Nauliza: Mbwembwe za Makinikia zimeishia wapi?

Nauliza: Mbwembwe za Makinikia zimeishia wapi?

Kama mada inavyojieleza
Rais Magufuli alikuja na mbwembwe kibao kukamata makinikia na kudai matrilioni ya shilingi kutoka kwa Acacia/Barrick

Tukaahidiwa kulipwa kishika uchumba cha bilioni 700
Nashangaa hadi Leo kimya, sijui mazungumzo yameishia wapi

Habari za makinikia zimefutika masikioni mwa watanzania sasa ni habari za bilionea dokta shika

Naskia na ile ndege yetu ya Boeing dreamliner nayo inaviziwa ikamatwe kisa tunadaiwa

Makinikia yameishia wapi jamani au zilikua mbwembwe tu za Sizonje a.k.a mzee kipara kutafuta kiki na tumwone mzalendo kumbe mzalendo uchwara

Ova[emoji41] [emoji41] [emoji41]
haya mambo sio rahisi kama unavyoenda kununua viroba kichochoroni kisha unavamia jukwaa kuandika pumba, hili ni suala la kitaifa lina taratibu zake wakimaliza utaambiwa kwa utaratibu serilakali haibadili gia angani inafuata utaratibu
 
Kiongozi hajui kimombo unategemea nini wkt alikuwa haelewi kilichokuwa kinajadiliwa
 
Hivi hitimisho za Yale mazungumzo hukusikia? Au ulikuwa busy kwa mange kimambi
 
Unaishi kwenye ulimwengu gani? Hujasikia kuwa na drealiner ipo njiani kupokonywa huko USA? Watu hawaendi mahakamani kwa kukurupuka. Huna uhakika kama Barrick/Acacia hawataenda mahakamni.

Kumbuka kilichosainiwa ni mapendekezo tu. Mapendekezo hayo yasipokubaliwa na Barrick na Board ya Acacia, serikali itafanya nini? Serikali ikichukua uamuzi wowote ule baada ya mapendekezo kukataliwa, Acacia watafanya nini?

Tuliaswa, tukapuuzwa.
Huwa nawaza Accasia wanaplan nn baada ya haya yote. Naiona hatari hawa jamaaa wanafanya hesabu zao waje waseme tumewasababishia hasara ya trillions of TZS na watataka tuwalipe.

Mzungu sio kuwa anaakili sana ila anajua anachofanya na anajua akifanye wakati gani.
 
Bora waseme twende na viroba tukagawane huo mchanga maana tunaweza kuambulia chochote.kuuacha pale bandari kunadababisha msongamano usiokuwa wa lazima na kuozesha makontena amabayo tungeyatumia kufungulia biashara badala ya kujenga frame
 
Ule ulikuwa wimbo wa Bongo flavor. Umeisha chuja.
Sasa Tusubiri wimbo mwingine. Tutaitwa Ikulu kumsikiliza muongeaji mwenye wingi wa "busara, hekima na maono"

Katika kipindi hiki cha mpito tukisubiri single nyingine, tuwe wavumilivu, watulivu na wapenda amani kama siku zote.
Single inayovuma sasa hivi ni ya ununuzi wa wanasihasa na viongozi wa upingaji na madalali wa ununuzi kupandishwa vyeo. Live ya kwanza tayari subiri inayofuata amesema wapo wengi. Hukusikia kile kibwagizo "... wako wapi? Wapumbafu kabisa" Mustafa wa miaka 69 naye kapewa unyumbakumi licha ya umri kutoruhusu
 
Hivi wewe hujiulizi kwanini mpaka leo serikali imepata kigugumizi kusema chochote kuhusu yale Makontena ya mchanga wa dhahabu pale Bandarini.

Je, bado tunayashikiria?
Je, tumewapa Acacia?
Je, nini hatma yake?
 
Watanzania tunaishi kwa matukio yote hayo kwa sababu ya CCM, makinikia yameisha tumehamia kununua wanachama wa vyama vya upinzani nalo litaisha
 
Watu wameshapewa chao,hakuna ishu tena.mi nasema hakuna enzi ambayo Tanzania inaibiwa kama hii enzi ya awamu ya 5.tunaibiwa nyie acheni tu.
 
Kama mada inavyojieleza
Rais Magufuli alikuja na mbwembwe kibao kukamata makinikia na kudai matrilioni ya shilingi kutoka kwa Acacia/Barrick

Tukaahidiwa kulipwa kishika uchumba cha bilioni 700
Nashangaa hadi Leo kimya, sijui mazungumzo yameishia wapi

Habari za makinikia zimefutika masikioni mwa watanzania sasa ni habari za bilionea dokta shika

Naskia na ile ndege yetu ya Boeing dreamliner nayo inaviziwa ikamatwe kisa tunadaiwa

Makinikia yameishia wapi jamani au zilikua mbwembwe tu za Sizonje a.k.a mzee kipara kutafuta kiki na tumwone mzalendo kumbe mzalendo uchwara

Ova[emoji41] [emoji41] [emoji41]
usomagi magazeti au kufatilia yanao endelea au unataka kila siku yawe wimbo wa taifa.
 
waliokuwa wanaleta mbwembwe ktk masuala ya msingi kabisa ya kitaifa, ni wale waliotaka kujiimarisha kisiasa kupitia kazi zinazofanywa na serikali.
Wale waliotishia kwamba tutashitakiwa ktk mahakama za kimataifa, lakini leo imekuwa tofauti na maono yao hasi, na mbwembwe zikapungua.
Kwani hatujashtakiwa mkuu, Mbona ndege yetu imezuiliwa kwa amri ya mahakama
 
Timu ya majadiliano ya wazalendo iliyoundwa na Mheshimiwa Raisi ilikutana na timu ya yule "mwanaume" kutoka Barrick wakajadiliana kwa takriban miezi miwili na baada ya hapo timu yetu ikaibuka na ushindi wa kishindo wa kuweza kushusha makadirio ya awali ya kulipwa USD 194 billion na kupata kishika uchumba cha USD 300 million. Aidha Tuliwashika pabaya mpaka wakakubali kugawana faida ya kiuchumi (Economic profit) nusu kwa nusu yaani wao 50% na sisi 50% ikihusisha pia umiliki wa mitaji wa migodi yao kwa asilimia 16. Na hayo ni makubaliano ya awali kwani bado kuna masuala ya kodi ambayo kulikuwa na mazungumzo ya kufikia muafaka unaonufaisha pande zote - wenyewe wanaita win win deal. Na kwa taarifa yako timu yetu ya wazalendo waliowagalagaza timu ya hawa wanyonyaji wa Barrick na ndugu zao Acacia wamepewa nishani kutambua mchango wao mkubwa kwenye mapinduzi ya sekta ya madini nchini. Nadhani nimekuelimisha kiasi cha kutosha.
 
Kama mada inavyojieleza
Rais Magufuli alikuja na mbwembwe kibao kukamata makinikia na kudai matrilioni ya shilingi kutoka kwa Acacia/Barrick

Tukaahidiwa kulipwa kishika uchumba cha bilioni 700
Nashangaa hadi Leo kimya, sijui mazungumzo yameishia wapi

Habari za makinikia zimefutika masikioni mwa watanzania sasa ni habari za bilionea dokta shika

Naskia na ile ndege yetu ya Boeing dreamliner nayo inaviziwa ikamatwe kisa tunadaiwa

Makinikia yameishia wapi jamani au zilikua mbwembwe tu za Sizonje a.k.a mzee kipara kutafuta kiki na tumwone mzalendo kumbe mzalendo uchwara

Ova[emoji41] [emoji41] [emoji41]
Ulikuwa umelala?kama vile umekurupuka usingizini.tumeshalipwa sehemu ya hela na maboss wao wengine wame resign.we kiboko....!
 
Ulikuwa umelala?kama vile umekurupuka usingizini.tumeshalipwa sehemu ya hela na maboss wao wengine wame resign.we kiboko....!
Tumelipwa lini broo acha kujisemea tu, hata harufu ya hiyo hela hatuisikii ww unasema tushalipwa alaa
 
Hapo sasa?! Labda wamelipa $300m, labda tushaanza kugawana faida 50-50, labda kweli tuna asilimia zetu 16, au ?!
 
Kuna watu bado wanasubiri Noah kama wanavyosubiri 50,000,000/= kwa kila kijiji? Endeleeni kusubiri meli jangwani! Sometimes miracles do happen! Of cause ikitokea kila mmoja atafurahi! Unaonaje furaha ya kupanda meli kwenye jangwa la sahara!
 
Back
Top Bottom