Baada ya kutazama utendaji kazi wa Rais wangu mheshimiwa JK na kufanya self assessment nimegundua kuwa naweza kuwa Rais wa Nchi hii....
Moja Kati ya kazi kubwa anayofanya JK ambayo nami naiweza vilivyo ni kupanga na kukubali mialiko ya nje na kusafiri hata Kama ni kufungua NGO, kupiga Picha na wasanii, na kuhudhulia mazishi.... Hizi ni kazi nilizozipenda tangu udogo wangu.
Kingine ni kukimbia matatizo yanapotokea kwa kukimbilia nje ya nchi na kumkabidhi Waziri Mkuu wangu kwanza achemke kisha Kuja kuyamaliza either kwa kukaa na wazee ww Dar es salaam Au hotuba Ikulu Huku ukichekacheka ... Hii experience nayo ninayo Kwani niliwahi kuwa muigizaji...
Kazi nyingine ya kuudhulia mazishi ya wasanii na kuwatembelea wakiwa wagonjwa ... Nayo nahifahamu vizuri sana na pia ni mwepesi Wa kufuatilia mazishi yenye ujiko...
Na kazi ya kupokea na kujaribu suti nayo sidhani Kama itanishinda Kama ninavyoweza kuhaidi mambo Mengi bila kutekeleza.....
Wana bodi nawaombeni mniorodheshehe kazi zingine za Rais ili niweze kujipima vizuri kabla sijaingia kwenye uchaguzi