National service with a difference; Compulsory National Service is coming back

mimi sijui kama itasaidia kitu maana mtazamo ni tofauti na serikali haiko serious hata siku moja na swala hili wanaimba tu kila mwaka utekelezaji zero. Na budget ya mwakani mtalisikia.
 
tatizo JKT ikurdui inatakiwa irudi kwa Idea Ile ile lakini strategy mpya. Wakiendela na strategy zile zile za zami itakuwa ni mzigo tu kwa taifa na utaishia kutengeneza wanajeshi wasio na kazi mtaani.

Ndo hapo sasa tutakuwa tunakaribisha mapinduzi ya kiukweli ukweli. teh teh teh.

Zaidi ya ukakamavu na uzalendo JK ya Kizazi hiki inatakiwa kuongeza mambo ya ufanisi , Tija na Uzalishaji na speciliasation

  • JKT na hata JWTZ wanatakiwa kuwa na mshamba makubwa ya mifano wilayani na mikoni JKT inataiwa kuwa na vituo vya kuwafunza watu ufugaji nyuki, kupanda miti nk
  • JKT inatakiwa kuanzisha vituo na ufundisha na kuendeleza vipaji vya michezo kama kuogelea,( Dar auMwanza) kukimbia,( Arusha) Kuendesha baiskeli( Mwanza), etc. Tena kwa hivi vipaji hakunahajaya kusbiri mtu kakomaa mifupa. Kila mwezi wa sita wakati shule za primary na sekondari zimefungwa wanweza kuwafundisha watto kuogelea etc
Mambo yale yale aliyoacha Nyerere na kina kawawa yalihitaji creative na innovative mindi ili yawe endelevu. Saaabu wengi wana mawazo magando waliona yamepitwa na wakati. ....

Nawasilisha
Mtazamaji,
Ungeongezea vile vile wawe na kitengo cha kufundisha skills, hasa kazi za mikono kama vile uselemara, kilimo cha kisasa, ili vijana waweze kujiajiri au kuanzisha miradi yao wanapomaliza muda jeshini.
 
Kwa namna mambo yalivyo shaghalabaghala wasi wasi wangu ni namna hili litakavyofanikiwa...ni jambo zuri so far kwa kua ndiyo chimbuko la uzalendo na moyo wa utayari linapokuja suala la manufaa ya wengi!
 
Mtazamaji,
Ungeongezea vile vile wawe na kitengo cha kufundisha skills, hasa kazi za mikono kama vile uselemara, kilimo cha kisasa, ili vijana waweze kujiajiri au kuanzisha miradi yao wanapomaliza muda jeshini.

jasusi uko sahii kabisa mfano angalia asali inayopatikana tanzania . Ujuzi tunategemea na inavyozalishwa ni wa kijadi zaidi. Ni wanfunzi wangapi wanamaliza sekondari mkoa wa taboa wanajua kuvuna asali. ????!!!!!

nadhani kulingana na jiografia ya Tanzania JK itazame kulingan na kanda vipaubele gani vipewe msisitizo

eg eg
kama kuna kituo cha JKT arusha msisitizo uwe ni mufugo, wanyama pori na utalii.
Kama kuna kituo cha JK RUKWA AU RUVUMA na iringa msisitizo uwe ni kilimo

Ndio maana nimettaja speciliasation. yale yale mawazo ya kina nyerere na kawawa yalitakiwa kuboreshwa ili JKT iwe na tija na faida. Ukitaka JKT ya Kigoma ifocus mambo yale yale ya JKT ya mwanza ,arusha na dar hapo itakuwa kosa. ofcourse kuna mambo yanatakiwa kuwa compulsory lakini specillsation ni muhimukulingana na eneona rasilimali zilizopo eneo fulani.

hayo ndio mawazo yangu ya JKT ya kizazi cha sasa.

Na sio JKT ilenge watu walimaliza chuo tu amabo wana uwezo wa kupata kazi za kushika kalamu. JKT inatakiwa ilenge kuwapa skilss watu walishindwa kuendelea na elimu ya sekondari au walioshia form IV.

Mfano nimesikia ziito anapendekeza wabunge wote abao hakwenda JK waende JKT. Ni vizur lakini kwa mpango wa muda mefu haina maana sana . Kuna watu kwa sasa amabo JKT inaweza uwasaidia sana kuliko watu walioshazoea kula kwa kalamu

Ni wao zuri lakini hizo pesa zilizotengwa kwa ajili yaJKT ni kichekesho...... Ni just usanii . yaani ni ndogo mnooo
 
Kama ni mwaka ujao wa fedha kwanini anaongelea mwaka huu wa fedha? I mean mwaka huu wa fedha ni kitu gani kinafanyika, hatutaki JKT mwaka ujao wao fedha kama nikuanza ianze leo la sivyo tuta amini wanatengeneza ma-camps ya kuibia kura 2015.
 
Naomba swala hili uliangalie from another angle.Yes watakuwa nguvu kazi, watapata ajira nk. nk.,lakini kumbuka vijana hawa sio wale wa 1973 na kurudi nyuma.Pia kumbuka kwamba sio wote watapata ajira.Infact wengi watakosa.Kama hujui nakupasha kwamba vijana hawa wamekuwa "BRED FOR A SPECIAL PURPOSE".Sasa, wakitoka huko na mbinu za kijeshi,halafu wakakosa ajira, tutapona kweli.To me, we will have dug our own grave, ingawa hata sasa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka.
Gazeti la leo,14 july 2009,linaripoti kwamba,Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,vijiji na Jiji la Tanga wanataka JKT irejeshwe kama ilivyokuwa zamani,yaani,nguvu kazi,Serikali iwakamate vijana Mijini,kushoto na kulia na kuwapeleka JKT,ili wakafanye kazi za ujenzi wa Taifa. Na hili ni jambo ambalo walikuwa wanalijadili na TAYODEA,Taasisi ya vijana Tanga,kwamba vijana wachukuliwe kutoka vijiweni wapelekwe JKT.

Wanasema wanataka Wabunge waishauri Serikali. Mimi nadhani ni jambo ambalo linaweza kufikiriwa,kuwa na militia,kuwapeleka vijana JKT, kwa sababu Mgambo na JKT walisaidia sana katika vita dhidi ya Iddi Amin. Na pia Waamerika wanawaruhusu wananchi wao kuwa na silaha kama jambo ambalo linaweza kuifanya nchi yao iwe salama kutokana na mashambulizi kutoka nje.

Kwa ajili ya Usalama wa nchi yetu,hili ni jambo ambalo tunapaswa kulifikiria. Siyo kuwaweka gerezani wazururaji ,jambo ambalo lilifanywa miaka kadhaa iliyopita na kuwafanya NCCR Mageuzi,akina Mabere Marando kulalamika sana,lakini kujaribu kuliondoa tatizo la ajira.
 
..kituko kingine ni kwamba Hussein Mwinyi alikimbia JKT wakati wake lilipokuwa kwa mujibu wa sheria.

..leo ana ujasiri wa kurudisha JKT ili watoto wa wenzake wakasote huko.

..binafsi nimekwenda JKT lakini napinga huu mpango wa kulianzisha upya jeshi hilo.

..kama tumeshindwa kuwafundisha vijana wetu kuipenda nchi yao kwa miaka 14 wanapokuwa mashuleni, tusitegemee tutafanikiwa kwa mwaka 1 au miezi 6 ya JKT.
 
hebu mpeleke kwanza kijana wako mkuu.
 
Uzalendo ni moyo wa mtu. Mbona mafisadi wengi wa leo wamepita jeshi na hiyo JKT lakini bado hawana lolote ni wezi watupu.ILA WASIWASI WANGU KIZAZI HIKI KIKIPITA JESHI, WAKIWA CHUONI WAKAANDAMANA KUTETEA HAKI ZAO SERIKALI HAIONI ITALETA MAPINDUZI YATAKAYOAMBATANA NA MAPAMBANO YA KUIKOMBOA NCHI DHIDI YA VIBAKA NA WEZI WA RASILIMALI.
 
..kituko kingine ni kwamba Hussein Mwinyi alikimbia JKT wakati wake lilipokuwa kwa mujibu wa sheria.

..leo ana ujasiri wa kurudisha JKT ili watoto wa wenzake wakasote huko.

..binafsi nimekwenda JKT lakini napinga huu mpango wa kulianzisha upya jeshi hilo.

..kama tumeshindwa kuwafundisha vijana wetu kuipenda nchi yao kwa miaka 14 wanapokuwa mashuleni, tusitegemee tutafanikiwa kwa mwaka 1 au miezi 6 ya JKT.
Kina Dick Cheney wako wengi.
 
Back
Top Bottom