Upandishaji holela wa nauli

National Interest

New Member
Feb 28, 2024
1
1
Kumekuwa na upandishaji holela wa nauli hususani kwa Karatu-Mbulu na Mbulu - Murray.

Mfano awali nauli kutoka Mbulu- Karatu ilikuwa sh.5000 na Sasa ni sh.7000 ongezeko la 40% ambalo limehusishwa na ongezeko la Bei ya mafuta ya chini ya 10% . Sasa inakuwaje mafuta yanaongezeka kwa 10% halafu nauli iongezeke kwa asilimia 40% karibu mara nne yake na imeshuhudiwa mara nyingi tu hata endapo Bei ya mafuta imeshuka nauli inabaki palepale so it remain unjustified.

Aidha nauli kutoka Mbulu-Murray ilikuwa 2000 na ikapandishwa na Sasa ni 4000 ongezeko la 200% ikihusishwa na ubovu wa barabara na mafuta kupanda bei chini ya 10%.

Mpaka muda wa kuposti, nauli Hizi zimebaki palepale pamoja na kwamba serikali imeshakarabati barabara kwa kutumia fedha za mfuko wa Road Fund na pia makali ya Bei za juu za bidhaa za mafuta imepungua naomba mamlaka husika ikafanye mapitio ya nauli hizi na ningeshauri iingilie kati haraka kukawe na ongezeko la 20% au chini (less than or equal to 20%) ya nauli hizi Ili kupunguza gharama za Maisha kwa wananchi wa Eneo lile.

Aidha kwa upande wa mizigo nauli zimeongezeka kwa asilimia sawasawa.
 
tumeipenda wenyewe, chaguo letu milele. acha waisome namba
 
Back
Top Bottom