Natarajia Kuhamia Kigoma Mjini! Nipe Tofauti Ya Maisha Na Dsm

mzama chumvini

JF-Expert Member
Mar 14, 2016
730
641
Sabakher Wadau;
Nimepata Job Kigoma Baada Ya Kuona Hapa Mzumbe Wananizingua! Nitakuwepo Pale General Hospital! Ningependa Kujua Tofaut Ya Maisha Iliyopo Kat Ya Dsm! Na Kigoma!! Ili Nipate Mwangaza Maana Sijawah Kufika! Shida Ndo Zinanipeleka Huko.
 
maisha utofauti ni inategemea na mtu mwenyewe mkuu..
kama wewe mtumbuaji mpenda zama chumvini kama jina lako, mpenda anasa mpenda starehe ..ukifika uko utakutana tu na wenzio watakao kuonesha jiji
kama wewe mpenda maendeleo nadhani ni nafasi yako nzuri ku save na kujikita na fursa za ujasiliamali, kwasababu jiji lolote ( except arusha na mengineyo yaliyo changamka ) apart from Dar, ni fursa ..tena especially kwako ulietokea dar umeona changamot9 nyingi..
 
Nilikuwepo Kigoma...mazingira ya pale ni mazuri sana, ni mji unaovutia sana pia pia hali ya maisha ni nzuri sana gharama za vitu zipo chini tofauti na Dar halafu kama unataka kujiongezea kipato basi Kigoma kuna fursa nyingi sana...nakushauri nenda tu ila kuwa makini ule mji una starehe sana hivyo usipokuwa makini hela yako itaishia kwenye bata aiseee..
 
**** kuna mikoa ambayo ni ya ovyo kigoma namba 1, Mpaka leo Jamaa wana mambo ya Umwinyi, Nakushaur kuwa Makin na watu wa kigma ni wasalit kama kiongoz Mkuu
 
It's a nice place hasa mitaa ya mji mwema, ina hali ya hewa km arusha hivi, khs unafuu wa maisha si sana maana vitu vinatoka dar, means transportation cost inafanya vipande! Beach zipo km 3 hv za kawaida! Husipende shobokea madada wa ujiji km ujaoa utaoa, uwe makini na omba omba maana kuna wengi balaa husipende kutoa hovyo, ni mkoa wenye vichaa wengi kinoma, husiibe au kudhurumu! Fursa zipo maana wazawa ni wavivu na hawana kununua vitu ki ukoo km kilimanjaro! Nakukusitizia sehemu nzuri ya kukaa ni mji mwema! Hospital IMO maweni sio mbali toka mji mwema rami tupu na km bajaji ni jero tu
 
Kigoma wasiojua wanaeza upondea sana ule mkoa. Kigoma ni mji mzuri sana kimaisha, hosipatal ya maweni pia ipo poa sana. Nenda mkuu ukiwa mjanja utayafurahia maisha. Siyo mji mkubwa na hauna heka heka kama dar ila kama ni mpendamaendleo unaeza tengeneza Pesa kigoma. Epuka sana totoz za pale kwani ni mufilis agent.
 
Kila kitu almost utakuta ni tofauti. Kama unapenda club kule hamna Kuna ukumbi tu wanapiga muziki.
Mji umejikusanya along kasulu road na njia inayoenda mjini, daladala za fasta ni bajaji bei 500, mjini saa moja tu pako kimyaa. Kuna imani bado za giza giza hivyo epuka kabisa wizi au dhuluma,pia imani hizo hadi kwenye mapenzi na biashara.
 
Kama akili yako haina mchangamchanga .....utakuwa milionea...pia hakuna foleni wala fukuto.......
 
**** kuna mikoa ambayo ni ya ovyo kigoma namba 1, Mpaka leo Jamaa wana mambo ya Umwinyi, Nakushaur kuwa Makin na watu wa kigma ni wasalit kama kiongoz Mkuu
eti na huyu ni great thinker,aiseee
Akili matope,mjifunze kusoma na kuelewa na kuchambua umechoulizwa.
Mtu kaleta hoja nyingine,wewe akili tope kwenye Siasa tuuuu
 
Jiandae kulala ndani halafu unaamka asubuhi nje tena umepakwa matope achana na kina brother K
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Utaipenda zaidi ukienda na ndege lakini kwa basi (hasa kibondo na kasulu)humo njiani hahahaaha utaanza kuichukia kigoma kabla hata hujafika.


Anyway mkuu vipi mbona unatupia sana thread Leo.
 
Jiandae kulala ndani halafu unaamka asubuhi nje tena umepakwa matope achana na kina brother K
Si kweli hizo hizo imani za kipumbavu...nimekaa Kigoma zaidi ya miezi sita kwa kazi maalumu pale Kibondo, Kasulu na Kigoma Mjini sijawahi kumbana au kusikia hivyo vitu...imani mbovu ukiiendekeza inakutokea puani
 
Back
Top Bottom