Miaka 10 bila Tanzania Institute Hospital, niliyoyasikia, kuyaona na kusimuliwa na miaka 9 bila gwiji wa moyo nchini Dr. Masau

Papaa pedeshee

JF-Expert Member
Nov 7, 2021
234
337
Tarehe 12 mwezi Aprili mwaka 2012 ukiwa usiku wa manene mithili ya mwizi anayevamia nyumba fulani ili kutimiza hadhima yake, hakika ilikuwa ni siku mbaya iliyoleta machungu makubwa sana kwa waliokuwa wafanyakazi wa Taasisi ya magonjwa moyo (THI) kupoteza ajira zao na vitu vyao binafsi baada ya taasisi hiyo kufungwa na wenye jengo bila hata watumishi hao kupewa taarifa yoyote aidha toka kwa mwajiri au taasisi ya Nssf iliyofunga jengo hilo baada ya mgogoro huo kusemekana ulitolewa maamuzi na mahakama huku mtendaji mkuu alidai jambo hilo bado lilikuwa halijafika mwisho kwa kuwa alikuwa hajapewa notisi husika.

Kufungwa kwa THI hakukuathiri watumishi pekee bali pia iliathiri wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodini na baadhi yao wakisubili upasuaji jambo ambalo liliwaathiri vibaya sana hata kisaikolojia.kadhia hiyo ilisababisha wengine kufariki ghafla kwa kuwa ni jambo ambalo hawakutegemea mbali ya kuhamishiwa ktk hospitali mbali mbali ambazo wagonjwa wenyewe hawajaenda huko awali kupata tiba badala yake walitibiwa THI,hivyo kuwapeleka huko tena bila ridhaa yao,hakika hawakutendewa haki kabisa.

Pamoja na wagonjwa kuhamishwa kwa nguvu bila ridhaa yao na hata bila ndugu kufahamishwa chochote,hakika ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa haki ya mgonjwa kutibiwa apendapo.hakika niseme wazi, kama ndugu wa wagonjwa wangechukua hatua ya kushitaki taasisi hiyo tena ikiwa imesababisha baadhi ya vifo vya wagonjwa,ni dhahili haki stahili ingepatikana kwa kuwa utaratibu wa kuwaondoa wagonjwa haukufuata utaratibu mzuri ikiwemo wagonjwa kupewa taarifa za awali juu ya kadhia iliyokuwepo endapo hawakuona busara ya kuja kuongea na watumishi ili pia waondoe vitu vyao binafsi kwani wafanyakazi wengi waliifadhi mali/ vitu vyao ofsini jambo ambalo halikufanyika wala hata siku ya kufungwa hawakuruhusiwa kuingia mtu yeyote,unyama wa ajabu sana waliofanyiwa watumishi na hasa wagonjwa na ndugu zao.

Imekuwa bahati mbaya sana pale mtanzania unapoonewa, kunyanyaswa,kuvunjiwa utu na ubinadamu na mengineyo kushindwa kujaribu kuchukua hatua stahili ikiwemo kudai haki yako,naamini ktk hili la THI kuna watu walitakiwa kufidiwa kwa kutwezwa utu wao ila hawakuchukua hatua,wakimwachia Mungu Baba muweza wa yote awe juu yao.

KUSAMBAA KWA TAARIFA: naamini siku ya kufungwa kwa THI, taarifa zake zilifunikwa zaidi kutokana na msiba wa msanii maarufu nchini marehemu Kanumba kwa kuwa ndiyo siku aliyokuwa akiagwa ktk viwanja vya LEADERS vilivyokuwa karibu sana na taasisi hiyo na kuzikwa ktk makaburi ya kinondoni, hivyo vyombo vyote vya habari zaidi ya 98% vilitekwa na tukio hilo la aina yake ya kuondokewa na gwiji wa nguzo ya filamu nchini. Hata hivyo gazeti la Ijumaa,linalomilikiwa na GLOBAL PUBLISHERS lilifanya kazi ipasavyo, Heko na shukurani ziwaendee kwao kwa kazi nzuri waliyoifanya lakini pia mitandao ya kijamii ikiwemo jamii forum na wengineo kwa kadiri walivyoweza ktk kuhabarisha umma.

NILIYOYASIKIA: siku ya kufungwa kwa taasisi hiyo, nikiwa nimesimama nje ya lango na watumishi wengine,mita chache na wenzangu,nikiwa karibu na kijana mmoja aliyesimamia zoezi la kufungwa na aliyewahi kuhudhuria hospitalini hapo kwa kuwa nduguye kama sikosei alikuwa ni babu yake,akitibiwa maradhi aliyokuwa nayo na nilimtambua kwa sura,nadhani alikuwa ni mtu wa kitengo maalumu kama vijana wasemavyo kutokana na mazungumzo yake. alisikika na nilimsikia akiongea na Aunt yake aliyeko Tabora na simu yake ikitoa sauti yakusikia,nilijisogea karibu zaidi na yafuatayo ni haya;
kijana: Aunt shikamoo! Habari ya huko Tabora.
Aunt: marahaba mwanangu, mnaendeleaje huko?
kijana: huku aunt hatujambo japo c sana.
Aunt: kuna nini?
kijana: Aunt, Dr.Masau anafanyiwa unyama wa ajabu, taasisi yake imefungwa.
Aunt: kwann mnamfanyia hivyo jamani!
Kijana: shangazi hata mimi naumia sana ila basi tu,ukizingatia Dr.Masau alimtibu vizuri mzee wetu. Ikulu hawataki kuiona hiyo taasisi kabisa.nami sina jinsi shangazi maana Dr.Masau alimtibu mzee wetu. Sina cha kufanya,nimajukumu ya kiofisi aunt ila naumia,wakubwa hawataki kuiona THI.
Aunt: jamani! Jamani!
Kijana: ndio hivyo aunt.baadaye.

Mwisho wa yale niliyoyasikia ktk mazungumzo ya watu hao.

Mengine niliyoyasikia ni tajiri mmoja mwenye hosipitali yake maeneo ya fire japo kwa sasa marehemu, akiwa na Prado silver,nikiwa miongoni mwa watumishi kama watatu,akisema tusiwe na wasiwasi kwa watumishi wote wa THI atawajiri na Appolo hospital ya moyo itahamia hapo.

Baada ya kuona kazi iliyoleta na kushuhudia wagonjwa waliokuwa wakihamishwa THI, jengo likiwa na maandishi, " jengo hili limeshatapata mwekezaji mpya,ni mali ya Nssf" kisha tajiri huyo na mdau mkubwa wa kada ya afya baada ya kuona vile aliondoka akijua kazi yake imekwisha.

Baada ya kuona trela ilivyokwenda,hakika nilisikitika,niliuzunika,niliumia sana,kumbe mbali na mgogo wa kudaiana juu ya pande hizo mbili,kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na wenye nchi,wenye mipango, wenye nguvu za ajabu kuhakikisha THI haitakuwepo tena kwa kivuli cha kudaiwa kodi ya pango huku wao michoro iliyokusudiwa ilikosewa na kuamuliwa na wafadhili wakuu wa THI warudie ili kuweza kulipa kodia hiyo,jambo ambalo wahusika hawakukubali kwa kuwa mwana THI hakutoa chochote, pengine hakutanguliza ahsante kwa wale wachache wazee wa percent,hawakuwa wengi,bali wachache tu na baadhi walidiriki kuomba hata hongo ya kufikia deni la michango ya watumishi ili wafukie makaburi,jamaa akakataa,mtu nne zikiwa zimefika ofisin kwa Dr.akawatolea nje,wakaondoka wanyonge sana,bati nzuri niliwaona baada ya kuitwa wakiondoka. Dr.apumzike kwa amani huko aliko na asamehewe yake madhaifu kama tulivyo binadamu wengine.

KUSUDIO LA KUKATA RUFAA: ni ukweli usiopingika na mtu anaweza kuhoji kuwa kama alionewa au THI ilionewa,kwann hakukata rufaa? Baada ya kufungwa kwa taasisi, mkurugenzi alijaribu kuwasiliana na mtetezi wake, majibu aliyopewa hayakuwa ya utetezi,ya mtu na mteja wake kabisa! Hata hivyo Dr.masau hakukata tamaa, alimuona jaji wa mahakama ya rufaa nyumbani kwake personally kwa ushauri, alipata mawaidha mazuri, aliwaona mawakili wengine akiwemo mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mpoki na wengineo, na wote hao walishauri akate rufaa,kwani moja ya kipengele cha mkataba ilikuwa kumaliza meza ya mazungumzo endapo mgogoro umetokea,na mengineyo ambayo waliona THI inastahili, je ilikuwaje? Masikini THI haikuwa na pesa tena hata kusonga mbele, ilibaki mithili ya yatima tu.

Wakati THI ikihaha huku na kule, ajabu, mtetezi wake aliyeaminiwa na Dr.akaibuka na kumshawishi Dr.Masau kutokata rufaa eti wenye jengo wamesema watampa vitu vyake vyote na wao wanachotaka ni jengo lao tu,masikini Dr.,mkurugenzi wangu,kumbe hakujua alikuwa anatafutiwa usemi wa from hero to zero! Dr.kwa kuamini tena,eti mtu wa nyumbani,kabila fulani! Akaacha kukata rufaa, akatafuta jengo akapata jengo karibu na kituo cha ubalozi wa Ufaransa,gharama kwa mwezi 60million, akajiuliza kama ataweza,akasema ngoja asubili vitu, kumbe mtego wa siku 14 kama sikosei za kukata rufaa mahakamani angeliona yafaa, kumbe mtego bhana! Akashawishiwa na mtetezi wake,akaingia kumi na nane,siku zikayoyoma,zikaisha,mnada ukatangazwa na vitu vikauzwa,akahamaki mbali na yeye kununua vyakuanzia ktk hatua nyingine huko mbeleni,bahati mbaya lengo halikutimia ipasavyo, akaondoka gwiji wa moyo Tanzania, mratibu wa magonjwa ya moyo Africa na makamu wa Rais wa shirikisho la moyo duniani kwa nyakati mbili tofauti,akiicha ofisi ndogo ya THI huko hospitali ya moyo Texas Marekani ambao walikuwa wadau wakubwa wa THI kwa asilimia kubwa kwa kutoa wataalumu bobezi wa moyo wakisaidiana na ujerumani na vifaa tiba kwa nyakati zote za uwepo wa THI.

Mungu ampumzishe Dr.masau,Mungu awakumbuke wana THI popote walipo kwa uzalendo wao kwa Taifa.je nikisema kulikuwa na harufu ya rushwa kwa upande fulani nitakosea? Sina maana kuna mtu alipokea rushwa toka mahala Lah! Mungu pekee ndio mwenye hukumu ya kweli na mwenye kuona mambo yote yaliyoko gizani na kufunuliwa nuruni,huku duniani mapito yenye hukumu za michongo ni mingi japo zipo hukumu nyingi zenye haki na ieleweke hivyo,nisinukuliwe vibaya ndugu zangu.

Matibabu ya bure: kufungwa kwa THI kuliacha simanzi na huzuni mkubwa kwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakitibiwa THI bila malipo yoyote kutokana na Uduni na kukoswa pesa ya kujitibu ndani ya familia zao,hivyo taasisi ilibeba dhamana hiyo,kwani kauli mbiu ya Dr.Masau ilichagizwa na neno, " TOKA MOYONI KWA AJILI YA MOYO" hivyo kwake utu na ubinadamu ulikuwa nguzo muhimu sana badala ya fedha na masilahi yake.
Maswali niliyojiuliza;

1. Je maamuzi ya kuiondoa na kuifuta THI yalikuwa sahihi kweli?

2.Ikulu ni taasisi pana ndiyo,ikiwa ni serikali ya awamu ya nne, je ni mkubwa gani hakutaka kuiona THI ikiwepo? Ikiwahudumia watanzania hasa wa hali ya chini? Japo na wageni nje ya nchi walitibiwa.nadhani hapa mhusika huko aliko kama yu hai basi anakijua vema badala ya mm kubashiri tu.

3. Je kwann yule mhindi, mwenye hospitali maeneo ya fire japo sasa ni marehemu,Mungu amurehemu huko aliko,kwann hakuchukua tena jengo kama alivyoahidi kwa wana THI? Badala yake alijengewa jengo na taasisi fulani ya umma kwa makubaliano fulani fulani hivi,hizi ni tetesi zilizovuma kipindi cha nyuma na hata mtandaoni kama sikosei.tetesi zingine kushindwa kuchukua jengo ni gharama kubwa alizoambiwa,mhindi akaachana na mchongo huo.

4. Je Dr.kutokuwa upande wa wapiga percent ndio gharama ya kuipoteza THI?

5. Je haikuitajika taasisi nyingine mbadala hapa nchini ya moyo kama zilivyo taasisi au hospitali zingine?

6. Je vitu vilivyouzwa,viliwezesha wadai kujilipa pesa yao? Jibu ni hapana, taasisi ilikuwa na thamani ya zaidi ya 10 billion kwa mwaka 2010 lakini mauzo ya vitu vile hayakufikia hata 500M kwa kuwa ktk minada takribani yote nilishuhudia.

7. Je mtetezi wa THI alikuwa na maana gani kumshawishi na kumlaghai De.Masau kuachana na wazo la kukata rufaa?

8. Je lugha za kejeli na maneno yasiyo na mtu na mteja wake japo sijayaimisha hapa, je yalikuwa yakiungwana? Yalikuwa yanaashiria nn? Je alikuwa ni mtu sahihi ktk uadilifu wa taaluma yake? Mungu na atuhukumu kadiri itakavyofaa kwa matendo yetu

9.maswali ni mengi mno; nimalize kwa kusema,kilio kwa wana THI kilikuwa kikubwa sana na hasa kwa DR.mzalendo wa nchi hii, kwani mbali na vitu kuuzwa, dollar zaidi ya 250,000, paundi zaidi ya 200,000 na pesa za kiarabu zaidi ya 180,000 na tshs zaidi 50M zilizokuwa ofisin kwake kwenye shelves na mabegi mahususi zilitoweka kusikojulikana ofisin kwake baada ya kufungwa kwa taasisi na alipoomba kuingia kuchukua vitu vyake binafsi hakuruhusiwa wala mtu yeyote.

Hivyo ni vitu vilivyokuwa ofisini kwake mbali na ofisi mbili za wahasibu zilizokuwa na shelves za pesa.hakika wahusika waliamua kuondoka na hata na nguo jamani! Ningetaja ila basi tu naishia hapo maana inauma sana mm kama miongoni mwa waathirika. Hayo yalibaina siku ya mnada ukiwa umetamatika, hakika ni tukio nisiloweza kulisahauaisha yangu yote hadi pale nitakapopumzishwa naola wangu.

Nawashukuru viongozi wa sasa wa Nssf kwa nia njema ya kuhakikisha jengo na mali ya umma hairabiki kwa kumpata mwekezaji mpya baada ya jengo kukaa zaidi ya miaka 5 bila shughuli yoyote zaidi ya biashara ya dada poa iliyokuwa imeshamiri ktk jengo hilo.

Lakini pia niwashukuru viongozi mahiri wafuko wenye jengo hilo, kwa nia njema na uzalendo mkubwa sana wenye kujali utu,ubinadamu,uzalendo kwa watu wengine hasa wana wana THI walioathirika na janga hilo kwa kutenda ubinadamu kuwalipa malipo yao ya uanachama mbali na kukatisha mikataba yao kimya kimya ambapo walipaswa kutafuta jawabu la nani kavunja mkataba wa kazi yao badala yake wamekuwa waungwana tu.

Ikiwa miaka 10 ya THI imetimia leo na miaka 9 ya gwiji wa moyo Dr.Masau, kutokuwepo ktk uso wa dunia hii,dhamira njema iliyokuwepo ya uwepo wa taasisi ya magonjwa ya moyo nchini, naomba serikali yangu ya sasa na wadau mbalimbali nchini,kuwekeza katika nyanja hiyo mhimu kwa nchi yetu kwa kuwa vifo vingi duniani kwa sasa vinatokana na watu wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo, hivyo serikali na wadau mbalimbali wapanuwe wigo ktk maeneo mengi nchini na hasa kutoa elimu juu ya kuepukana na maradhi hayo kwani matibabu yake ni gharama kubwa sana ambazo mtu wa kawaida ni ngumu sana kujigharamia na kuangalia namna bora ya kupunguza vifo vya watanzania vitokanavyo na maradhi hayo hapa nchini.nawasilisha kwa nia njema.
 
Nashukuru kuona kumbe mpo wenye kumbukukumbu nzuri dhidi ya watu kama Dr Masau.

Mtu ambaye aliwahi kukaa na Mtanzania yeyote mwenye maono dhidi ya taifa lake na kumsikiliza ndiye anaweza kuandika na kumuelezea kiundani mtu huyo, vinginevyo afrika tubaki kuwa black human na nadhani hata roho zetu ni nyeusi as our appearance!.
 
Halafu utawasikia watu humu wakimsifia huyo Rais wa awamu ya Nne mpaka kero.

Utawasikia nyumbu wa ufipa wakimsifia huyu Baba msoga Dakitari wa Mtandao wa dhuluma nchi hii.

Hiyo yoote ilikuwa ni kuiandaa Ile taasisi iliyoshirikiana na Janaba kutunajisi wanyonge wa nchi hii.

Malipo yao yataonekana hapa hapa Duniani siku moja.
Maana Mungu si Juma!
 
Kweli kabisa mkuu,Afrika bado tuna safari ndefu sana maana viongozi wengi wa Afrika wanataka kuabudiwa na kusujudiwa badala ya kuheshimu wataalamu wenye ujuzi wao na hata kuwasadia ili Taifa kusonga mbele zaidi.
 
Umenena kweli kabisa mkuu.kuhusu taasisi ya THI ilizungukwa na mizengo ya kila aina kwa kisingizio cha kushindwa kulipa kodi wakati c kweli ila nyuma yake kulikuwa na madubwana yenye nguvu ya dola na pesa kuhakikisha taasisi haitakuwepo na badala yake kukuza jina la mwenye jina ktk taasisi fulani hivi hapa nchini. Mungu atatuhukumu kwa kila hali kwa wakati sahihi.
 
Halafu utawasikia watu humu wakimsifia huyo Rais wa awamu ya Nne mpaka kero.

Utawasikia nyumbu wa ufipa wakimsifia huyu Baba msoga Dakitari wa Mtandao wa dhuluma nchi hii.

Hiyo yoote ilikuwa ni kuiandaa Ile taasisi iliyoshirikiana na Janaba kutunajisi wanyonge wa nchi hii.

Malipo yao yataonekana hapa hapa Duniani siku moja.
Maana Mungu si Juma!
Mungu ni juma.

Matatizo yetu yatatatuliwa na sisi wenyewe.

Huyo mungu KWA vigano na visasili navyovisikia yupo huko juu anakula bata kwenye maziwa na asali .. hana tofauti na watawala wetu .

Kifupi ni mshe...

Tunahitaji mapinduzi ya kifikra
 
Kweli kabisa mkuu,Afrika bado tuna safari ndefu sana maana viongozi wengi wa Afrika wanataka kuabudiwa na kusujudiwa badala ya kuheshimu wataalamu wenye ujuzi wao na hata kuwasadia ili Taifa kusonga mbele zaidi.
Nawaunga mkono wataalam waliofanikiwa wakiwa nje ya nchi na kukataa kurudi kutumika nchini mwao.

Viongozi wa kiafrika wakienda nje na kuonana na wananchi wao (diaspora) huwashawishi warudi nyumbani kuja kulitumikia taifa na kuwekeza huko, ilihali maneno yao hayashabihiani na matendo pindi wakirudi.

Mfano mdogo ni kama ya late Dr. Masau ni masikitiko makubwa sana unafurahi kurudi home kuwekeza kumbe unafuata kifo, narudia ni heri uonekane siyo mzalendo kuliko kuja kutendwa.
 
Umenena kweli kabisa mkuu, heri kubaki nje ya nchi kuliko kuja kunyanyasika hapa nchini.
 
Tarehe 12 mwezi Aprili mwaka 2012 ukiwa usiku wa manene mithili ya mwizi anayevamia nyumba fulani ili kutimiza hadhima yake, hakika ilikuwa ni siku mbaya iliyoleta machungu makubwa sana kwa waliokuwa wafanyakazi wa Taasisi ya magonjwa moyo (THI) kupoteza ajira zao na vitu vyao binafsi baada ya taasisi hiyo kufungwa na wenye jengo bila hata watumishi hao kupewa taarifa yoyote aidha toka kwa mwajiri au taasisi ya Nssf iliyofunga jengo hilo baada ya mgogoro huo kusemekana ulitolewa maamuzi na mahakama huku mtendaji mkuu alidai jambo hilo bado lilikuwa halijafika mwisho kwa kuwa alikuwa hajapewa notisi husika.

Kufungwa kwa THI hakukuathiri watumishi pekee bali pia iliathiri wagonjwa waliokuwa wamelazwa wodini na baadhi yao wakisubili upasuaji jambo ambalo liliwaathiri vibaya sana hata kisaikolojia.kadhia hiyo ilisababisha wengine kufariki ghafla kwa kuwa ni jambo ambalo hawakutegemea mbali ya kuhamishiwa ktk hospitali mbali mbali ambazo wagonjwa wenyewe hawajaenda huko awali kupata tiba badala yake walitibiwa THI,hivyo kuwapeleka huko tena bila ridhaa yao,hakika hawakutendewa haki kabisa.

Pamoja na wagonjwa kuhamishwa kwa nguvu bila ridhaa yao na hata bila ndugu kufahamishwa chochote,hakika ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa haki ya mgonjwa kutibiwa apendapo.hakika niseme wazi, kama ndugu wa wagonjwa wangechukua hatua ya kushitaki taasisi hiyo tena ikiwa imesababisha baadhi ya vifo vya wagonjwa,ni dhahili haki stahili ingepatikana kwa kuwa utaratibu wa kuwaondoa wagonjwa haukufuata utaratibu mzuri ikiwemo wagonjwa kupewa taarifa za awali juu ya kadhia iliyokuwepo endapo hawakuona busara ya kuja kuongea na watumishi ili pia waondoe vitu vyao binafsi kwani wafanyakazi wengi waliifadhi mali/ vitu vyao ofsini jambo ambalo halikufanyika wala hata siku ya kufungwa hawakuruhusiwa kuingia mtu yeyote,unyama wa ajabu sana waliofanyiwa watumishi na hasa wagonjwa na ndugu zao.

Imekuwa bahati mbaya sana pale mtanzania unapoonewa, kunyanyaswa,kuvunjiwa utu na ubinadamu na mengineyo kushindwa kujaribu kuchukua hatua stahili ikiwemo kudai haki yako,naamini ktk hili la THI kuna watu walitakiwa kufidiwa kwa kutwezwa utu wao ila hawakuchukua hatua,wakimwachia Mungu Baba muweza wa yote awe juu yao.

KUSAMBAA KWA TAARIFA: naamini siku ya kufungwa kwa THI, taarifa zake zilifunikwa zaidi kutokana na msiba wa msanii maarufu nchini marehemu Kanumba kwa kuwa ndiyo siku aliyokuwa akiagwa ktk viwanja vya LEADERS vilivyokuwa karibu sana na taasisi hiyo na kuzikwa ktk makaburi ya kinondoni, hivyo vyombo vyote vya habari zaidi ya 98% vilitekwa na tukio hilo la aina yake ya kuondokewa na gwiji wa nguzo ya filamu nchini. Hata hivyo gazeti la Ijumaa,linalomilikiwa na GLOBAL PUBLISHERS lilifanya kazi ipasavyo, Heko na shukurani ziwaendee kwao kwa kazi nzuri waliyoifanya lakini pia mitandao ya kijamii ikiwemo jamii forum na wengineo kwa kadiri walivyoweza ktk kuhabarisha umma.

NILIYOYASIKIA: siku ya kufungwa kwa taasisi hiyo, nikiwa nimesimama nje ya lango na watumishi wengine,mita chache na wenzangu,nikiwa karibu na kijana mmoja aliyesimamia zoezi la kufungwa na aliyewahi kuhudhuria hospitalini hapo kwa kuwa nduguye kama sikosei alikuwa ni babu yake,akitibiwa maradhi aliyokuwa nayo na nilimtambua kwa sura,nadhani alikuwa ni mtu wa kitengo maalumu kama vijana wasemavyo kutokana na mazungumzo yake. alisikika na nilimsikia akiongea na Aunt yake aliyeko Tabora na simu yake ikitoa sauti yakusikia,nilijisogea karibu zaidi na yafuatayo ni haya;
kijana: Aunt shikamoo! Habari ya huko Tabora.
Aunt: marahaba mwanangu, mnaendeleaje huko?
kijana: huku aunt hatujambo japo c sana.
Aunt: kuna nini?
kijana: Aunt, Dr.Masau anafanyiwa unyama wa ajabu, taasisi yake imefungwa.
Aunt: kwann mnamfanyia hivyo jamani!
Kijana: shangazi hata mimi naumia sana ila basi tu,ukizingatia Dr.Masau alimtibu vizuri mzee wetu. Ikulu hawataki kuiona hiyo taasisi kabisa.nami sina jinsi shangazi maana Dr.Masau alimtibu mzee wetu. Sina cha kufanya,nimajukumu ya kiofisi aunt ila naumia,wakubwa hawataki kuiona THI.
Aunt: jamani! Jamani!
Kijana: ndio hivyo aunt.baadaye.

Mwisho wa yale niliyoyasikia ktk mazungumzo ya watu hao.

Mengine niliyoyasikia ni tajiri mmoja mwenye hosipitali yake maeneo ya fire japo kwa sasa marehemu, akiwa na Prado silver,nikiwa miongoni mwa watumishi kama watatu,akisema tusiwe na wasiwasi kwa watumishi wote wa THI atawajiri na Appolo hospital ya moyo itahamia hapo.

Baada ya kuona kazi iliyoleta na kushuhudia wagonjwa waliokuwa wakihamishwa THI, jengo likiwa na maandishi, " jengo hili limeshatapata mwekezaji mpya,ni mali ya Nssf" kisha tajiri huyo na mdau mkubwa wa kada ya afya baada ya kuona vile aliondoka akijua kazi yake imekwisha.

Baada ya kuona trela ilivyokwenda,hakika nilisikitika,niliuzunika,niliumia sana,kumbe mbali na mgogo wa kudaiana juu ya pande hizo mbili,kumbe nyuma ya pazia kulikuwa na wenye nchi,wenye mipango, wenye nguvu za ajabu kuhakikisha THI haitakuwepo tena kwa kivuli cha kudaiwa kodi ya pango huku wao michoro iliyokusudiwa ilikosewa na kuamuliwa na wafadhili wakuu wa THI warudie ili kuweza kulipa kodia hiyo,jambo ambalo wahusika hawakukubali kwa kuwa mwana THI hakutoa chochote, pengine hakutanguliza ahsante kwa wale wachache wazee wa percent,hawakuwa wengi,bali wachache tu na baadhi walidiriki kuomba hata hongo ya kufikia deni la michango ya watumishi ili wafukie makaburi,jamaa akakataa,mtu nne zikiwa zimefika ofisin kwa Dr.akawatolea nje,wakaondoka wanyonge sana,bati nzuri niliwaona baada ya kuitwa wakiondoka. Dr.apumzike kwa amani huko aliko na asamehewe yake madhaifu kama tulivyo binadamu wengine.

KUSUDIO LA KUKATA RUFAA: ni ukweli usiopingika na mtu anaweza kuhoji kuwa kama alionewa au THI ilionewa,kwann hakukata rufaa? Baada ya kufungwa kwa taasisi, mkurugenzi alijaribu kuwasiliana na mtetezi wake, majibu aliyopewa hayakuwa ya utetezi,ya mtu na mteja wake kabisa! Hata hivyo Dr.masau hakukata tamaa, alimuona jaji wa mahakama ya rufaa nyumbani kwake personally kwa ushauri, alipata mawaidha mazuri, aliwaona mawakili wengine akiwemo mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Mpoki na wengineo, na wote hao walishauri akate rufaa,kwani moja ya kipengele cha mkataba ilikuwa kumaliza meza ya mazungumzo endapo mgogoro umetokea,na mengineyo ambayo waliona THI inastahili, je ilikuwaje? Masikini THI haikuwa na pesa tena hata kusonga mbele, ilibaki mithili ya yatima tu.

Wakati THI ikihaha huku na kule, ajabu, mtetezi wake aliyeaminiwa na Dr.akaibuka na kumshawishi Dr.Masau kutokata rufaa eti wenye jengo wamesema watampa vitu vyake vyote na wao wanachotaka ni jengo lao tu,masikini Dr.,mkurugenzi wangu,kumbe hakujua alikuwa anatafutiwa usemi wa from hero to zero! Dr.kwa kuamini tena,eti mtu wa nyumbani,kabila fulani! Akaacha kukata rufaa, akatafuta jengo akapata jengo karibu na kituo cha ubalozi wa Ufaransa,gharama kwa mwezi 60million, akajiuliza kama ataweza,akasema ngoja asubili vitu, kumbe mtego wa siku 14 kama sikosei za kukata rufaa mahakamani angeliona yafaa, kumbe mtego bhana! Akashawishiwa na mtetezi wake,akaingia kumi na nane,siku zikayoyoma,zikaisha,mnada ukatangazwa na vitu vikauzwa,akahamaki mbali na yeye kununua vyakuanzia ktk hatua nyingine huko mbeleni,bahati mbaya lengo halikutimia ipasavyo, akaondoka gwiji wa moyo Tanzania, mratibu wa magonjwa ya moyo Africa na makamu wa Rais wa shirikisho la moyo duniani kwa nyakati mbili tofauti,akiicha ofisi ndogo ya THI huko hospitali ya moyo Texas Marekani ambao walikuwa wadau wakubwa wa THI kwa asilimia kubwa kwa kutoa wataalumu bobezi wa moyo wakisaidiana na ujerumani na vifaa tiba kwa nyakati zote za uwepo wa THI.

Mungu ampumzishe Dr.masau,Mungu awakumbuke wana THI popote walipo kwa uzalendo wao kwa Taifa.je nikisema kulikuwa na harufu ya rushwa kwa upande fulani nitakosea? Sina maana kuna mtu alipokea rushwa toka mahala Lah! Mungu pekee ndio mwenye hukumu ya kweli na mwenye kuona mambo yote yaliyoko gizani na kufunuliwa nuruni,huku duniani mapito yenye hukumu za michongo ni mingi japo zipo hukumu nyingi zenye haki na ieleweke hivyo,nisinukuliwe vibaya ndugu zangu.

Matibabu ya bure: kufungwa kwa THI kuliacha simanzi na huzuni mkubwa kwa baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakitibiwa THI bila malipo yoyote kutokana na Uduni na kukoswa pesa ya kujitibu ndani ya familia zao,hivyo taasisi ilibeba dhamana hiyo,kwani kauli mbiu ya Dr.Masau ilichagizwa na neno, " TOKA MOYONI KWA AJILI YA MOYO" hivyo kwake utu na ubinadamu ulikuwa nguzo muhimu sana badala ya fedha na masilahi yake.
Maswali niliyojiuliza;

1. Je maamuzi ya kuiondoa na kuifuta THI yalikuwa sahihi kweli?

2.Ikulu ni taasisi pana ndiyo,ikiwa ni serikali ya awamu ya nne, je ni mkubwa gani hakutaka kuiona THI ikiwepo? Ikiwahudumia watanzania hasa wa hali ya chini? Japo na wageni nje ya nchi walitibiwa.nadhani hapa mhusika huko aliko kama yu hai basi anakijua vema badala ya mm kubashiri tu.

3. Je kwann yule mhindi, mwenye hospitali maeneo ya fire japo sasa ni marehemu,Mungu amurehemu huko aliko,kwann hakuchukua tena jengo kama alivyoahidi kwa wana THI? Badala yake alijengewa jengo na taasisi fulani ya umma kwa makubaliano fulani fulani hivi,hizi ni tetesi zilizovuma kipindi cha nyuma na hata mtandaoni kama sikosei.tetesi zingine kushindwa kuchukua jengo ni gharama kubwa alizoambiwa,mhindi akaachana na mchongo huo.

4. Je Dr.kutokuwa upande wa wapiga percent ndio gharama ya kuipoteza THI?

5. Je haikuitajika taasisi nyingine mbadala hapa nchini ya moyo kama zilivyo taasisi au hospitali zingine?

6. Je vitu vilivyouzwa,viliwezesha wadai kujilipa pesa yao? Jibu ni hapana, taasisi ilikuwa na thamani ya zaidi ya 10 billion kwa mwaka 2010 lakini mauzo ya vitu vile hayakufikia hata 500M kwa kuwa ktk minada takribani yote nilishuhudia.

7. Je mtetezi wa THI alikuwa na maana gani kumshawishi na kumlaghai De.Masau kuachana na wazo la kukata rufaa?

8. Je lugha za kejeli na maneno yasiyo na mtu na mteja wake japo sijayaimisha hapa, je yalikuwa yakiungwana? Yalikuwa yanaashiria nn? Je alikuwa ni mtu sahihi ktk uadilifu wa taaluma yake? Mungu na atuhukumu kadiri itakavyofaa kwa matendo yetu

9.maswali ni mengi mno; nimalize kwa kusema,kilio kwa wana THI kilikuwa kikubwa sana na hasa kwa DR.mzalendo wa nchi hii, kwani mbali na vitu kuuzwa, dollar zaidi ya 250,000, paundi zaidi ya 200,000 na pesa za kiarabu zaidi ya 180,000 na tshs zaidi 50M zilizokuwa ofisin kwake kwenye shelves na mabegi mahususi zilitoweka kusikojulikana ofisin kwake baada ya kufungwa kwa taasisi na alipoomba kuingia kuchukua vitu vyake binafsi hakuruhusiwa wala mtu yeyote.

Hivyo ni vitu vilivyokuwa ofisini kwake mbali na ofisi mbili za wahasibu zilizokuwa na shelves za pesa.hakika wahusika waliamua kuondoka na hata na nguo jamani! Ningetaja ila basi tu naishia hapo maana inauma sana mm kama miongoni mwa waathirika. Hayo yalibaina siku ya mnada ukiwa umetamatika, hakika ni tukio nisiloweza kulisahauaisha yangu yote hadi pale nitakapopumzishwa naola wangu.

Nawashukuru viongozi wa sasa wa Nssf kwa nia njema ya kuhakikisha jengo na mali ya umma hairabiki kwa kumpata mwekezaji mpya baada ya jengo kukaa zaidi ya miaka 5 bila shughuli yoyote zaidi ya biashara ya dada poa iliyokuwa imeshamiri ktk jengo hilo.

Lakini pia niwashukuru viongozi mahiri wafuko wenye jengo hilo, kwa nia njema na uzalendo mkubwa sana wenye kujali utu,ubinadamu,uzalendo kwa watu wengine hasa wana wana THI walioathirika na janga hilo kwa kutenda ubinadamu kuwalipa malipo yao ya uanachama mbali na kukatisha mikataba yao kimya kimya ambapo walipaswa kutafuta jawabu la nani kavunja mkataba wa kazi yao badala yake wamekuwa waungwana tu.

Ikiwa miaka 10 ya THI imetimia leo na miaka 9 ya gwiji wa moyo Dr.Masau, kutokuwepo ktk uso wa dunia hii,dhamira njema iliyokuwepo ya uwepo wa taasisi ya magonjwa ya moyo nchini, naomba serikali yangu ya sasa na wadau mbalimbali nchini,kuwekeza katika nyanja hiyo mhimu kwa nchi yetu kwa kuwa vifo vingi duniani kwa sasa vinatokana na watu wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo, hivyo serikali na wadau mbalimbali wapanuwe wigo ktk maeneo mengi nchini na hasa kutoa elimu juu ya kuepukana na maradhi hayo kwani matibabu yake ni gharama kubwa sana ambazo mtu wa kawaida ni ngumu sana kujigharamia na kuangalia namna bora ya kupunguza vifo vya watanzania vitokanavyo na maradhi hayo hapa nchini.nawasilisha kwa nia njema.
Nakushukuru sana kwa kuandika taarifa hii. Sina mengi ya kuandika ila kwa huzuni nasema MUNGU MWENYE HAKI atatoa hukumu yake.
 
Back
Top Bottom