Nauza shamba eka tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauza shamba eka tatu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Namdawa, Sep 6, 2011.

 1. N

  Namdawa Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nina shamba langu ambalo ninaliuza liko nje kidogo na Dar es salaam.Mkoa ni Pwani wilaya ya Kibaha.Sio mbali na barabarani.Sehemu lilipo Shamba hili ni eneo linajulikana sana kama Kwa Mbago.Lina ukubwa wa eka tatu.

  Kama uko na basi unashukia Visiga kwa kipofu.Ni sehemu ambayo kuna kuwa na trafic police wakati wote yaani wana usalama wa barabarani karibu sana kabla hujafika Mlandizi ukitokea Dar es salaam
  ni eneo ambalo linakuwa sana hivi sasa kuna barabara inafika hadi shambani kubwa imechongwa vizuri na watu hivi sasa wengi wamehamia huko.Maji pia na umeme vipo karibu.
  Kuna miti na bwawa nzuri ambalo lilikuwa linaandaliwa kwa kufuga samaki.Bado halijaisha ujenzi wake.Pia kuna nyumba ambayo ilijengwa ikifugia mifugo hivi sasa mifugo nimehamishia mahali pengine.Kuna matofali kiasi na mananasi kiasi.na pia kisima ambacho pia hakijaisha.Ni vitu ambavyo mtu anaweza kuanza kufanya vitu vyake sio kana kwamba ni vya lazima mtu kuviwekea maanani.

  Watu wengi wameanza kujenga na kuna miradi mingi inaendeshwa na ipo karibu na msitu wa serikali.Mbele yangu kuna watu wengi sana wanafanya miradi mbalimbali.Nimeamua kuuza si kwa sababu kuna tatizo hapana lakini Nimeshindwa kupaendeleza kutokana na majukumu niliyonayo kwa sasa.Nimelitumia zaidi ya miaka kadhaa.
  Ninaliuza kwa Tsh.milioni Ishirini.unaweza kuniandikia kwa email hii. nmuzeh@yahoo.co.uk
  Unaweza ukapiga simu 0712-308941 kwa wale ambao watapenda kwenda kuliona yuko dada ambaye analiangalia unaweza kupiga simu yake number 0714-031301 Karibuni
   
 2. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  asante mkuu
   
Loading...