Navunja ndoa ya mtu!!!!

Navunja ndoa ya mtu!!!!

Sikulaumu na pia sikutetei....kuna mambo ambayo tunapaswa kuyawekea tahadhari toka mwanzo hasa tunapokuwa tunawasiliana na wake/waume za watu ..Na wewe inaonyesha uli-mess up from the day go..mfano hata wewe ukijiweka kwenye nafasi ya huyo jamaa ..afu mtu unayemhisi ampigie simu mkeo ..asiongeee..lolz..nahsi utaona ambavyo ni ngumu sana kuaminika kirahisirahisi...

La kwanza jifunze namna bora ya kuishi na mke wa mtu hata kama mnafanya kazi pamoja (distancing)...La pili, kuhusu hili jambo kama una mke mshirikishe kwanza ili ajue kilichokutokea na hata likitokea la kutokea akupe support (manake unaweza kupoteza huku na kule)..Then, usifanye mawasiliano yeyote na huyu dada..hell no...naaamini kama hamkuwa na kitu chochote the truth will set you free..........................

point taken unajua huyo mmewe ni lazima afikili hivyo kutokana na yeye alitoka safari hapo msimlaumu jamaa yee hawezi ona ukweli kwa jinsi situation ilivyo.
 
Yani bado nahasira n wewe halafu unakuja kunitangaza huku eeh?

Mimi unanionea bure sina mahusiano ya kimapenzi na mkeo, ninachokuomba ni unisamehe kwa ile Call iliyopigwa kimakosa na mtoto
 
Huyu jamaa anampenda sana mkewe kiasi kwamba anakuwa na wivu wa kijinga, na tunaomfahamu huyu dada hapa ofisini hana tabia anazomzania labda huko mtaani kwao...mimi kinachoniuma ni huyu dada ikivunjika ndoa yake ilihali hana kwasababu yangu na akiwa hana uhusiano wowote na mimi
Kuna Baadhi Ya Watu Husema Wanaume Sometimes Huwa Chanzo Kwa wake / Partner Wao Kucheat, Simply Because Wamekuwa Wakituhumiwa sana Kuwa Si Waaminifu Kitu Ambacho Si Kweli.
 
Wanaume bana kama vp aende ata ofs za tigo voda akafatilie call zake na zawko.kam kuna ukweli
 
Ila inaniumiza sana, nimejifunza kitu kikubwa sana hya mambo ya wivu

Pole aise. Ushauri wa kukata mawasiliano naye kwa muda alioutoa mjumbe ninauunga mkomo asilimia zote.
Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.
 
ACHA MAMBO ZAKO WEWE!!!!!!!!!! Kazi gani MNAONGEA HADI USIKU!!!!!! Nyamaaaaff!!!!!!!! Wewe ndo mwenye tabia CHAFU ya kutumia kigezo cha kazi kuendeleza mahusiano yasiyo rasmi na mke wa mwenzio!!!!!!!! Ndio mnafanya kazi ila mida ya kaz si Asubuhi hadi Saa 11 kwa nyie wajenzi wa taifa hata saa 2usiku si mbaya!!!!!! Ila wewe usivo na soni saa 4 wampigia mke wa mtu kisa Kazi!!!!!!!!!!!

Aaaaaaaaaah! Give us a break bana!We sema ukweli tu pamoja na kazi kuna kielement cha EVIL INTENTIONS na unajisikia raha kuongea na huyo dada, basi kakitokea kasababu tu ushamuendea hewani!Mimi simu yangu ya kikazi saa 11 kamili NAIZIMAAAA hadi kesho yake! Kazi haziishagi zitaendelea kesho! Dharura zitajiju manake nikiwaendekeza maboss kama nyie utafanya kaz hadi jumapili!!!!!!!!!

Kubali kuwa ulilofanya ni unyanyasaji wa kiofisi! Hadi mtoto kuipiga ile namba manake imekaa juu juu kwa kupigwa sanaaa! Ifike Mahali mabosi muheshimu ndoa za wenzenu! Sio kisa ndo boss kila dakika wapiga piga tuuuu!!!!!!!! Haya Mchukue ufanye nae kazi vizuri basi masaa 24 piga saa hivi!

Huyo mumewe sio mpuuzi wala mjinga kufikia uamuzi huo! HUYU KUNA MIPAKA ALIVUKA SEMA HASEMI TU HUMU!!!!!!!!

Mh mbona umemtuhumu hvo wkt hajesema km yeye ni bos wake ni mfanyakaz mwenzake na huwa anamuachia kaz zake amfanyie akienda kwenye mambo ya kijamii!
Naona km ume2nga thread yako halafu umeassume sana badala ya kujib au kutoa ushauri kwa mujibu wa mtoa mada!
Wakina dada walioolewa maofisin walio weng wanabebwa kwa stail hii kwan wanamajukumu mengi ya kifamilia!
Kaa ukijua si kila mtu anasimu ya ofcn na co kila ofic inatoa cm au inatoa cmu kwa kila mfanyakaz!
Sion hayo unayomsema huyu kaka!
 
We ndo maana nakupendaga, hucheleweshi, yeye mwenyewe ajifikifirie ni kwa kipind gani mzee wa watu kavumilia. Toka airport mwawasiliana tuuu, et kazi za kiofisi, hakumbuki shemeji katoka safari kamiss kitumbua, ye full kupiga. Kama mzee wa watu alikuwa katunisha suruali toka yuko angani na ukame wa kitumbua, kashuka ndan ya ndege kwenye gari full kula denda we waja na visimu vyako vya kiofisi. Hakyanan Sikuelewi. Tena kavumilia, ningekuwa mimi Mbona hata hilo la kutoka airport lingekuwa chungu

Angekataa kumfanyia huyu dada kaz zake angeenda kumpokea mumewe Airport!?
Angeacha kuzfanya kwa sababu kuna vitu havielewi na kuogopa kuwasiliana na huyu mama kesho arud ofisin akute km alivoiacha,ingekua ni bora zaid kwa mtazamo wenu?
Na km ni daily report ambayo lazima itumwe everyday je angesema nin huyu dada kwa bos wao kesho kazin?
Inawezekana hamjakutana na hii hal bado!
 
wewe unaelezwa ukweli lakini mbishi. Unaambiwa acha kuzoea kuwasiliana nasi mara kwa mara tulioolewa kaka ni hatari

Basi na nyie kuwen tayar kubeba mizigo yenu yote co mnataka msaidiwe kaz muweze attend family issue zenu kuwarithisha waume zenu visiran halafu shukuran ndo hii kuwaingza watu kwenye matatizo yasowahusu!
Utasikia "ooh naomba unsaidie kumalizia hapa nawah kujiandaa na mtoko na shemejio" asa huku nyuma mtu kakwama likaz ni lako asikutxt au kukupigia?anachelewa kuiwah familia yake kwa huruma yake tu anakusaidia kumaliza mikaz yako mpk saa 3 za usiku akikupigia cmu kwa manufaa yako amekosea!
Akina kaka wakiamua kuacha kuwasaidia kina dada maofisin weng hasa wenye waume visiran km wa huyu dada wataacha kaz au wataachika mana kila siku utachelewa kurud na hata huo mda wa kwenda mpokea mumeo airpot hautaupata!
 
Looh!! makubwa haya

Hata mim hili nimelishangaa mama angu husema "MUME/MKE WA KWANZA NI KAZI YAKO"
kwa mujibu wa huu hata iweje usiache kaz yako ambao ndo urith walokupa wazaz wako kupitia elimu kisa kumrithisha mwenz wako naye anapaswa kuithamin na kuishem kaz yako na wewe vile vile!
 
Afadhali umejua kuwa wewe ndiyo chanzo.

Ulipoona mumewe ameanza kuingiwa wasiwasi na wewe ulifanyaje? Hilo ndilo kosa lako la kwanza.

Hata wewe fikiria, mtu kaenda kumpokea mumewe toka safari,kwanza maana yake hawajaonana muda kiasi, halafu njia nzima anaongea na wewe, hadi anafika nyumbani anaongea na wewe, hadi saa 2 usiku?! Ungekuwa wewe ungejisikiaje?

Kulikua na ulazima gani wa wewe kumpigia simu hadi saa 2 usiku eti kisa unamsaidia kazi?
Maana hawakuweza kuongea habari zozote za familia yao hadi ulipokata simu, hivyo ni kama vile huyo dada alikua kazini tu, mumewe angeweza kwenda hata kwa tax nyumbani.

Kosa la huyo dada pia ni kukuendekeza, angeweza kukwambia kama huwezi kuifanya (maana ulimpigia simu mda wote aliokuwa anaifanya, hivyo ni kama aliifanya mwenyewe) ataifanya hiyo kazi mwenyewe siku iliyofuata ili apate muda wa kuwa na mumewe.

Inategemeana na kazi mkuu wengine kazi zetu hazilali na ukilaza jua kuna vitu kibao havifanyk na km ni Internationa Org ndo balaa mana unaweza kwamisha nchi kibao na ni bonge la msala ucpokuwa na sabab ya kueleweka na hukutoa taarifa inakula kwako mazma!
 
siwezi toa ushauri hapa maana nimesikiliza upende mmoja tu!
lakin vile vile hadi mtoto achezee sim na ikajipiga kuna kitu hapa nahisi mtoto alienda kwenye kitufe cha kupiga simu ambapo unaweza kukutana na sim zilizopigwa, naye kabonyeza pale sim ikajipiga! km mazingira ndo hayo inaonesha ulikuwa umeongea na huyo mke wa jamaa mda mfupi ulopita! mliongea nini? cheza mbali na ndoa ya mtu!
 
Angekuwa ni mtu mwenye busara angekubari nionane naye tuzungumze, nijuavyo mimi mtu anaweza akakumegea na hata ukimgundua anaendeleza jeuri hilo hajalifahamu, labda anasababu zake zingine

Mwachie mkewe amweleze. Wewe ili mradi umeshajaribu kuongea naye akawa anakataa na hasira zake bado ziko juu, ukiendelea kutaka kuongea naye utakuwa unamtibua zaidi. Pia, kosa si lako wala la mkewe, ni tatizo la mumewe kuwa na wivu uliopitiliza. Kuna wanaume wagumu sana, hawaamini kabisa mahusiano yanaweza kuishia kuwa ya kikazi peke yake.
 
Wadau mwenzenu nipo kwenye wakati mgumu sana psychologicaly, kuna dada anataka kuachika kwasababu yangu ilihali hana kosa lolote....Ishu iko hivi Kuna dada(mke wa mtu) nipo naye karibu sana kikazi, siku asipokuwepo ofisini kuna baadhi ya kazi zake hunachia nimsaidie namimi nisipokuwepo ofisini naye hunipa ushirikiano wa hivyo kutokana na nature ya kazi zetu kufanana sana.

Kutokana na ukaribu huu mmewe alianza kuwa na wasiwasi namimi, kwasababu kuna siku nilimpigia simu mkewe akapokea yeye bila hata kujibu salamu yangu akaniuliza shida yangu ni nini? mimi nikamueleza kwamba shida yangu ni ya kikazi nataka kuongea na mkewe,..... kumbe alikuwa naye jirani akampatia nikaongea naye, yalikuwa ni masuala ya kikazi tu yaliyohitaji ufafnuzi wa sekunde chache tu alafu zilikuwa ni saa za kazi, ishu ni kwamba huyu dada na mmewe walikuwa likizo.

Hivi majuzi huyu dada aliwahi kidogo kutoka ofisini kwasababu alikuwa anawahi kumpokea mmewe Airport alikuwa ametokea nje ya nchi kusimamia matibabu ya ndugu yake, all the way kwenda airpot na kuelekea nyumbani kwao tukawa tunawasiliana na huyu dada kuhusiana na vikazi alivyoniachia pale kazini nimsaidie mpaka nilipomaliza mida ya saa2 usiku.

Nikiwa nyumbani mida ya saa4 usiku mwanangu wa miaka3 alichukua simu yangu ikiwa chumbani mimi nikiwa sebureni akawa anaichezea, kwa bahati mbaya akapiga simu kwenda kwa yule dada ikapokelewa na mmewe kila akiongea simu yangu ilikuwa kimya maana alikuwa anaichea mtoto na hakujua kama kapiga simu. baadaye kidogo akapiga yeye, mwanangu akaniletea simu nilipoipokea kumbe ni yule bwana anapiga akaniambia maneno machache tu "HAJAKWAMBIA KWAMBA NIMERUDI? KUANZIA SASA NIMEKUACHIA" nilipojaribu kutaka kujua zaidi nini kinaendelea akanikatia simu, kila nikipiga simu ikawa haipokelewi, kwenye mida ya saa6 usiku akapiga yule dada akiwa amepigwa na kahifadhiwa kwa jirani ndipo nilipogundua nini kilitokea, nimejaribu kumuomba huyu jamaa tuonane tuongee ameniambia nikae mbali naye.

Wadau naombeni ushauri nimsaidieje huyu dada ili kuokoa ndoa yake maana jana amerudi nyumbani kwake lakini mmewe hamsemeshi kitu chochote, akijaribu kumuelewesha anamuambia aje kwangu yeye hataki kuishi naye, najisikia vibaya sana kwasababu mimi ndiyo chanzo na naofia maisha yangu kujisogeza kwenda kunusuru hii ndoa.

Angalia pia isilete shida kwenye ndoa yako, mkeo analijua hili?
 
huyo bwana ni mbumbumbu wa mapenzi, huyo ni mzinzi akidhani na mkwewe ndivyo alivyo, yaani mwizi huwaza kiwizi tu
 
Basi na nyie kuwen tayar kubeba mizigo yenu yote co mnataka msaidiwe kaz muweze attend family issue zenu kuwarithisha waume zenu visiran halafu shukuran ndo hii kuwaingza watu kwenye matatizo yasowahusu!
Utasikia "ooh naomba unsaidie kumalizia hapa nawah kujiandaa na mtoko na shemejio" asa huku nyuma mtu kakwama likaz ni lako asikutxt au kukupigia?anachelewa kuiwah familia yake kwa huruma yake tu anakusaidia kumaliza mikaz yako mpk saa 3 za usiku akikupigia cmu kwa manufaa yako amekosea!
Akina kaka wakiamua kuacha kuwasaidia kina dada maofisin weng hasa wenye waume visiran km wa huyu dada wataacha kaz au wataachika mana kila siku utachelewa kurud na hata huo mda wa kwenda mpokea mumeo airpot hautaupata!
Ndugu achana na mke wa mtu. Tunaweza ila nyie mnataka kujionyesha ufahari kuwa mko juu na mnaona fahari kutusaidia. Acha kabisa kutafuta ufahari. Mke wa mtu sumu
 
Mimi unanionea bure sina
mahusiano ya kimapenzi na mkeo, ninachokuomba ni unisamehe kwa ile Call
iliyopigwa kimakosa na mtoto

Mvaa Tai, we ngoja upigwe ndo akili zitakuja.Inavyoonyesha kuna vitu unatuficha! haiwezekani namba ya mtu ambaye huna mawasiliano ya mara kwa mara ikawa juu juu namna hiyo! we unamgongea umelikoroga ngoja ulinywe!
 
Last edited by a moderator:
Mimi unanionea bure sina
mahusiano ya kimapenzi na mkeo, ninachokuomba ni unisamehe kwa ile Call
iliyopigwa kimakosa na mtoto

Mvaa Tai, we ngoja upigwe ndo akili zitakuja.Inavyoonyesha kuna vitu unatuficha! haiwezekani namba ya mtu ambaye huna mawasiliano ya mara kwa mara ikawa juu juu namna hiyo! we unamgongea umelikoroga ngoja ulinywe!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom