Nauza mchele

ituganhila

Member
Aug 25, 2009
24
0
Habari wana jamii,

mimi ni mkulima ninao mchele mwingi nauza; mchele huu umelimwa hapahapa Tanzania. Kutokana na wingi wa mchele nilionao, utafaa kwa watu wengi kama shule na vyuo ambako wanafunzi ni wengi zaidi.
Kwa yeyote anayehitaji mchele kwa kiasi kikubwa tuwasiliane tafadhali. Aidha nakaribisha ushauri.

Ituganhila
 
Kaka, nimevutiwa na tangazo lako, sio kwa sababu mimi ni mnunuzi, la hasha, bali kwa kuwa niko katika maandalizi ya kulima mpunga.

Hongera kwa kulima na kufanikiwa kupata mchele mwingi.

Hata hivyo ningekushauri katika Tangazo lako uongeze taarifa zifuatazo: Mahali mchele ulipo, namna ambayo wateja watarajiwa (seriuos prospective buyers only) wanaweza ona sampuli ya mchele wako, kiasi gani cha mchele, kwa kilo, unacho, bei elekezi kwa kilo na mchele wako ni aina gani hasa ukizingatia kuwa Shule wanazingatia zaidi uwezo wa mchele kuvimba ukipikwa zaidi ya harufu.

Ninakutakia mafanikio mema!
 
Nahitaji kujua 1. Mahali mchele ulipo. 2. Bei ya mchele 3. Aina ya mchele (Mbegu) Na 4. unauza kuanzia kilo ngapi. Nasubiri jibu tafadhali
 
Hapa ndipo wajasariamali tunapokwama, tunatoa taarifa pungufu namna hii unategemea soko lako litakuwaje??
 
Hapa ndipo wajasariamali tunapokwama, tunatoa taarifa pungufu namna hii unategemea soko lako litakuwaje??

Nadhani Elimu ya Masoko, ikiwemo matumizi sahihi ya Mitandao kama huu kwa nyenzo ya Masoko, kwa Wakulima/Wajasiriamali wa hapa kwetu ni mchakato. Tuvumiliane, tuelimishane, tukumbushane na taratibu tutafika!
 
Nahitaji kujua 1. Mahali mchele ulipo. 2. Bei ya mchele 3. Aina ya mchele (Mbegu) Na 4. unauza kuanzia kilo ngapi. Nasubiri jibu tafadhali

Mimi niko hapa Dar na mawasiliano yanawezakufanyika nikakuletea sample 2. bei ni 1500 3. aina ni jamii ya supa hii ni supa saro 5 (4) ni kutokana na uwezo wako ningependa uanze na tani 5 na kuendelea hata tani 100 ukitaka. ninao

Nakushukuru kwa kuonesha nia.

ituganhila
 
Nadhani Elimu ya Masoko, ikiwemo matumizi sahihi ya Mitandao kama huu kwa nyenzo ya Masoko, kwa Wakulima/Wajasiriamali wa hapa kwetu ni mchakato. Tuvumiliane, tuelimishane, tukumbushane na taratibu tutafika!

Nakushukuru sana ndugu kwa kumuelimisha ndugu huyo; mimi nimelima nimepata mpunga nauza. nimefanya sehemu yangu kuufahamisha umma kuwa nina mchele nauza. wengine wameeelewa, wataelewa,wengine watabeza, wengine watadharau na wengine watafuatilia hasa wenye nia ya dhati. Wengine watawaelimisha wengine
 
Kaka, nimevutiwa na tangazo lako, sio kwa sababu mimi ni mnunuzi, la hasha, bali kwa kuwa niko katika maandalizi ya kulima mpunga.

Hongera kwa kulima na kufanikiwa kupata mchele mwingi.

Hata hivyo ningekushauri katika Tangazo lako uongeze taarifa zifuatazo: Mahali mchele ulipo, namna ambayo wateja watarajiwa (seriuos prospective buyers only) wanaweza ona sampuli ya mchele wako, kiasi gani cha mchele, kwa kilo, unacho, bei elekezi kwa kilo na mchele wako ni aina gani hasa ukizingatia kuwa Shule wanazingatia zaidi uwezo wa mchele kuvimba ukipikwa zaidi ya harufu.

Ninakutakia mafanikio mema!

Nakushukuru sana ndugu kwa kunielewa. mimi niko hapa Dar, naweza kuwasiliana nao na wakapa sapmle, Aina ya mchele ni supa saro 5 (Jamii ya supa) ni mzuri sana na una harufu nzuri utaupenda, mchele ni mwingi kiasi unachotaka ndo maana nikaelekeza kwa wenye shule au vyuo ikimaanisha kuwa mzigo ni mkubwa, bei ni Tshs 1500/=
Nakushukuru kwa kuonesha nia ya dhati na ushauri.
 
Hapa ndipo wajasariamali tunapokwama, tunatoa taarifa pungufu namna hii unategemea soko lako litakuwaje??

Nakushukuru ndugu, kumbe umeelewa kuwa na uza mchele. sasa ungeuliwa hizo taarifa zingine unazoona zimepungua ili nikueleweshe. huu ni mtandao wanajamii wanaingia na kutoka si sawa na gazeti(Newspapers) ambayo yakitoka lazima yawe na habari kamili.
Mapungufu unayo wewe ndugu uliza ujibiwe
 
Mkuu ,

kwa kushauriana tu kama siku nyingine ukija na tangazo - ili kupugnuza maswali mengi weka maelezo yakinifu. Nia ya wengi si kubeza ila kutoa changamoto. Ungesema

Nauza mchele kwa jumla- Mchele huu ni aina ya Super Saro , Bei elekezi ni Tsh 1500 kwa kilo (maelezo yapo kwa wanunuzi wakubwa), Kwa maelezo zaidi napatikana kwa namba hii 000000.

NB: Mbona 1500 ni bei kubwa sana kwa kuuza in Bulk (Jumla) ? think twice
 
Back
Top Bottom