Naungana na nchi ya Kazakhstan, tuwe na siku 4 za kazi na 3 za mapumziko

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,035
49,718
Kwa wale Waislamu inatakiwa Muunge Mkono pendekezo la Siku ya Ijumaa kujumuishwa kama public holiday yaani Weekend hakuna kufanya kazi.

Kwa nini Jumapili na Jumamosi ni Weekend na sio Ijumaa?

Hii itakuwa nzuri sana Kwa Wafanyakazi pia.

============

walking-through-astana-kazakhstan-1.jpg

Nchi ya Kazakhstan iko mbioni kupitisha mpango wa kuwa na siku nne za kufanya kazi kwa juma moja. Taifa hilo la Asia ya Kati litatekeleza hatua hiyo kuanzia Julai 1 mwaka huu na tayari watu wameanza kuwa na hisia tofauti juu ya mpango huo.

Kuna wale ambao wanaeleza uwapo wa mkanganyiko wa jinsi jambo hilo litakavyofanya kazi huku wengine wakifurahia mpango huo. Hata hivyo sheria iliyopo sasa inashinikiza kuwa Jumapili ni siku ya mapumziko bila kujali makubaliano ya namna yoyote.

Aidha, utekelezaji wa mpango huo utawawezesha waajiri kujadili jinsi ya kufanya kazi na wafanyakazi ili kupata siku hizo nne.
 
Kwanza inabidi utambue kuwa siku aliyotupatia Mungu ya kupumzika ni moja tu yaani ya saba na kila wakijaribu kuipoteza identit ya Mungu huwa wanashindwa, maana nddio utambulisho wa Mungu.

Ndio maana tumelazimika kuwa na siku mbili kwa sababu kuna original na fake. Kwa hiyo kila jitihada zinazofanyika ili kuwe na siku moja ya kupumzika TOFAUTI NA SIKU ALIYOWEKA MUNGU MWENYEWE MAMBO HUWA YANASHINDIKANA.

Kwa hiyo inatupasa tumrejee Muumba na kufuata taratibu za Mbinguni.
 
Dunia ya leo hata hizo jumamosi na jumapili siku hizi tunaingia mzigoni, unakwenda kuabudu ukitoka straight kwenye hustle, wengine mnataka siku za kufanya kazi zipunguzwe.
 
Allah Hataki Mapumziko!

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

[ AL - JUMUA' - 10 ]
Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.

Hivyo kudai Mapumziko ni ukafiri
 
Dunia ya leo hata hizo jumamosi na jumapili siku hizi tunaingia mzigoni, unakwenda kuabudu ukitoka straight kwenye hustle, wengine mnataka siku za kufanya kazi zipunguzwe.
Ni wewe umechagua ila sie Watumishi hatuendi
 
Kwanza inabidi utambue kuwa siku aliyotupatia Mungu ya kupumzika ni moja tu yaani ya saba na kila wakijaribu kuipoteza identit ya Mungu huwa wanashindwa, maana nddio utambulisho wa Mungu.

Ndio maana tumelazimika kuwa na siku mbili kwa sababu kuna original na fake. Kwa hiyo kila jitihada zinazofanyika ili kuwe na siku moja ya kupumzika TOFAUTI NA SIKU ALIYOWEKA MUNGU MWENYEWE MAMBO HUWA YANASHINDIKANA.

Kwa hiyo inatupasa tumrejee Muumba na kufuata taratibu za Mbinguni.
Siku ya saba ni ijumaa lakini Mkuu
 
Back
Top Bottom