakiwa hata kama watafanya upuuzi
 
Hizi ndio sababu za kuipenda CCM.......labda



UDSM-violence.jpg
 
lipumba hawezi kuibeba ccm anakitu gani cha ajabu .
 
Ata ningekuwa mimi kama mfumo uliopo nafaidikia nao lazima niipende CCM
Ila kama mfumo uliopo kwangu ni kama Nuksi ie mambo hayaendi maisha yanazidi kuwa magumu siku hadi siku CCM apo inakuwa haiitajiki!Hasa matabaka ya wenye nazo zidi ya wasiokuwa nazo kuzidi kuongezeka.
 
sababu za kuichukia CCM ni nyingi kuliko sababu za kuipenda kwa mtanzania wa kawaida kitu ambacho ni tofauti kwa makada hao stori ni tofauti.

ccm inasema kama unafedha jenga kiwanda. sisi wananchi tunasema ili kujenga viwanda serikali iwawezeshe wananchi kuwapatia mitaji mmana hakuna anayejenga kiwanda kwa fedha zake mfukoni bali wanakopa na kujenga.

ukienda nchi zilizopiga hatua kiuchumumi wanadhibiti uchumi wao kwa kuweka masharti magumu ya kuingiza bidhaa na kuboresha mazingira ya kutoa nje bidhaa ili kuzuia bidhaa za nje kuingia kwa wingi na kuzorotesha uchumi na kuchochea bidhaa kwenda nje ili kuimarisha uchumi. tanzania hakuna mfumo, pato la taifa likiongezeka bidhaa za anasa kama magari, vifaa vya elekronic vinaongezeka na kutudidimiza kiuchumi.

mzalendo akishindana na mgeni katika kandarasi wanapewa wageni kitu ambacho kinadidimiza uchumi maana ukimpa kandarasi mzalendo unapata huduma kama ni barabara na fedha inaendelea kuwa yako kwani inarudi katika mzunguko wako wa fedha wa ndani na utaipata tu kama serikali kupitia makusanyo mbalimbali. lakini ukimpa mgeni akijenga barabara fedha anahamisha anapeleka kwao unabaki na barabara tu fedha umepoteza. hivyo kwa serikali makini inahakikisha inazuia fedha zisitoke katika mzunguko kirahisi.

ccm wameshindwa kabisa kudhibiti uchumi na matokeo yake ni kuongezeka kwa umasikini, ukosefu wa ajira, huduma za jamii kulegalega hasa hii ndio sababu kuu ya kuichukia CCM
 
Nilidhani wasiojua kusoma na kuandika ni wa kizazi cha shule za Mulugo tu kumbe I was wrong, kama hata watu wazima mnaandika hivi
 
usiweke akili zako rehani!hv the freedom of mind kabla hujatoa thead yataka ngumu hii!nyambaffffffff..........!
 
wewe uaipenda ccm na kuchukia vyama vya upinzani. si umwambie mwnykt wako avifutilie mbali? mbona mnatoa ruzuku kwa vyama mnavyovichukia? kama wote 2taipenda ccm nan atipenda cdm cuf au nccr? post ndeeefu isiyo na mantiki! mashabiki wa ccm masaburi!!
 
Usiogope... tunakukumbusha tu...

TAREHE 05-01-2011
Police wawapiga risasi watu zaidi ya 11 ktk maandamano ya CHADEMA. Waua watu 3.

TAREHE_10-2011
Dk.Mwakyembe aenda India kutibiwa kutokana na Kupewa Sumu.PoliCCM walipotezea kisiasa.

TAREHE_02-2012
Shehe Ali khamis Kuuawa kwa mapanga.

TAREHE 26-06-2012
Dr.Ulimboka akatekwa na kufanyiwa unyama.

TAREHE 18-07-2012
Mv spice yazama.

TAREHE 02-09-2012
Daudi Mwangosi auliwa na polisi Iringa.

TAREHE 28-09-2012
LHRC Waishtaki serikali ya K.. ICC

TAREHE 12-10-2012
Mtoto kudhihaki Kitabu kitakatifu (haijawahi kutokea Tz)

TAREHE 16-10-2012
Shehe Farid A. Hadi kiongozi wa Uhamsho kutekwa na kupotea(Alipatikana)

TAREHE _12-2012
Padre Ambrose apigwa risasi Zanzibar

TAREHE _02-2013
Padre Evarist Mushi apigwa risasi Zanzibar.

TAREHE 18-02-2013
Matokeo kidato cha 4 mabovu,haijawahi kutokea duniani tangu kuumbwa kwa Adam na Hawa.
Waliopata div 4 na 0 ni takriban 95%

TAREHE 05-03-2013
Kibanda afanyiwa ya Ulimboka.

TAREHE _03-2013
Lwakatale (mkurugenzi wa usalama CHADEMA) atuhumiwa kwa Ugaidi.

TAREHE 17-04-2013
wabunge 6 wa CHADEMA watolewa nje ya bunge,Ndugai/naibu spika awapa adhabu ya kutoingia bungeni siku 5 kinyume na kanuni za bunge.

Siku hiyohiyo mh.Lema amtaja Rais kuwa ndie mwanzilishi wa udini.

TAREHE 25-04-2013
Lema avamiwa usiku wa manane na polisi kwa amri ya Mulongo/mkuu wa mkoa wa Arusha

UPDATE,

TAREHE 05-05-2013
Mlipuko watokea kanisani Arusha...
Mheshimiwa rais akiwa angani na ndege kuelekea Kuwait kuta..


TAREHE 08-05-2013
Lwakatale/mkulugenzi wa usalama wa CHADEMA afutiwa mashtaka ya ugaidi.

MWAKA 2013
.Deni la taifa lafikia tril.22 wakati Kikwete alikuta deni ni tril.5

.Dola moja=1,600 tshs wakat alikuta dola moja=600tshs.

TAREHE 14-05-2013
tetesi za
Kikwete kuandaliwa mpango wa kuwa rais wa Tz hadi mwaka 2017 badala ya mwaka 2015,ili asimamie kukamilika kwa uundwaji wa katiba mpya.
 
sababu za kuichukia CCM ni nyingi kuliko sababu za kuipenda kwa mtanzania wa kawaida kitu ambacho ni tofauti kwa makada hao stori ni tofauti.

ccm inasema kama unafedha jenga kiwanda. sisi wananchi tunasema ili kujenga viwanda serikali iwawezeshe wananchi kuwapatia mitaji mmana hakuna anayejenga kiwanda kwa fedha zake mfukoni bali wanakopa na kujenga.

ukienda nchi zilizopiga hatua kiuchumumi wanadhibiti uchumi wao kwa kuweka masharti magumu ya kuingiza bidhaa na kuboresha mazingira ya kutoa nje bidhaa ili kuzuia bidhaa za nje kuingia kwa wingi na kuzorotesha uchumi na kuchochea bidhaa kwenda nje ili kuimarisha uchumi. tanzania hakuna mfumo, pato la taifa likiongezeka bidhaa za anasa kama magari, vifaa vya elekronic vinaongezeka na kutudidimiza kiuchumi.

mzalendo akishindana na mgeni katika kandarasi wanapewa wageni kitu ambacho kinadidimiza uchumi maana ukimpa kandarasi mzalendo unapata huduma kama ni barabara na fedha inaendelea kuwa yako kwani inarudi katika mzunguko wako wa fedha wa ndani na utaipata tu kama serikali kupitia makusanyo mbalimbali. lakini ukimpa mgeni akijenga barabara fedha anahamisha anapeleka kwao unabaki na barabara tu fedha umepoteza. hivyo kwa serikali makini inahakikisha inazuia fedha zisitoke katika mzunguko kirahisi.

ccm wameshindwa kabisa kudhibiti uchumi na matokeo yake ni kuongezeka kwa umasikini, ukosefu wa ajira, huduma za jamii kulegalega hasa hii ndio sababu kuu ya kuichukia CCM

Mtasubiri sana chama kitakachokuja kuwagawia fedha za kufanyia biashara........................................Tatizo ukabila na umimi!!!!! Tunashindwa kuungana kisha tukahodhi ardhi yetu tukaiombea kibali na hati miliki mwisho wa siku itunike kama collateral. Lakini tunataka mtu atoke mbande yeye peke yake aanzishe kiwanda cha kupasua magogo.....wapi na wapi bwana. Hatutaki kufanya biashara ya ubia kwa kuogopa kuibiana (na si kuibiwa na CCM).
 
Wazee wa mtwara wamshukuru dangote kwa kukubali kuwekeza
 
Ni kweli tuko wengi (mimi ni mmojawao) tusioipenda ccm. Naomba nikupe sababu zangu kama ambavyo wewe umekuwa na uhuru wa kueleza kwa nini unawashangaa watu wasioipenda ccm!

Kwanza, mimi sikuzaliwa miaka ya 90 na kwenda mbele. Kadi yangu ya ccm niliipata siku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipoanzishwa pale Zanzibar 5.2.1977. Naomba unielewe ninapozungumzia CCM (ya Mwalimu) ninaitofautisha na ccm (ya magamba).

Kumbuka ya kuwa kabla ya CCM kulikuwa na chama cha TANU kilichoanzishwa 7.7.1954 na Afro Shiraz Party (ASP, sina hakika na tarehe kilipoanzishwa). Hivi ndivyo vyama vilivyoleta uhuru wa nchi hizi mbili za Tanganyika (9.12.1961) na Mapinduzi ya Zanzibar (12.1.1964). Baada ya nchi hizi mbili kuungana 26.4.1964 na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado tulibaki na vyama vyetu vikuu viwili, pamoja na vyama vingine kadhaa vya siasa ambavyo havikuwa madarakani. Mwaka 1965, serikali ikavifunga vyama vingine vyote vya siasa na kuanzisha katiba ya chama kimoja, kwa lugha ya kiingereza tunasema (One Party Constitution). Lakini kwa ukweli, nchi yetu haikuwa ya chama kimoja, kwa kuwa tulikuwa bado tuna TANU na ASP. Mwalimu na viongozi waliokuwa madarakani wakati huo waliliona hilo, na kuelewa ya kwamba litakuja kuleta migogoro siku zijazo, ndipo walipoamua kuviunganisha vyama hivi viwili na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kabla ya CCM kuanzishwa, chama cha TANU 5.2.1967 kilipitisha Azimio la Arusha, lililokuwa limeweka misingi kuhusu mwelekeo wa nchi yetu na kutoa dira ya maendeleo ya nchi yetu. Makosa ya Azimio la Arusha yalikuwepo, lakini kuna mazuri mengi sana ambayo yamefanyiwa tafiti mbalimbali na kuonyesha ya kuwa Tanzania ilikuwa mfano mzuri wa kuigwa na nchi zingine za Afrika hata nje ya bara letu. Kubwa katika hayo ilikuwa ni kujaribu kuleta usawa wa wananchi wake. Cheo cha Mheshimiwa kiliondolewa, kila mtu aliitwa Ndugu. Ilikuwa ndugu mbunge, ndugu waziri, ndugu dereva wa basi n.k. Mishahara ya kima cha chini iliongezwa na kodi ya mapato (income tax) kufutwa kwa wafanyakazi wa kima cha chini, lakini wafanyakazi wa ngazi za kati na za juu waliongezewa kodi. Hii ilifanya kuwa na hali inayoelekea kuweka usawa, hakukuwa na matajiri sana wala masikini sana. Miiko ya viongozi iliwekwa, ikiwemo; Kiongozi haruhusiwi kuwa na mishahara miwili, kiongozi haruhusiwi kuwa na hisa katika makampuni, kiongozi haruhusiwi kuwa na nyumba ya kupangisha n.k. Na katiba ilitamka wazi ya kuwa Kiongozi ni Mume na Mke, ama Mke na Mume. Kwa mantiki hii ilikuwa haiwezekani kiongozi akafungua duka kwa jina la mkewe, ama kama ni mke basi asingeweza kufungua biashara yoyote kwa jina la mumewe.

Njia zote kuu za uchumi zilitaifishwa, kulikuwa hakuna benki binafsi, hakuna shirika la bima binafsi, hakuna shirika la nyumba binafsi, na viwanda na makampuni yote makuu yalitaifishwa na serikali, yakawa mashirika ya umma. Shule zote na hospitali zilitaifishwa. Wakati huo tulikuwa watoto wote wa kitanzania tunasoma kwenye shule za serikali. Kwenye darasa moja kuna watoto wa wakulima, watoto wa wakuu wa mikoa, watoto wa mawaziri. Elimu ilikuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka Chuo Kikuu. Gharama ya mzazi ilikuwa sare za shule, tulipatiwa vitabu vya kiada, madaftari, kalamu, rula, 'mathematical sets' na mahitaji mengine yote bure kwa kuwa serikali ilikusanya kodi, na kuitumia kutoa huduma muhimu kama elimu bila malipo. Ile imani unayoizungumzia ya kuwa 'Binadamu wote ni sawa ilitekelezwa kwa vitendo', sio majukwaani. Hospitali zilikuwepo kila wilaya, na zahanati na vituo vya afya vilijengwa navyo vilitoa huduma bure. Huduma za kliniki za kina mama na watoto, upasuaji, vipimo vya X-ray, mpaka dawa zilikuwa zinapatikana kwenye hospitali za serikali bure. Enzi hizo hata biashara ya maduka ya dawa ilikuwa haina maana kwa kuwa mgonjwa anapofika hospitali anapewa dawa zote alizoandikiwa bila malipo. Hiyo ndiyo Tanzania yangu niliyokuwa ninajivunia, hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) ninachokikumbuka mimi. Kiongozi alikuwa anaapa ya kuwa 'Cheo ni dhamana...', cheo hakikuwa usultani wa kurithishwa kutoka baba, kwenda kwa mama na watoto, cheo hakikuwa kinatumika kutuma majeshi kuumiza raia, kubambikia watu kesi zisizokuwa na msingi. Wakati huo mtu akiteuliwa kushika wadhifa haisemwi ya kuwa 'fulani kaula', kwa kuwa haikumaanisha ya kuwa yeye ni mjanja sana kuliko wengine, ila alikuwa anapewa madaraka ili afanye kazi kwa niaba ya wananchi. Kiongozi alikuwa mtumishi wa wananchi, akiwanyenyekea na kusikiliza shida zao na sio kuwatisha kwa kuwaletea virungu pale wasipokubaliane naye. Wewe na mimi hatuwezi kukubaliana kila kitu, ndivyo tulivyoumbwa kama binadamu kila mmoja ana mawazo yake. La kufanya ni kusikiliza kila mtu apewe nafasi aseme aliulo nalo tushauriane, tufike mahali pa kukubaliana ili tupate kutatua matatizo yetu kama taifa. Hiyo ndiyo CCM iliyopendwa.

ccm ya leo imegeuka saratani!
ccm ni mali ya waheshimiwa, hakuna tena ndugu!
ccm kimegeuka chama cha matajiri, angalia mishahara ya viongozi, tazama mahekalu yanayoshamiri kila kukicha, wakati huo huo walala hoi wanadidimia kwenye dimbwi la umaskini!
ccm ni chama cha familia fulani, akitoka baba anakuja mwana, mke, shemeji na swahiba!
ccm imefanya walio madarakani wamesahau ya kuwa cheo ni dhamana, wanatukana hadharani bila hata kuchuja wanayoyasema (Lusinde, Serukamba na wengine) na viongozi ambao wangepaswa kukemea haya wanawalinda!
ccm imegeuka kitovu cha biashara halali na haramu, kinyume na yale yaliyokuwa maadili ya TANU na CCM kwamba kiongozi asiwe mfanyabiashara!
ccm imehakikisha ya kwamba elimu na afya hazipatikani bure ama kwa gharama nafuu kwa kila mtu. Matokeo yake ni wachache wenye pesa wanaoweza kuwasomesha watoto wao ili waendelee kuwa kwenye nyadhifa za juu na watanzania wengine wabaki nyuma. Sasa tuna 'watawala' na 'watawaliwa'. Huduma za afya sasa ni kupelekwa India, watanzania wangapi wenye uwezo huo?

Inaelekea wewe bado ni kijana mdogo sana huyajui uyasemayo. Mimi nimeguswa sana na hayo yote. Amini usiamini, bado ninayo kadi yangu ya CCM ya mwaka 1977. Nimeiweka kama kumbukumbu kwa yeyote atakayekuja kudai ya kuwa siipendi nchi yangu.

Mimi ni mwanachama hai wa CDM, sioni aibu kutamka hivyo, na sitanyamaza hadi pale ccm ya jk na mashetani wenzake watakapong'oka madarakani!

Peoples' Power!!!
 
Back
Top Bottom