Godlisten Masawe
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 738
- 283
Tunazungumzia nauli kupanda kutoka shillingi mia hadi mia mbili, na katika my original post, nimeelezea kwa uwezo wangu wote binafsi naona tatizo lipo wapi. Vinginevyo hakuna anaekataa kwamba wananchi wana hali mbaya, lakini wapo wanaopinga (mimi nikiwa mmoja wapo) vitendo vya baadhi ya viongozi kutumia hali hizo mbaya za wananchi, kisiasa.
Mkuu maelezo yako vile vile hayajibu hoja.. Sema spinning iko wapi na ukweli ni upi maana katoa mifano wewe toa yako tuitazame na sio kufanya yale yale unayoyapinga kutoka kwa mchambuzi..Unnecessarily...kamanda mchambuzi huwa nakuheshimu sana. Nakumbuka ile article yako juu ya Baba wa Taifa Nyerere! Leo umechemka. Naona umeinga kwenye mradi wa spinning na propaganda wa Magufuli, kwa kujua ama kutojua. Pole! Juzi nilimsikia mtangazaji mmoja wa Clouds FM (nililazimika kusikiliza coz nilikuwa ndani ya gari ya mtu), akiweka sauti ya Pombe Magufuli, hasa pale aliposema ati anamheshimu sana Mdee kwa sababu ana-concetrate na jimbo lake (hajui kuwa Mdee yuko safarini), akasema ati Mnyika ameshindwa kushughulikia mambo kama ya mabweni UDSM na nauli ya Ubungo Terminal (pia hajui jitihada za Mnyika ndizo zilisababisha nauli isipande kwenda shilingi 300 kama ilivyokuwa imepangwa na sasa hivi kutokana na juhudi hizo, jiji linapitia sheria ndogo ndogo juu ya suala la Ubungo Terminal kucheki utaratibu huo).
Mtangazaji yule (alikuwa Redio One, somebody Ayo sijui), kama ulivyofanya wewe hapa, akamalizia kwa kusema "hiyo ni sauti juu ya Waziri Magufuli akijibu hoja za wabunge wa Dar es Salaam juu msimamo wao wa kupinga ongezeko la nauli ya shilingi 100, akiwemo Mbunge wa Ubungo, John Mnyika." Come one what a crap!
The same to u brother. Hoja yako hii ya kipuuzi kabisa isiyolingana na uwezo wako niliozoea kuuona hapa mara kwa mara! Nimeshindwa kuendelea kusoma mpaka mwisho baada ya kuona kuwa umeingia kwa kiasi kikubwa katika spinning ya Kundi la Pombe Magufuli, ambalo limeamua kuweka msisitizo kuwa kinachopingwa na wote wenye akili timamu eti ni ONGEZEKO LA SH. 100! To hell, hii si hoja kwa watu wenye akili walioona crap ya Magufuli bro. Kuna issues kadhaa za msingi, suala si sh. 100, hata kidogo, ukijadili hivyo ure missin the point at large bro! Nitakueleza baadae kidogo!
Qualify some several conclusions zako, mara unasema serikali inaweka pesa nyingi sana katika kuendesha kivuko hicho!!!!! He kiasi gani hicho bro hebu kiseme! Je kinatosha au hakitoshi kujenga daraja hapo mahali ili tuondokane na bugudha ya watu kulipia mahali ambapo haikusathili kama serikali ingetimiza tu wajibu wake wa kutoa huduma kwa watu kwa kujenga daraja! Kuna vitu kadhaa katika hoja yako nataka nikueleze ili ufikirie upya attack zako kwa Mnyika na wabunge wenzake. Ntakueleza...punde
Mkuu usizungumzie badiliko la nauli ya binadamu tu, hebu jaribu kuzungumzia nauli ya kuvusha GutaIngekuwa ni wabunge wa CCM peke yake, pengine nisinge hoji kwani tumewazoea wabunge wengi wa CCM (sio wote), kuja na matamshi ya ajabu ajabu. Mnyika ni mtu makini sana kutumbukia katika sakata lillojaa mantiki kuliko siasa, na hilo ndilo limenigusa zaidi.
Heshima kwako Mchambuzi;
Una mawazo mazuri sana kamanda.
Pamoja na wabunge kutumia matatizo (hali mbaya) ya wananchi kujinufaisha kisiasa; Binafsi nawaunga mkono tamko la wabunge wa dsm kwa sababu moja tu ifuatayo;
- Taifa letu limeazimisha miaka hamsini ya uhuru, ilitakiwa pale tuwe na daraja na wananchi tuvuke bure (bila kutoa hata tshs. 5), Sitaki kuangalia wala kufahamu mapato na gharama za uendeshaji wa kivuko.
Hawa viongozi wetu wabunge hawakulizungumzia hilo sasa unataka Mchambuzi ndio alizungumzie?.. wao wanashindwa nini kusema wazi kwamba hawakukubaliana na sehemu hiii maana kilichopingwa na wananchi ni nauli toka Tsh 100 kwenda 200 na wabunge wamekurupuka kuunga mkono bila kueleza sehemu wanazozipinga wao. Wale wote waliokuwepo ktk mkutano wakizomea hawakuwa wafanyabiashara bali wananchi wapanda kivuko hicho. Na huyo kijana aloogelea toka magogoni hadi kigamboni mbona hakubeba pakacha la ndizi?.Mkuu usizungumzie badiliko la nauli ya binadamu tu, hebu jaribu kuzungumzia nauli ya kuvusha Guta
Si kweli kwamba mtu anayetoka kigamboni kuja upande wa pili wa Dar kwa kutumia pantoni analipa shilingi 200 tu. Tukumbuke kwamba wakazi wa kigamboni wanatumia nauli kutoka majumbani mwao ili kufika eneo la feri na wanatumia tena shilingi 200 kuvuka. Hivyo ongezeko hilo la 100 sio tu limeongeza nauli ya msafiri wa kigamboni kuwa 200 bali tunatakiwa kujumlisha pia nauli wanazotumia kutoka majumbani mwao kufika hapo feri kwa ajili ya kuvuka. Hivyo basi kuna ambao walikua wanatumia shilingi 300 kwa siku sasa watalipa 400 na ambao walikuwa wanatumia 400 sasa wanalipa 500. Tusiupotoshe umma kwamba nauli imeongeza kutoka 100 kwenda 200 bali tuangalie nauli kutoka kule wakazi hawa wa kigamboni wanapoishi mpaka kuvuka kwa kutumia hilo pantoni.
Hawa viongozi wetu wabunge hawakulizungumzia hilo sasa unataka Mchambuzi ndio alizungumzie?.. wao wanashindwa nini kusema wazi kwamba hawakukubaliana na sehemu hiii maana kilichopingwa na wananchi ni nauli toka Tsh 100 kwenda 200 na wabunge wamekurupuka kuunga mkono bila kueleza sehemu wanazozipinga wao. Wale wote waliokuwepo ktk mkutano wakizomea hawakuwa wafanyabiashara bali wananchi wapanda kivuko hicho. Na huyo kijana aloogelea toka magogoni hadi kigamboni mbona hakubeba pakacha la ndizi?.
Mtoa mada umewasilisha hoja kwa mapana na marefu yake, ila kuna takwimu hapa hazijakaa sawa: -
Umesema gharama kwa sasa ni 98% ya (9,000,000) mapato kwa siku kwa nauli ya Tsh 100. Na ukasema nauli ikiwa Tsh 200 salio litakuwa ni sh.333, 332 (laki tatu), badala ya Sh. 166,666? Si kweli. Nauli ikiwa Tsh. 200, Salio litakuwa ni Tsh. 166,666 ongeza 9,000,000 (itayotokana na ongezeko la tsh 100 ktk nauli mpya) mana gharama zitakuwa covered na ile 98% ya 9,000,000 ya mwanzo wakat nauli ni Tsh 100 na sio kuwa nauli ikiongezeka kuwa 200 gharama nazo ztaongezeka kuwa 98% ya (9,000,000+9,000,000).
Pia ungetueleza gharama za uendeshaji kwa kina, Makusanyo kutoka kwenye nauli na ruzuku/subsidy ya serikali kwa siku/mwezi kabla ya kusema kwamba nani yupo sahihi au yupo wrong. Na imani kupitia kivuko hicho serikali inatoa huduma na sio kuwa inafanyabiashara, hivyo hatutegemei serikali kuweka kiwango ambacho kitamuumiza mwananchi as if serikali inafanya biashara. Kama unasema katika uendeshaji wa kivuko hicho zaidi ya nauli wanazotozwa wananchi kuna ruzuku ya serikali. Nina imani kubwa either hiyo ruzuku ni ndogo sana au haipo kbs au kama ipo basi kuna ufisadi mkubwa unaofanyika. Na labda pengine ndio msingi wa kelele za Wabunge
Mana kwa harakaharaka nimegawanya hicho kiasi ulichokitaja cha gharama za uendeshaji (Tsh8.8m) kwa tsh 2000 ya diesel kwa lita. Nimepata jumla ya liter 4400 za diesel zinatumika kwa siku. Ila kwa kuwa kuna mahitaji mengine ktk kuendesha panton hizo, assume lita 500 i.e 1,000,000/= kwa siku itacover hayo mahitaj mengine km grease, mishahara n.k. Bado liter 3900 kwa siku ni nyingi mno kwa matumizi ya panton mbili labda kama kuna mengine ila siamin kwamba gharama za uendeshaji wa panton hizo mbili kwa siku ni tsh Tsh 8.8m.
Umetoa hoja za msingi na zemye mantiki;no comment kwa sasa,namsubiri Mnyika aje atoe utetezi wake hapa;halafu nitachanganya na zangu!!!
Hakuna hoja huwezi kumfananisha mkaazi wa Kigamboni na hao wanao lipa nauli ya mia tatu kutoka Posta mpaka Feri. Au huoni tofauti?