Nauli mpya za mabasi ya mkoani hizi hapa!

Nauli mpya za mabasi ya mkoani hizi hapa!

daaah ndo wana sema gharama za uendeshaji zimepanda?? sasa na hao FASTJET wao gharama hazipandi?? Au ndo ule msemo uliozoeleka kwamba viongozi wetu wanafikiria kwa kutumia tumbo?? T 2015 CDM
 
Janga jingine hili. Mwisho wa siku ni mlalahoi ndiye atakaye umizwa na mabadiliko haya.Bei za bidhaa zitapanda huko vijijini: mafuta ya taa, chumvi, kiberiti, sukari...kwa kutaja vichache

Ni kweli mkuu, hili litapelekea hata bei za kununua hayo mabasi kupanda zaidi!
 
lol, hapo kwenye red mbona unatutisha!!! Na migomba ilivyoharibika ikiwa na marufuku za uvuvi ziwani si ndo tumekwisha!!?

By the way, ukiangalia jinsi hawa SUMATRA/TABOA (sijui na mambo gani mengine) wanavyopanga nauli ndio utajua kuwa hawana lolote la maana wanalofikiria. Hebu angalia mfumo wote wa nauli unaelekeza 'DAR - .....(upcountry)'. Yaani ile theory aliyoacha mkoloni mpaka leo hawawazi upya, kwa nini hawataji mfano Bukoba - Musoma, Tabora - Kigoma, Uvinza - Sumbawanga nk. Yaani wenyewe wanaamini nchi yote inasafiri kuja na kutoka Dar. Kwa kifupi hawana jipya na ni bora wangeacha nguvu ya soko ifanye kazi yake kama Fasjet wanavyoofa 32k

Mkuu umenena, sio watu wanakuwa kama makasuku, matokeo yake ni nauli kutoka wilaya moja hadi nyingine ndani ya mkoa mmoja inakuwa kubwa kuliko ya Songea hasi Dar!!!
 
Back
Top Bottom