National service with a difference; Compulsory National Service is coming back | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

National service with a difference; Compulsory National Service is coming back

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Andrew Nyerere, Jul 14, 2009.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Gazeti la leo,14 july 2009,linaripoti kwamba,Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri,vijiji na Jiji la Tanga wanataka JKT irejeshwe kama ilivyokuwa zamani,yaani,nguvu kazi,Serikali iwakamate vijana Mijini,kushoto na kulia na kuwapeleka JKT,ili wakafanye kazi za ujenzi wa Taifa. Na hili ni jambo ambalo walikuwa wanalijadili na TAYODEA,Taasisi ya vijana Tanga,kwamba vijana wachukuliwe kutoka vijiweni wapelekwe JKT.

  Wanasema wanataka Wabunge waishauri Serikali. Mimi nadhani ni jambo ambalo linaweza kufikiriwa,kuwa na militia,kuwapeleka vijana JKT, kwa sababu Mgambo na JKT walisaidia sana katika vita dhidi ya Iddi Amin. Na pia Waamerika wanawaruhusu wananchi wao kuwa na silaha kama jambo ambalo linaweza kuifanya nchi yao iwe salama kutokana na mashambulizi kutoka nje.

  Kwa ajili ya Usalama wa nchi yetu,hili ni jambo ambalo tunapaswa kulifikiria. Siyo kuwaweka gerezani wazururaji ,jambo ambalo lilifanywa miaka kadhaa iliyopita na kuwafanya NCCR Mageuzi,akina Mabere Marando kulalamika sana,lakini kujaribu kuliondoa tatizo la ajira.
   
 2. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huko itakuwa wame enda kupata ajira ama kupata mafunzo na kurudi kijiweni ? kasi na ufundi katika kushika bunduki vitaenea Tanzania na ujambazi utakuwa wa hali ya juu badaye .Huniamini kaa tulia uone
   
 3. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Lazima wapate mafunzo kama ya Veta,yaani ,siyo kuwatupa kule,lakini kufanya jambo kuwasaidia vijana.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,764
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  ..nimepitia JKT na sikuona faida yake.

  ..ilikuwa ni sawa na mwaka mzima wa kukaa kijiweni tu.

  ..binafsi ningependekeza iwe ni suala la HIARI ya mhusika kujiunga na JKT.

  ..anayeona atafadika ajiunge na JKT, asiyefahamu manufaa yake aachwe aendelee na maisha yake.
   
 5. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu unasemaje ? Hii iko katika Electral mannifesto yetu CCM kaa mbali kabisa tutapaje kura za vijana bila kuwaweka sawa?
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Watanzania wenzangu.

  Naomba niongelee kwa ufupi sana kuhusu national service program a.k.a. JKT:

  Kama kiingereza kidogo nilichonacho kinanitosha kutafsri kwamba "National Service" inamaana ya kulitumikia Taifa, ya kutoa huduma kwa taifa.

  Kwa maana kwamba kila raia mwenye umri zaidi ya miaka 18 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ali/anastahili kulitumikia taifa lake kwa lazima kwa kipindi kisichopungua miezi sita... au kwa sasa twaweza hata sema miezi mitatu.

  Cha muhimu ni kwamba tuzungumzie kutumikia taifa kwa maana kutoa huduma kwa taifa, sio tafsiri tuliyonanyo leo ya kwamba JKT au National Service ni kulenga shabaha, kupiga gwaride na kulima tu, tena ati kwenye makambi tu.

  Tupanue tafsiri ya national service a.k.a huduma kwa jamii iwe kila mtanzania akishafika elimu ya juu/kati (yaani post secondary school)... ndani ya miaka mitatu baada ya kuanza kazi yoyote ile... alazimike kutumikia jamii kwa wiki 6 compulsory... kulingana na fani yake. mfano daktari ataenda kusaidia kwenye hospital za serikali, mwalimu ataenda kufundisha kwenye shule za serikali ... generally wengine wataenda kufundisha kwenye shule za kata... wale wa kutoka Sokoine University of Kilimo watakwenda mashambani etc. kwa wanafunzi wanaweza kwa kweli kuunganisha mara tu wakimaliza shule na wale wengine ambao wako makazini ndio watakalazimia kupewa muda ndani ya miaka mitatu. kukamilisha hii requirement (a bill may be passed through national assembly)

  Mtanzania huyu atatakiwa kwa wakati atakao taka yeye ndani ya hiyo miaka mitatu atoe huduma hiyo na akishamaliza atapatiwa cheti cha kitaifa.

  Pendekezo hili litatatua kwa kiasi kikubwa sana uhaba wa walimu, madaktari etc. Na pia kurudisha uzalendo uliopotea etc.

  Endeeleni kujadili...
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Mfumo wa elimu Tanzania unahitaji msukumo mpya. Hatujajitosheleza na hatuendi na kasi iliyopo katika elimu.

  Kwa vyovyote vile mawazo yako ni moja ya mbinu kadhaa zinazoweza kutusaidia kutatua matatizo hayo kwa kuwasaidia watu wengi kupata ujuzi na maarifa ya kukabiliana na changamoto zinazotuzunguka.

  Bila kuliangalia suala la elimu kwa upana ulionao, hatuwezi kuvuka salama kule tunakotaka kwenda. Tutakwama maana dunia ya mishe mishe haitatusaidia kuweza kunegitiate chochote katika biashara za kisomi zinazoendelea kushamiri kila siku inayopita.
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kasheshe,

  Ni mawazo mazuri sana na hayo ndiyo yaliyokuwa malengo ya National Service tangu mwanzo chini ya Serikali ya Awamu ya Kwanza kwamba vijana waende National Service kulitumikia taifa na sio kulenga shabaha na kupiga gwaride peke yake. Kulenga shabaha na kupiga gwaride vilikuwa ni mazoezi ya kujenga ukakamavu kwa vijana hao. Hata hivyo, baadhi ya wasomi wa wakati huo walikataa hawakutaka kujiunga na JKT wakaona kwamba wanakandamizwa na kulazimishwa kufanya jambo ambalo wao walikuwa hawalitaki na labda hawakuona faida yake .

  Katika kijitabu cha "Tanzania Itajengwa na Wenye Moyo" chenye maneno ya hotuba aliyoitoa Mwalimu Nyerere mwaka 1966 Oktoba baada ya kuwafukuza wanafunzi wote walioandamana kugomea National Service; anaelezea wazi kabisa madhumuni ya kuanzishwa kwa JKT nchini. Nikinukuu Mwalimu alisema:

  "Wananchi, National Service hatukuanzisha sisi. Mataifa mengi duniani yana National Service. Taifa linawaambia vijana wake; tunataka vijana mlitumikie Taifa lenu. Taifa linadai utumishi toka kwa vijana. Linadai huduma kwa vijana. Na vijana wanaitika wito huo kwenda kulihudumia Taifa kwa kazi yo yote ambayo Taifa linahitaji ifanywe. Kwa desturi "National Service" au huduma wanayoitiwa vijana hawa wa mataifa haya mengine duniani, ni huduma ya kivita. Wanaitwa vijana wafundishwe kazi ya kivita. Ikiwa kesho na kesho kutwa hapana budi, basi waende wakapigane …. Hiyo ndiyo National Service ya kawaida kwa mataifa mengine duniani…… Na sisi, wananchi, tumeanzisha National Service hapa. Tofauti ya kweli baina ya National Service yetu na zingine ni nini. Kwanza, ya kwetu si ya kivita; ni ya UJENZI. tumewaita vijana waingie katika National Service, na kazi tutakayowapa ni ya UJENZI KATIKA NCHI."

  Juu ya
  "kila mtanzania akishafika elimu ya juu/kati (yaani post secondary school)... ndani ya miaka mitatu baada ya kuanza kazi yoyote ile... alazimike kutumikia jamii kwa wiki 6 compulsory... kulingana na fani yake."

  Tangu mwanzo, hiyo ndiyo ilikuwa nia na madhumuni ya National Service kwamba kila Mtanzania mwenye elimu ya chini/ elimu ya juu/kati na hata yule asiye na elimu aende National Service kutumikia jamii kwa miaka miwili au miezi kadhaa kulingana na fani yake. Lakini Wahitimu/Wasomi wale walikataa mpango huo. Tena hao waliokuwa wakigomea mpango wa National Service (mpango wa kutoa huduma kwa Taifa lao) walikuwa ni wale ambao walisomeshwa bureeee na taifa hadi Chuo Kikuu!

  Sioni ni muujiza gani utatumika kuwafanya wale ambao leo hii wamejisomesha ama wamesomeshwa kwa shida na wazazi wao bila msaada wowote wa Serikali kukubali kirahisi kwenda National Service kujitolea hata kama ni kwa miezi mitatu tu.


  Kwa maoni yangu nadhani inabidi kwanza ifanywe kazi upya ya kujenga PATRIOTISM kwenye nyoyo za Watanzania hususan vijana ili waelewe vyema na kukubali kwamba wanao wajibu mkubwa wa kujitolea kulitumikia Taifa lao kwa kujiunga na National Service ama kushiriki katika mipango mingine yo yote ya kujitolea kwa manufaa ya Taifa.

  Nadhani Sheria ya kwenda National Service ilitungwa wakati ule. Kama ilifutwa basi irudishwe ili iwe ni lazima na si hiari mtu kwenda National Service.

   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Maneno mazito sana haya mkuu!!! tuendelee kuchangia maoni kwa uzalendo wetu ... kila jambo linalojadiliwa hapa JF kwa umakini litawahi kuwafikia wadau (serikali, bunge, wananchi) wakati fulani iwe mwezi huu, mwaka huu au muda mwingine huko mbeleni.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,764
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,

  ..Ghana wao wanachukua vijana waliomaliza vyuo vikuu na kuwapa kazi ktk maidara ya serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja. vijana hao huwa wanalipwa allowance ndogo na siyo mishahara.

  ..JKT hii ya miaka nenda rudi ibakie kuwa "chekeche" la vijana wanaotaka kujiunga na JWTZ,POLISI,na MAGEREZA, kama NCOs [Non Commisioned Officers].
   
 11. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nataka kwenda kutumikia taifa Benki Kuu. Kwani lazima kina kagoda tu wakatumikie huko na sisi tuishie Mgambo na Ruvu? Halafu wewe kasheshe, tukalime na kuchezea mikia ya ngombe wakati wenzetu wananyonya tu kilaini na mijumba ya vibilioni kazaa achilia mbali mausafiri na mialawansi ya chai n.k.

  Tukubaliane kwanza jinsi ya kuigawa Tanzania kila mtu akishapata chake ndio tuamue kuwekeza na kuijenga pamoja! Wao wanapatana jinsi ya kuimega nchi dodoma na sisi tunaweka mikakati ya kwenda kulima wakati hata hiyo mbolea wanauza kwa magendo DRC na Malawi!
   
 12. K

  Koba JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Hivi kuna tofauti gani kwa wale walioenda JKT na ambao hawakwenda? JKT was a waste of time kwa vijana wengi na ni chombo cha propaganda tuu za CCM na serikali yake kuharibu watu akili na sera zao za ujamaa uchwara,ndio maana mpaka leo nchi imejaa mafisadi na wababaishaji.
   
 13. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Sasa Mkuu Koba wewe unazungumzia PAST, wenzio hapo waliotangulia kuchangia wanazunguzia FUTURE...!!!

  Tunaomba mchango wako kwenye Future ya JKT.
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145

  Exactly this my point, tutumikie taifa kwa skills zetu mbalimbali na tuone fahari kutumia elimu yako ya historia kwenda kufundisha shule x.
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Kwani tatizo letu ni pesa? Mbona nyingi tu wanatumia kubembea na kuwapa wengine wajiridhishe mfano EPA, IPTL, Richmonduli, RA., Loliondo, Ndulu na hekalu lake, etc etc.

  Au kuna wa kulipwa na wengine wasio wa kulipwa?
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Hatuna tatizo la pesa...ni tatizo la strategies and priorities zetu kuhusu yale yanayotuzunguka.
  Kuna vitu vingap ambavyo havina lolote la kuongeza na kila siku tunapangia hela za matumizi huko?
   
 17. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  You made my day!!!
   
 18. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kwamba waliomaliza vyuo vikuu na kidato cha 6, watapelekwa JKT na kambi zimekwisha andaliwa.
  Mwenye taarifa za kuaminika atujuze tafadhali
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  mataahira hawa jamaa
   
 20. M

  Mmanyi Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui
   
Loading...