Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,956
NAWAPA HILI DARASA, MUYAEPUKE MARADHI
Ukiipata PID, unaweza ukalia
Au pata fibroid, theatre utaingia
Ukiugua STD, waharibu genitalia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Mle mboga za majani, kuikwepa anemia
Zipunguze burudani, ukwepe insomnia
Ukifika uzeeni, usipate dementia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kansa ya thyroid, Sauti itakauka
Hata ya Raynoid, Vidole vitanyauka
Kikoroma very loud,mke atakuchoka
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Vitamini na matunda, huimarisha akili
Afya yako kulinda, mwili wako unawili
Uviepuke vidonda, vya tumbo hata vya mwili
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kaswende usiipate, usizae mazezeta
Kansa ya prostate, mkojo utafukuta
Au pata stroke, shida nyingi utapata
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Bora upate mimba, ongeza populesheni
Omba usizipate mba, za kichwani au ukeni
Waweza kosa mchumba, ukiwa na depresheni
Nawapa hili darasa, muyaepuke maradhi
Muuepuke ulevi, kukwepa maradhi moyo
Weza pata HIV, kama ngono si mchoyo
Utakufa hivihivi, bora uwe kibogoyo
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Unaijua aleji, ya pua au ya ngozi
Kifua wakichalenji, ukipata kikohozi
Huwezi kukwepa chaji, kupata kamili dozi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kansa yaua jama, ya tumbo ama ya ziwa
Gonorrhea ninasema, kupona inachelewa
Ukiipata lymphoma, damu weza ishiwa
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti akiwa mgumba, Au mume infertile,
Pressure itawakumba, kunywa dawa hii, ile
Ndoa yaweza kuyumba, mganga huyu na yule
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti usitoe mimba, ngono zembe epukeni
Salama ya tatu bomba, ibebeni mikobani
Au subiri mchumba, epuka infeksheni
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
BPH inatesa, Ukipata uzeeni
Chiken pox kinasa, enzi zile utotoni
Usiipate pangusa, punguzeni maruhani
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Bora upate mafua, yale ya influenza
TB itakuzuzua, utamwambukiza mwenza
Kichocho utaugua, Ukinywa maji ya Mwanza
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kiepuke Kisukari, Insulini hufilisi
Bacteria si shwari,ogopa meningitisi
Ukishusha suruari, utaibamba AIDsi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Zoezi fanya ugali, ukwepe hipatensheni
Kula papai na wali, kwepa konstipasheni
Bia ziweke mbali, kunywa kidogo waini
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Pata mental ilinesi, utaja kula kinyesi
Watu wote tawadisi, mamamkwe kumkisi
Utapata hepatitisi, kifanya ya Ibilisi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Mwanangu hana asthma, na otitisi media
Figo zangu shwari nzima,sijawahi ugulia
Dada hana papiloma, na hata leukemia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti yangu si zezeta, mzuri ametameta
Sipendi ma-witch dokta, mlo safi aupata
Ukipenda kunifata, afya bora utapata
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Nadhani haya yatosha, kuna mengi sikusema
Siyo kama nawatisha, mimi dokta huruma
Sitaki mkaharisha, nawapa haya kwa wema
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Ukiipata PID, unaweza ukalia
Au pata fibroid, theatre utaingia
Ukiugua STD, waharibu genitalia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Mle mboga za majani, kuikwepa anemia
Zipunguze burudani, ukwepe insomnia
Ukifika uzeeni, usipate dementia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kansa ya thyroid, Sauti itakauka
Hata ya Raynoid, Vidole vitanyauka
Kikoroma very loud,mke atakuchoka
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Vitamini na matunda, huimarisha akili
Afya yako kulinda, mwili wako unawili
Uviepuke vidonda, vya tumbo hata vya mwili
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kaswende usiipate, usizae mazezeta
Kansa ya prostate, mkojo utafukuta
Au pata stroke, shida nyingi utapata
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Bora upate mimba, ongeza populesheni
Omba usizipate mba, za kichwani au ukeni
Waweza kosa mchumba, ukiwa na depresheni
Nawapa hili darasa, muyaepuke maradhi
Muuepuke ulevi, kukwepa maradhi moyo
Weza pata HIV, kama ngono si mchoyo
Utakufa hivihivi, bora uwe kibogoyo
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Unaijua aleji, ya pua au ya ngozi
Kifua wakichalenji, ukipata kikohozi
Huwezi kukwepa chaji, kupata kamili dozi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kansa yaua jama, ya tumbo ama ya ziwa
Gonorrhea ninasema, kupona inachelewa
Ukiipata lymphoma, damu weza ishiwa
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti akiwa mgumba, Au mume infertile,
Pressure itawakumba, kunywa dawa hii, ile
Ndoa yaweza kuyumba, mganga huyu na yule
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti usitoe mimba, ngono zembe epukeni
Salama ya tatu bomba, ibebeni mikobani
Au subiri mchumba, epuka infeksheni
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
BPH inatesa, Ukipata uzeeni
Chiken pox kinasa, enzi zile utotoni
Usiipate pangusa, punguzeni maruhani
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Bora upate mafua, yale ya influenza
TB itakuzuzua, utamwambukiza mwenza
Kichocho utaugua, Ukinywa maji ya Mwanza
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Kiepuke Kisukari, Insulini hufilisi
Bacteria si shwari,ogopa meningitisi
Ukishusha suruari, utaibamba AIDsi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Zoezi fanya ugali, ukwepe hipatensheni
Kula papai na wali, kwepa konstipasheni
Bia ziweke mbali, kunywa kidogo waini
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Pata mental ilinesi, utaja kula kinyesi
Watu wote tawadisi, mamamkwe kumkisi
Utapata hepatitisi, kifanya ya Ibilisi
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Mwanangu hana asthma, na otitisi media
Figo zangu shwari nzima,sijawahi ugulia
Dada hana papiloma, na hata leukemia
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Binti yangu si zezeta, mzuri ametameta
Sipendi ma-witch dokta, mlo safi aupata
Ukipenda kunifata, afya bora utapata
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi
Nadhani haya yatosha, kuna mengi sikusema
Siyo kama nawatisha, mimi dokta huruma
Sitaki mkaharisha, nawapa haya kwa wema
Nawapa hili darasa, Muyaepuke maradhi