Nauli Arusha - Dar yashuka mpaka shilingi 13,000-15,000

bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,015
4,982
WanaJF wenzangu naona huu ukosefu wa abiria umesababisha nauli kushuka kwa kiwango kikubwa Sana.

Sasa hivi ukipanda basi mkizidi sana mpo ishirini.Nipo hapa stand kubwa ya mabasi Arusha naongea na wapiga debe pamoja na mawakala wa mabasi wanachoniambia kinasikitisha kwa kweli.

Wanadai sasa hivi wanaendesha kampuni kwa hasara kwani abiria hamna na abiria mmoja mmoja anaekuja analalamika Hana hela ndo mana ikafika hatua tunampandisha kwenye basi hadi kwa tsh 13000 au 15000.

Na kwa Sasa yale mabasi ya luxury ya asubuhi kabisa Yanabeba abiria hadi kwa elfu 20000.

Jamani sasa hivi mtu akitaka kusafiri toka nyumbani na hela yako yoyote tu uliokuwa nayo Basi utapata.
 
WP_20170331_003.jpg
hali ilivo asubuhi hii
 
TAIFA la watu wasio nafuraha duniani.kila kitu hakiendi SAWA,na tuliowapa jukumu la kuongoza wanaona SAWA.
 
Nauli ikipanda mnalialia
ikishuka pia mlie!!
Wacheni unafiki
ujue walio kuwa wakisafiri mara kwa mara hawakuwa na sababu za maana za kusafiri
Mkuu nauli kushuka wanaolia sio abiria Bali Ni hao mawakala na wapiga debe pamoja na wamiliki kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko kipato
kwa upande WA pili wapiga debe na mawakala wanalia kutokana na kukosa posho
 
Anaye shusha nani?
 
mwezi wa 3-4-5 hakunaga wasafir
mimi naendaga masasi gari halijajaa
mnarudi hata watu 20
mvua hizi nani asafiri
 
Mkuu nauli kushuka wanaolia sio abiria Bali Ni hao mawakala na wapiga debe pamoja na wamiliki kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa kuliko kipato
kwa upande WA pili wapiga debe na mawakala wanalia kutokana na kukosa posho
Wapiga debe ndio wanaongoza kwa kupandisha nauli za mabasi, hawana tofauti na madalali wa nyumba.

Kiuhalisia hatutakiwi kuwa na wapiga debe kwenye stands za mabasi, ni basi tu nchi hii ni masikini, watu masikini, ajira hamna, hatutaki kulima na kurudi vijijini, hivyo ni ngumu kukwepa wapiga debe.
 
Walio kijijini kwa Sasa wanataman kuhamia mjini, wakulima Nao wananyonywa wanalima mazao lakini yananunuliwa kwa Bei ya hasara sana, hawapati kitu na wakati mwingine swala la Bara bara( miundombinu) ni mibovu sana
 
Back
Top Bottom