Nauza gari yangu X5 (BMW)

Nauza gari yangu X5 (BMW)

hio gari yako ina multiple engines.....taratibu unakuja ninapotaka

Hahahaa, wewe naona unataka kumkimbiza mapema majaa, huenda kweli gari anayo lakini hajui specs kwa hiyo ameamua kugoogle na katika copy paste fasterfaster amejikuta amemix mambo! Kuna dogo mmoja alikujaga humu anauza lamborghini, maswali yalipoanza sijamuonaga tena JF mpaka leo!
 
karibia na saloon ya professor jay, ni pm namba yako. kesho njoo saa tisa jion ukishuka msasani mwisho niambie nije nikuchukue

na mimi kesho saa tisa jioni nakuja kuiona NJOO NAYO MSASANI MWISHO hapo kona ya kwenda shule ya msingi nitakuona bila kunipigia simu,nitakuja hapo saa tisa
 
Kumbe inawezekana??Mbona juzi ulinishambulia niliposema nahitaji Prado kwa 12ML ndo hivyo ukishikwa auangalii ulinunua bei gani au Market price!

Hahahaa, umesahau mkuu, rejea tena kwenye thread yako, sijakushambulia hata sehemu moja, mimi nilikuwa moja ya watu wachache sana waliokuwa wanakusupport! Mimi nadeal sana na magari mkuu, naelewa huwa zinatokea ndiyo maana nikawa nakutia moyo.
 
Japo bei haiendani na bei la soko la sasa kwa gari used ya 2013, lakini wengi tumeingia kwenye post hii kimakosa. Maana hatuwezi hata kununua Nissan March et al... Kaka MCHUNGUZI HURU wewe ni mzalendo mtoto wa mkulima au mzungu wa unga? Bei hiyo kaka ni sawa na bure.
 
Last edited by a moderator:
Upya wa gari ni millage sio maneno. Taja kilometa ilizotembea.

Kumbe kuwauzia bidhaa 'great thinker' iwe nzuri au boya inabidi usiwe na hasira na uwe tayari kujibu maswali ya maana na ya kijinga. Merry Xmas.
 
Japo bei haiendani na bei la soko la sasa kwa gari used ya 2013, lakini wengi tumeingia kwenye post hii kimakosa. Maana hatuwezi hata kununua Nissan March et al... Kaka MCHUNGUZI HURU wewe ni mzalendo mtoto wa mkulima au mzungu wa unga? Bei hiyo kaka ni sawa na bure.
Hiyo dharau ya wezekana wewe hata bodaboda huna unakuja hapa kuleta pang'ang'a wewe unajua humu kuna watu waina gani!Kwakuwa watu wanajua hata bei zake wanashangaa hii gari kuwa ya bei chee!yawezekana mbovu pia!!Ikifa central box inazo2 moja 8ml!bado kuzifanyia setting ziwe compatible na system ya gari kutokana na accessories zilizopo katika gari!inajua hapo ina turn bei gani??na siajabu Noble motors wakakwambia hatuna toa cash tuagize!
 
Japo bei haiendani na bei la soko la sasa kwa gari used ya 2013, lakini wengi tumeingia kwenye post hii kimakosa. Maana hatuwezi hata kununua Nissan March et al... Kaka MCHUNGUZI HURU wewe ni mzalendo mtoto wa mkulima au mzungu wa unga? Bei hiyo kaka ni sawa na bure.

usiseme watanzania ni masikini....sema mimi ni masikini....sikumbuki nani alisema maneno haya ila naamini alilenga watu kama wewe...
 
Hivi kweli upo serious au unaleta utani hapa. X5 ya 2013 kwa milioni 48 za kitanzania? Hebu niambie upo Msasani sehemu gani nikutembelee kesho Alhamisi tarehe 26 December 2013 ili niione hiyo gari.

Tiba
Upo sahihi sana ila nadhani hapa tunatofautiana maana halisi ya neno gari jipya, maana kununua mwaka huu si lazima liwe la mwaka huuu, kwa BMW X5 ya 2013 huwezi pata wa bei hiyo.Sasa sijui muuzaji yeye anaelewa nini swala hili ndio maana hakutaka hata kutaja mwaka wa gari kwenye maada yake pale juu
 
Mkiambiwa mnunue Toyota mnasema gari la being rahisi. Haya sasa utamuuzia nani huo msiba wa x5? Acheni kuiga, nunua gari za kijapani na hutapata shida kuliuza.

Mkuu ushawahi kuingia kwenye Bimmer lakini? Nafikiri toyota utasahau km ina exist..... Kitu kama upo ndani ya ndege first class.... Toyota utafanya service kila trip... BMW utasahau sema ikidai service nayo maumivu... Lkn km una miliki la 2013 utashindwa kupiga service kweli? Watu wengine wana prefer gari za uhakika sio mkusanyiko wa vyuma toyota...
 
usiseme watanzania ni masikini....sema mimi ni masikini....sikumbuki nani alisema maneno haya ila naamini alilenga watu kama wewe...

MKuu hamjaleta mrejesho, wewe na Tiba wote mlisema mtaenda kulicheki, au jamaa alitokomea?!!
 
Last edited by a moderator:
MKuu hamjaleta mrejesho, wewe na Tiba wote mlisema mtaenda kulicheki, au jamaa alitokomea?!!

wala sikutaka kupoteza muda....sijaenda coz hakuna 2013 bmw X5 ya tsh 48M....angesema ana shida kama kidney transplant sawa...sio kuleta gari ingine ndio bmw X5 2013 kwa 48m....naamini huyu jamaa ana X5 ya 2001-2004 ila kaileta tanzania miezi sita iliopita ndio anasema 'mpya'
 
Mkiambiwa mnunue Toyota mnasema gari la being rahisi. Haya sasa utamuuzia nani huo msiba wa x5? Acheni kuiga, nunua gari za kijapani na hutapata shida kuliuza.

Watu wengine mna mawazo mgando sana, mimi nina ford sedan na sina mpango wa kuuza labda after 25yrs
 
M
wala sikutaka kupoteza muda....sijaenda coz hakuna 2013 bmw X5 ya tsh 48M....angesema ana shida kama kidney transplant sawa...sio kuleta gari ingine ndio bmw X5 2013 kwa 48m....naamini huyu jamaa ana X5 ya 2001-2004 ila kaileta tanzania miezi sita iliopita ndio anasema 'mpya'
Mkuu ungemwambia hata aje nayo tu labda, things change sana kuna kama hiyo BMW X5 ya 2011nimeshuhudia kwa macho yangu inauzwa kwa mnada AD$27,000 kama tsh 39m last thursday kupitia hapa www.pickles.com.au mnada wa magari ya serikali ya huku
 
hio usd 27,000 inakaribia 48m na hio ni huko haijafika hapa uilipie ushuru na 2011 sasa 2013 kailipia na ushuru inakuwa ngumu kuamini
 
Nilinunua mpya kabisa kutoka ujerumani, nimetumia miezi sita tu. nauza milioni 48. kiukweli haipungui bei kabisa kwakuwa naiamini sana hii gari. napatikana msasani, nauza kwakuwa nimeagiza gari nyingine inaingia mapema mwakan. tuma pm kama unahitaji

Unaposema mpya kabisa una maanisha umeinunua iko na 0km na umeitumia kwa miezi 6 tu?

odometer inasomaje sasa hivi? pia kama walivosema wengine, weka picha!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom