Nawashangaa wanaoichukia CCM!! Hebu soma hapa.

Nawashangaa wanaoichukia CCM!! Hebu soma hapa.

Usiogope... tunakukumbusha tu...

Kikwete ni nani? Ni CCM ama ni mtu mwenye cheo cha rais? Na rais maana yake ni CCM? Na polisi= CCM? Vyama vingine havitakuwa na jeshi? Upuuuuuuuziii mtupu. Nimetoa mada nikitegemea majibu ya kisayansi lakini kumbe majibu niyapatayo ni ya kisharobalo na ki-face book......
 
Mtasubiri sana chama kitakachokuja kuwagawia fedha za kufanyia biashara........................................Tatizo ukabila na umimi!!!!! Tunashindwa kuungana kisha tukahodhi ardhi yetu tukaiombea kibali na hati miliki mwisho wa siku itunike kama collateral. Lakini tunataka mtu atoke mbande yeye peke yake aanzishe kiwanda cha kupasua magogo.....wapi na wapi bwana. Hatutaki kufanya biashara ya ubia kwa kuogopa kuibiana (na si kuibiwa na CCM).

swala la kushirikiana ni kisingizio kwani hofu iliyopo juu ya ushirika ina mantiki juzijuzi hapa watu walichangishana fedha wakiita nicol mwisho wake nini?

badala ya kusimama kwenye majukwaa na kusema watu washirikiane serikali inaweza kuanzisha makampuni na kuwauzia watu hisa. je huu si ushirika na kazi ya serikali ni nini kama sio kutoa njia. leo unaambiwa unda ushirika utaungana na nani aliyetayari ingawa watu wanataka faida lakini riski ni nyingi.
 
Mtoa mada anasema kuwa nchi inang'aa kwa sababu ya tochi sola na taa za mchina ! Kwani ccm ndo wamegawa hizo nishati kwa wananchi bure au watu kwa juhudi zao japo wananyonywa kwa kodi kubwa wamejinunulia - wapenda ccm mhh!
 
Imekuwa ni kawaida sana kwa kizazi cha sasa kilichozaliwakati yqa mwaka 1990 na kuja huku mbele miaka ya 2000. Imekuwa ni kawaida sanakusikia mabezo mengi tu kwamba CCM ni chama kisichofaa kuongoza.

Kikwete ni nani? Ni CCM ama ni mtu mwenye cheo cha rais? Na rais maana yake ni CCM? Na polisi= CCM? Vyama vingine havitakuwa na jeshi? Upuuuuuuuziii mtupu. Nimetoa mada nikitegemea majibu ya kisayansi

Yani unajikanyaga toka mwanzo, hata kutumia kompyuta tu hujui, halafu unataka majibu ya kisayansi! Hivi sayansi unaijua wewe?!

Umeanza mwenyewe kwa kusema watu wanaibeza CCM kuwa ni chama kisichofaa kuongoza na umehitimisha kuwa CCM ndio chama kinachotakiwa kuongoza. Ukitajiwa maovu ya viongozi wa CCM unatoa mapovu, ooh.. kwani wao ni CCM au ni watu binafsi!!! Hivi unajielewa au umelewa viroba?!
Kwani kuna mahali watu waliipigia CCM kura, au wataipigia kura kuwaongoza au waliwapigia akina Kikwete unaowakana leo?!!

Mkuu watu wanavyokuambia hazimo timamu hawakudanganyi, jiangalie upya, kama vipi wahi hospitali...
 
sijui lini tutakua na mawazo huru bila kujipendekeza upande wowote. Tuna macho lkn hatuoni
 
Naona ulikuwa unajifunza kuandika kutumia computer. Asante kwa mazoezi. Jaribu tena kuandika vizuri zaidi. Sasa badirisha namna ya mwandiko tuone.
 
Nimetoka kwenye ban hapa naweza kurudishwa tena ngoja nisepe.
 
tuikosoe ccm pale inapokosea au kuteleza na pale inastahili kusifiwa tuipe haki yake ili iende ipasavyo mana ni chama cha wanyonge
 
hv waungwan hii ya Lumumba kutoa buku 7 kwa kupost information in ukweli kiaasi gani?
 
Yapo mengi ya kutaka ccm sasa itoke ili awepo mwingine wa kuuleta mfumo mpya:
1. Ccm haijui kuwa gamba ni kulitupia mbali azimio la arusha na kulikumbatia azimio la zanzibar.
2. Katika kufanya hivyo chama kina wenyewe (akina rostamu aziz, manji, jeet patel, wale wa somaia group, mwigulu, kinana, nape, n.k)
3.kimesahau kuna wazee walitumikia vizuri nchi hii lakini hakuna kanuni wala sheria ya wao kupata pensheni. Rejea sheria ya pensheni ya viongozi wanaopata pesa sawa na bajeti ya wizara mojawapo kwa mwaka huku kuwa watumishi wengine walikuwa kama........
4. Angalia uongozi wa nchi hii umekewa na utaratibu wa watoto wa viongozi hao ndio waendelee kuongoza nchi hii pia ndio wamiliki wa ajira nzuri na fursa zote za nchi hii.
Kutokuwepo na mkakati wa wakulima wadogowadogo kuweza kujiondoa katika umaskini.
5.angalia jiji la dar ambako ndiko tanzania: Watu wanapandana wakigombania usafiri baada ya miaka 52 ya uhuru. Uchafu umekithiri, ukiondoa barabara chache tu maeneo mengi ni madimbwi ya maji na matope kedekede mvua inaponyesha, hata vibanda vilivyokuwa vya jumuia kuchotea maji havipo tena, maji mengi ni ya chumvi sio safi na salama na umeme bado unakatikakatika tu.
5. Rejea bodi ya mikopo, rejea wizi na udanganyifu wa mitihani (huenda wengi wa wasomi wa hivi karibuni ni wezi wa mitihani au wadanganyifu wa mitihani- mwigulu, nape, n.k)
6.rejea shule za kata na kushindwa kwa wanafunzi wa level zote.
7. Mkulima hawezi kumudu gharama za matibabu.
8. Gharama ya cementi kagera ni maratatu ya bei ya dar, huku bei ya bia ni sawa bin sawa.
9. Yapo lukuki na lukuki.
Hivyo ccm kitoke ili chama kingine kije na utaratibu mbadala maana haya niliyoyataja yamekuwa kivumiliwa bila ccm kujirekebisha na badala yake wanakwapua kama wasio na uhakika wakuendelea kuwepo.
 
Kwa inayoyafanya CCM na mtu ukayasifia,ni sawa na kuyafunua makalio yako, kujipanua ili nyuki waingie na kujisifu kuwa u-mbunifu wa mzinga wako mwenyewe!
 
Kwa hiyo vyama vya upinzani havitakuwa na FFU na vitaruhusu mambo ya kipuuzipuuzi tu yaendelee!!!!!!!!

Wataboreshewa Mazingira ya Kazi na Maslahi.
Watajikuta wanatumia Busara Zaid Kutatua Matatizo bADALA YA mIGUVU mIINGI ISIYO na Maana
 
cna uhakika kama baba mwanaasha kama alishinda 2010. kwa mana hyo cwezi kuchangia hadi nipate uhakika.
 
sababu za kuichukia CCM ni nyingi kuliko sababu za kuipenda kwa mtanzania wa kawaida kitu ambacho ni tofauti kwa makada hao stori ni tofauti.

ccm inasema kama unafedha jenga kiwanda. sisi wananchi tunasema ili kujenga viwanda serikali iwawezeshe wananchi kuwapatia mitaji mmana hakuna anayejenga kiwanda kwa fedha zake mfukoni bali wanakopa na kujenga.

ukienda nchi zilizopiga hatua kiuchumumi wanadhibiti uchumi wao kwa kuweka masharti magumu ya kuingiza bidhaa na kuboresha mazingira ya kutoa nje bidhaa ili kuzuia bidhaa za nje kuingia kwa wingi na kuzorotesha uchumi na kuchochea bidhaa kwenda nje ili kuimarisha uchumi. tanzania hakuna mfumo, pato la taifa likiongezeka bidhaa za anasa kama magari, vifaa vya elekronic vinaongezeka na kutudidimiza kiuchumi.

mzalendo akishindana na mgeni katika kandarasi wanapewa wageni kitu ambacho kinadidimiza uchumi maana ukimpa kandarasi mzalendo unapata huduma kama ni barabara na fedha inaendelea kuwa yako kwani inarudi katika mzunguko wako wa fedha wa ndani na utaipata tu kama serikali kupitia makusanyo mbalimbali. lakini ukimpa mgeni akijenga barabara fedha anahamisha anapeleka kwao unabaki na barabara tu fedha umepoteza. hivyo kwa serikali makini inahakikisha inazuia fedha zisitoke katika mzunguko kirahisi.

ccm wameshindwa kabisa kudhibiti uchumi na matokeo yake ni kuongezeka kwa umasikini, ukosefu wa ajira, huduma za jamii kulegalega hasa hii ndio sababu kuu ya kuichukia CCM
Daaah!! Akili nyingi sanaaa,,,Umenifariji ndugu yangu


Sent from my BlackBerry Z10 using JamiiForums
 
Ni kweli tuko wengi (mimi ni mmojawao) tusioipenda ccm. Naomba nikupe sababu zangu kama ambavyo wewe umekuwa na uhuru wa kueleza kwa nini unawashangaa watu wasioipenda ccm!

Kwanza, mimi sikuzaliwa miaka ya 90 na kwenda mbele. Kadi yangu ya ccm niliipata siku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipoanzishwa pale Zanzibar 5.2.1977. Naomba unielewe ninapozungumzia CCM (ya Mwalimu) ninaitofautisha na ccm (ya magamba).

Kumbuka ya kuwa kabla ya CCM kulikuwa na chama cha TANU kilichoanzishwa 7.7.1954 na Afro Shiraz Party (ASP, sina hakika na tarehe kilipoanzishwa). Hivi ndivyo vyama vilivyoleta uhuru wa nchi hizi mbili za Tanganyika (9.12.1961) na Mapinduzi ya Zanzibar (12.1.1964). Baada ya nchi hizi mbili kuungana 26.4.1964 na kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado tulibaki na vyama vyetu vikuu viwili, pamoja na vyama vingine kadhaa vya siasa ambavyo havikuwa madarakani. Mwaka 1965, serikali ikavifunga vyama vingine vyote vya siasa na kuanzisha katiba ya chama kimoja, kwa lugha ya kiingereza tunasema (One Party Constitution). Lakini kwa ukweli, nchi yetu haikuwa ya chama kimoja, kwa kuwa tulikuwa bado tuna TANU na ASP. Mwalimu na viongozi waliokuwa madarakani wakati huo waliliona hilo, na kuelewa ya kwamba litakuja kuleta migogoro siku zijazo, ndipo walipoamua kuviunganisha vyama hivi viwili na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kabla ya CCM kuanzishwa, chama cha TANU 5.2.1967 kilipitisha Azimio la Arusha, lililokuwa limeweka misingi kuhusu mwelekeo wa nchi yetu na kutoa dira ya maendeleo ya nchi yetu. Makosa ya Azimio la Arusha yalikuwepo, lakini kuna mazuri mengi sana ambayo yamefanyiwa tafiti mbalimbali na kuonyesha ya kuwa Tanzania ilikuwa mfano mzuri wa kuigwa na nchi zingine za Afrika hata nje ya bara letu. Kubwa katika hayo ilikuwa ni kujaribu kuleta usawa wa wananchi wake. Cheo cha Mheshimiwa kiliondolewa, kila mtu aliitwa Ndugu. Ilikuwa ndugu mbunge, ndugu waziri, ndugu dereva wa basi n.k. Mishahara ya kima cha chini iliongezwa na kodi ya mapato (income tax) kufutwa kwa wafanyakazi wa kima cha chini, lakini wafanyakazi wa ngazi za kati na za juu waliongezewa kodi. Hii ilifanya kuwa na hali inayoelekea kuweka usawa, hakukuwa na matajiri sana wala masikini sana. Miiko ya viongozi iliwekwa, ikiwemo; Kiongozi haruhusiwi kuwa na mishahara miwili, kiongozi haruhusiwi kuwa na hisa katika makampuni, kiongozi haruhusiwi kuwa na nyumba ya kupangisha n.k. Na katiba ilitamka wazi ya kuwa Kiongozi ni Mume na Mke, ama Mke na Mume. Kwa mantiki hii ilikuwa haiwezekani kiongozi akafungua duka kwa jina la mkewe, ama kama ni mke basi asingeweza kufungua biashara yoyote kwa jina la mumewe.

Njia zote kuu za uchumi zilitaifishwa, kulikuwa hakuna benki binafsi, hakuna shirika la bima binafsi, hakuna shirika la nyumba binafsi, na viwanda na makampuni yote makuu yalitaifishwa na serikali, yakawa mashirika ya umma. Shule zote na hospitali zilitaifishwa. Wakati huo tulikuwa watoto wote wa kitanzania tunasoma kwenye shule za serikali. Kwenye darasa moja kuna watoto wa wakulima, watoto wa wakuu wa mikoa, watoto wa mawaziri. Elimu ilikuwa bure kuanzia darasa la kwanza mpaka Chuo Kikuu. Gharama ya mzazi ilikuwa sare za shule, tulipatiwa vitabu vya kiada, madaftari, kalamu, rula, 'mathematical sets' na mahitaji mengine yote bure kwa kuwa serikali ilikusanya kodi, na kuitumia kutoa huduma muhimu kama elimu bila malipo. Ile imani unayoizungumzia ya kuwa 'Binadamu wote ni sawa ilitekelezwa kwa vitendo', sio majukwaani. Hospitali zilikuwepo kila wilaya, na zahanati na vituo vya afya vilijengwa navyo vilitoa huduma bure. Huduma za kliniki za kina mama na watoto, upasuaji, vipimo vya X-ray, mpaka dawa zilikuwa zinapatikana kwenye hospitali za serikali bure. Enzi hizo hata biashara ya maduka ya dawa ilikuwa haina maana kwa kuwa mgonjwa anapofika hospitali anapewa dawa zote alizoandikiwa bila malipo. Hiyo ndiyo Tanzania yangu niliyokuwa ninajivunia, hicho ndicho Chama Cha Mapinduzi (CCM) ninachokikumbuka mimi. Kiongozi alikuwa anaapa ya kuwa 'Cheo ni dhamana...', cheo hakikuwa usultani wa kurithishwa kutoka baba, kwenda kwa mama na watoto, cheo hakikuwa kinatumika kutuma majeshi kuumiza raia, kubambikia watu kesi zisizokuwa na msingi. Wakati huo mtu akiteuliwa kushika wadhifa haisemwi ya kuwa 'fulani kaula', kwa kuwa haikumaanisha ya kuwa yeye ni mjanja sana kuliko wengine, ila alikuwa anapewa madaraka ili afanye kazi kwa niaba ya wananchi. Kiongozi alikuwa mtumishi wa wananchi, akiwanyenyekea na kusikiliza shida zao na sio kuwatisha kwa kuwaletea virungu pale wasipokubaliane naye. Wewe na mimi hatuwezi kukubaliana kila kitu, ndivyo tulivyoumbwa kama binadamu kila mmoja ana mawazo yake. La kufanya ni kusikiliza kila mtu apewe nafasi aseme aliulo nalo tushauriane, tufike mahali pa kukubaliana ili tupate kutatua matatizo yetu kama taifa. Hiyo ndiyo CCM iliyopendwa.

ccm ya leo imegeuka saratani!
ccm ni mali ya waheshimiwa, hakuna tena ndugu!
ccm kimegeuka chama cha matajiri, angalia mishahara ya viongozi, tazama mahekalu yanayoshamiri kila kukicha, wakati huo huo walala hoi wanadidimia kwenye dimbwi la umaskini!
ccm ni chama cha familia fulani, akitoka baba anakuja mwana, mke, shemeji na swahiba!
ccm imefanya walio madarakani wamesahau ya kuwa cheo ni dhamana, wanatukana hadharani bila hata kuchuja wanayoyasema (Lusinde, Serukamba na wengine) na viongozi ambao wangepaswa kukemea haya wanawalinda!
ccm imegeuka kitovu cha biashara halali na haramu, kinyume na yale yaliyokuwa maadili ya TANU na CCM kwamba kiongozi asiwe mfanyabiashara!
ccm imehakikisha ya kwamba elimu na afya hazipatikani bure ama kwa gharama nafuu kwa kila mtu. Matokeo yake ni wachache wenye pesa wanaoweza kuwasomesha watoto wao ili waendelee kuwa kwenye nyadhifa za juu na watanzania wengine wabaki nyuma. Sasa tuna 'watawala' na 'watawaliwa'. Huduma za afya sasa ni kupelekwa India, watanzania wangapi wenye uwezo huo?

Inaelekea wewe bado ni kijana mdogo sana huyajui uyasemayo. Mimi nimeguswa sana na hayo yote. Amini usiamini, bado ninayo kadi yangu ya CCM ya mwaka 1977. Nimeiweka kama kumbukumbu kwa yeyote atakayekuja kudai ya kuwa siipendi nchi yangu.

Mimi ni mwanachama hai wa CDM, sioni aibu kutamka hivyo, na sitanyamaza hadi pale ccm ya jk na mashetani wenzake watakapong'oka madarakani!

Peoples' Power!!!
I agree with u 100%....Nimefarijika Baba Yangu...Mwenyezi Mungu akujaalie afya njema na uzima..#People 's Power(M4C)


Sent from my BlackBerry Z10 using JamiiForums
 
Nawachukia kwa sababu hii hapa.

Kula hujala na Kamshahara kenyewe unakolipwa ka pesa ya madafu halafu unaleta mbwembwe za kudandia gari eti unawawahi chadema...utaja kufa bure jinga wewe!!!
jinga kweli hl poli ccm linay kurusha kitu kizito
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Natabiri kwamba mwandishi wa Riwaya hii aliandika akiwa na njaa ( yaani kabla hajala ).
 
Back
Top Bottom