Natangaza kugombea Urais

Natangaza kugombea Urais

Kwa jinsi ulijipanga Dr Slaa anaweza kupata kura 50.
 
kweli mkulu kafanya urais kuwa ni kazi rahisi na nyepesi ,nakumbuka katika hotuba ya Mwl nyerer alisema ,"ikulu si mahali mahali pa kukimbilia kwani hakuna biashara yoyote ya kufanya"
 
Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Kwi! , Fastjet a.k.a Vasco Da Gama !
 
Baada ya kutazama utendaji kazi wa Rais wangu mheshimiwa JK na kufanya self assessment nimegundua kuwa naweza kuwa Rais wa Nchi hii....

Moja Kati ya kazi kubwa anayofanya JK ambayo nami naiweza vilivyo ni kupanga na kukubali mialiko ya nje na kusafiri hata Kama ni kufungua NGO, kupiga Picha na wasanii, na kuhudhulia mazishi.... Hizi ni kazi nilizozipenda tangu udogo wangu.


Kingine ni kukimbia matatizo yanapotokea kwa kukimbilia nje ya nchi na kumkabidhi Waziri Mkuu wangu kwanza achemke kisha Kuja kuyamaliza either kwa kukaa na wazee ww Dar es salaam Au hotuba Ikulu Huku ukichekacheka ... Hii experience nayo ninayo Kwani niliwahi kuwa muigizaji...

Kazi nyingine ya kuudhulia mazishi ya wasanii na kuwatembelea wakiwa wagonjwa ... Nayo nahifahamu vizuri sana na pia ni mwepesi Wa kufuatilia mazishi yenye ujiko...

Na kazi ya kupokea na kujaribu suti nayo sidhani Kama itanishinda Kama ninavyoweza kuhaidi mambo Mengi bila kutekeleza.....

Wana bodi nawaombeni mniorodheshehe kazi zingine za Rais ili niweze kujipima vizuri kabla sijaingia kwenye uchaguzi
Khaa!!! kumbe wewe bogasi hujajua vizuri halafu unatangaza nia!!!! Kajipange upya!!!!
 
Niko Ikulu hapa mh analalamika,anasema viwanda alivyoanzisha kwa ajiri yakuzalisha nguvu kazi ya Taifa vimegeuka kuzalisha majungu na unafiki,na kila anachobuni nyie mnaiga tu na kumnanga,Nashauri mods waondoe huu uzi tucje ikosa JF
 
Kaka Rohombaya hapo lengo ni kuwa makini zaidi sitaki nimisi kazi za Rais.... kama unafahamu hata moja ambayo sijajiandaa nayo ni vizuri ukanikumbusha


Khaa!!! kumbe wewe bogasi hujajua vizuri halafu unatangaza nia!!!! Kajipange upya!!!!
 
Mzito Kabwela nadhani hujanisoma vizuri.... nakushauri urudie kusoma upya uzi huu... Nipo napiga Jaramba kugombea Urais 2015.... Bila shaka umeelewa!!!! nje ya hapo napata mashaka na ubongo wako .si vibaya ukapimwa

Unaonaje ukiwa nyumba ndogo yake msaidiane kutatua matatizo ya kifamilia? Au hupendi kuwa second lady mkuu muonamambo atakapoukwaa urais?
 
Tongs Hilo nimejiandaa vya kutosha kwani viburudisho vyote vya tangu primary, secondary na university na hata wale niliokutana nao mtaani orodha yao nimeiweka vizuri kusubiri nitakapokuwa Rais wa nchi hii
Una viburudisho vya kutosha kujaza nafasi za viti maalum, ubunge wa kuteuliwa, u-DC, nk?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom