Nawachukia sana Polisi

Nawachukia sana Polisi

Inasikitisha mno kuwa tunaishi kwenye nchi ambayo sensitive issue kama hii inaishia kulalama humu JF, wananchi wa nchi nyingine wanafanikiwa wapi ambapo watanzania wanashindwa?,push backs zitaanza vipi na lini?,Hamza (rip)alionyesha njia baada ya kudhulumiwa ?,tuendelee kula mtori mifupa tutakutana nayo chini.
Rest in peace Hamza.
 
sijui ni kwanini mtu akivaa zile sare anakuwa mkatili kupinduki then hawana huruma hata robo ...yaani majambazi wanaroho nzuri kuliko maaskari....usije ukachukua make wake aisee watakufanya kitu mbaya....sijui ni kwanini ukifanya Ile kazi unageuka unakuwa mnyama.....
 
Hawa jamaa mimi ndo wananichukia sana na kila ninapopita au kukaa wakijua hawaji au nikifika kwenye vijiwe vya bata wanahama hadi siku 1 mwenye bar alinifuata na kuniomba nisiwe naenda pale siku ya j4 hadi ijumaa. Shida ni kwamba mimi nawatambua sana mishe zao sasa wanakuwa na hofu na wala siyo snitch
 
Jifunze kulipa kisasi aliyekufanyia ubaya mpe anachostaili aya mambo ya kumuachia Mungu yatakutesa maisha yako yote kama huwezi kumshtaki basi pigs komboraa alale kitandani afilisike kwa ugonjwa

Sent from my Infinix X571 using JamiiForums mobile app
We ndo unampoteza , kusamehe ndo big deal.
Utalipa kisasi kwa wangapi? Capacity yao unaijua ? kuna watu nao wamejipanga kwa ubaya na ni kazi yao , anaqeza kukuweka busy mwaka mnatafutana tu , yanini?
Mi hata unikanyage mguu kwa makusudi , nitakuomba msamaha mie na kuondoka , Maisha yenyewe mafupi sitaki mtu aniingizie ratiba zake kwenye plan yangu ya lifestlye.
 
Kwa nilipofikia Acha niwachukie tuu hawa viumbe wanaojiita polisi, sio polisi wa kwenye muvi namaanisha hawa polisi wetu wa Tz, yaani nawachukia sana.

Wamesababisha nianze kuishi Maisha ya kimaskini, sina hatia yoyote lakini walinikamata na kuning'ang'ania.

Hawakutaka kuniachia, hawakutaka kunipa dhamana, waliendelea kunishikilia wakinituhumu kwa mambo mazito ambayo sihusiki nayo.

Wameniachia muda ukiwa umeenda sana, wameniachia ni baada ya ndg zangu kuhangaika sana, Wameniachia kwa kunipeleka mahakamani na kunibambika kesi isiyo yangu

Nina maumivu makali sana juu ya uonezi walionifanyia polisi hawa...

Wanaotuchelewesha kwenye kudai katiba mpya walaaniwe wote
 
Mkuu pole sana...
Unajua Polisi ni binadamu na wana udhaifu mkubwa hasa kwenye tamaa ya hela..

Mishahara yao ni midogo.. Angalia hata barabarani sehemu ya wazi lakini askari wanasimamisha gari kuomba hela kwa nguvu..

Ukiwa umepelekwa polisi huna kosa.. Jishushe.. Usijidai unajua sheria.. Maana wao wana namna ya kutengeneza kosa / ushahidi.. Sasa ukiwa mbishi wanapeleka ushahidi huo kwa hakimu na ukifanya masihara unakula mvua ya kutosha..

Kuna ndugu yetu alikuwa anadaiwa hela flani hataki kulipa.. Anayemdai akaenda polisi akawapa hela.. Jamaa akakamatwa.. Humo kituoni akajidai mimi sina kosa nipelekeni mahakamani... Sijui nina mwanasheria...

Jioni yupo kituoni anaona askari wanatoa silaha store kisha akashikishwa kwa nguvu mikononi..

Akaambiwa tunakupa ujambazi kwa kutumia silaha.. Na huwa ni miaka 30.. akaomba kuongea na ndugu.. tukajichanga Kwanza ili atoke.. Kisha tukajichanga kupunguza deni analodaiwa...

Ushauri kwa mazingira yetu yalivyo mabovu ya kubambikiana kesi.. Ni vizuri kuwa mpole.. Kutoa ushirikiano... Na ikibidi wape chochote polisi ili usiumie zaidi
 
Ni watu wabaya na wenye tamaa,hawana cha undugu
Kuna siku nilipata ajari ya barabaran ikinihusisha mimi na boda

Lakin ili tumalize hyo inshu kwenye kituo cha polisi pamoja na kumpigia shemeji yetu wa kike ndo mkuu wa kituo nikajua tutayamaliza fresh lakin bado pesa ilihusika pamoja na kumuita shemeji,hapo ndo niliamin hawa watu sio wa kawaida
 
Ila hawa jamaa huwa wananimaliza pale linapotokea tukio mtaani let say labda la mauaji au la kujeruhi,wakija mtaani wanachukua watu wengi sana wengine hata ambao hawahusian kabisa na hilo tukio mfano wanaweza kubeba hata mpita njia tu

Mkishafika kituoni mnahojiwa kama ulikuwa mpita njia unakuwa unahis kuwa ni inshu ndogo utahojiwa na kuondoka lakin ajabu ni kuwa watakung'ang'ania na watahakikisha kutoka humo lazima utoe hela tena nyingi tu
 
Hawa wangese ambapo huwa wananishangaza zaidi ni pale ambapo wewe ukiwa umeshikiliwa au ukiwa na kesi wanakupeleka puta puta sana lakin ikitokea siku wewe umeenda kumshitaki mtu pale unashangaa jamaa wanakuwa kama wazito hv kufanya jambo lako na unaweza kumleta mtuhumiwa wako pale lakin ukaona tena kama wanakuwa upande wake na kuanza kuwasihi myamalize yaan kisimple simple tu
 
sijui ni kwanini mtu akivaa zile sare anakuwa mkatili kupinduki then hawana huruma hata robo ...yaani majambazi wanaroho nzuri kuliko maaskari....usije ukachukua make wake aisee watakufanya kitu mbaya....sijui ni kwanini ukifanya Ile kazi unageuka unakuwa mnyama.....
Mkuu kwenye ujambazi Kuna wachamungu Safi lkn kwenye upolisi Kuna mashetani Safi....

Kataa Polisi usiwe na urafiki na mipolisisiemu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom