Nauliza jamani, kuna ubaya wowote ukimuomba mwajiri akupe job description

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
892
293
Hello wana jf! Ndugu zangu mimi ni mgeni ktk swala ajira, mnisaidie kama kuna umuhmu wa kudai job descriptn from the employer, na je mwajiri akikufanyisha kazi nje na job description unahtajika kuchukua hatua gani?
 
Kha! Sasa unafanyeje kazi bila kuwa na JD? Au Ndio hio experience inayotajwa Kila siku? HR ndio responsible person WA kukupatia JD
 
Mara nyingi hizi JD ya mwisho kabisa wanasema na kazi nyingine utakazo pangiwa na mkuu wako
 
Lengo langu ni hatua zipi utachukua endapo mwajiri amekupa kazi ambayo haiendani kabisa na skills wala haiendani na kilicholengwa kuajiriwa zako/it undervalue you
Mara nyingi hizi JD ya mwisho kabisa wanasema na kazi nyingine utakazo pangiwa na mkuu wako
 
mkuu wala si vibaya kuomba JD kwa sababu itakusaidia kujua hata kazi zilizoongezeka tena JD inatakiwa muwe mnapewa kla baada ya muda fulan kwa sababu kazi mara nyingine zinaongezeka sasa usipokua aware unaeza sema mbona hii si kazi yangu kama JD ya awali inavyoeleza kumbe ni sahihi wewe kufanya ile kazi kutokana na changes zinazotokea
 
Lengo langu ni hatua zipi utachukua endapo mwajiri amekupa kazi ambayo haiendani kabisa na skills wala haiendani na kilicholengwa kuajiriwa zako/it undervalue you

Embu tupe mfano wa hicho kitu anachokutuma na kinakuundervalue? Au tuseme mfano we muhasibu halafu anakutuma uwe dereva? Dadavua mkuu
 
Ni muhimu sana ila kwa zamu hizi za ukosefu wa Ajira unaweza ukawa unaweka rehani kibarua chako.
 
Hello wana jf! Ndugu zangu mimi ni mgeni ktk swala ajira, mnisaidie kama kuna umuhmu wa kudai job descriptn from the employer, na je mwajiri akikufanyisha kazi nje na job description unahtajika kuchukua hatua gani?
Hivi wewe unafanya kazi bila JD unategemea nini. Kuna siku mwajiri atakuambia umfulie nguo zake za huko chini kwake na hutaweza kumbishia kwa kuwa huna JD na atakuambia hayo ni sehemu ya majukumu yako.
 
Job description ni guidelines tu na ni statick. Waajiri wameenda mbele zaidi na kuandaa workplans na appraisal tools ambazo zinatafsiri utendaji wako wa kazi wa kila siku na kutumika kama kipimo chako cha ufanisi. Ungekuwa kwangu ningekutwisha vyote ujue unachodai kinaweza kuwa na madhara.
 
Kuna ofisi nyingine huwa wanatoa kwa kila mtumishi kila unapoisha mwaka wa fedha na vikao vya makisio ya mapato na matumizi ili kila inapofika julai mosi kila mtumishi anajua anawajibikaje.omba tu mkuu ni haki yako wala sio tatizo.
 
Je' ajira yako ni 'private or public' kama ni serikalini barua yako ya ajira ilipaswa kuambatanishwa na JD. Ni haki yako!
 
Ushauri wenu ni wa maana sana, japo mmeniweka njia panda kutokana na wengne kukataa na wengne kukubali, kwa ujumla nalenga private sector, nimeamua kuomba ushauri baada ya kuona nimekuwa namfanyia mwajiri/bossi kazi zake binafsi out of the company works ie sending me to his home, making his personal transaction etc! Modes naombeni mniunganishie hi comment pamoja na topic angu, asanteni!
 
Kha! Sasa unafanyeje kazi bila kuwa na JD? Au Ndio hio experience inayotajwa Kila siku? HR ndio responsible person WA kukupatia JD

Sasa bila job description unafanyaje kazi? Utendaji wako unapimwa kwa kutumia kigezo gani? Job description under normal cirumstances inatolewa na hiring unit na copy inawekwa kwenye personal file la mfanyakazi na HR. Kila mfanyakazi lazima awe na job description labda kwenye set up za kitanzania ambapo mambo yanafanyika kwa mazoea tu.

Tiba
 
Hello wana jf! Ndugu zangu mimi ni mgeni ktk swala ajira, mnisaidie kama kuna umuhmu wa kudai job descriptn from the employer, na je mwajiri akikufanyisha kazi nje na job description unahtajika kuchukua hatua gani?

hakuna mwajiri anayependa ujue hiyo kitu.
 
Mkuu hujasema upo sekta ipi, ama ni dereva, au ni nani. Pia naona kama vile wewe ni mtata, unasema ni mgeni katika ajira, wakati huo huo unataka kumchukulia bosi wako HATUA, kuwa makini, unaweza usifike mbali. Cha msingi, fanya kazi za watu kutokana na unavyotumwa, kama hujaridhika na hiyo kazi achana nayo, tafuta nyingine. Kwa hizo hatua unazopanga, utajipitezea muda na uhaminifu kazini kwako
 
Asante sana, bora nifuate ushauri wako!

JD lazima we unaye kataa ndio unae take oppotunity hata kulala na wafanyakaz if u knw somethng isn't right speak it out even if ur minority ....
 
Back
Top Bottom