Natangaza kugombea ubunge jimbo la KARATU...

Natangaza kugombea ubunge jimbo la KARATU...

Hawa ndio waleta fujo,unaanza kwa kusema utagombea ubunge na usipopitishwa na chama utaona unaonewa kwa jinsi ulivyojiaminisha,umeshiriki kujenga chama au unaibuka kwa tamaa ya ubunge,kwanini usingeanzia kwenye serikali za mitaa.
Kuna mwingine namsikia jimbo la Busega wakati kwenye kujenga chama alikuwa anakisaidia ccm

mkuu sio lazima kuanzia serikali za mitaa mbona David Silinde alipomaliza chuo alienda mbozi akagombea na akapata,ni ibara ipi ya katiba inayosema mtu akitaka kuwania au kugombea nafasi ya ubunge ni lazima aanzie kwenye serikali za mitaa
 
Mkuu ni haki yangu kikatiba kugombea nafasi yeyote ile ya uongozi kama mtanzania ,,Natse unayemzungumzia pia ana haki yake kikatiba, kidemokrasia sasa sioni kinachokupa shida hapo wew hapo....
jibu maswali yote....ujiandae kisaikolojia pia maana hutapita popote
 
Kilala kheri mwanafunzi wangu!!!!!Ila umewauliza wazee wa kwetu wanasemaje!!!Je umeshapitia rika lako na wanakuunga mkono!?Akina mama je!!?Nini malengo yako!!?Utawafanyia nn wanakaratu!!!Karatu ni mji unaokua kwa "speed" sana kwa sababu ya uttalii!!Je vijana wasiokuwa na ajira pale vijiweni utawasaiidiaje!?Stand yetu kweli siyo nzuri!!!Sehemu ya kuingia na kutoka ni ndogo sana kiasi magari/mabasi makubwa inawawia ngumu kuingia na kipindi cha mvua maji hutuama kiasi abiria tunakosa hata pakukanyagaa!!!!Naomba mikakati yako uliyopanga na msukumo uliokutuma kugombea ubunge jimbo la Karatu!!!!Karatu inawasomi wengi sana wenye degree;masters;PhD nk!!!!Tufafanulie wana Karatu ili tuukuunge mkono!!!!!!!
Daffi Karatu
 
Haraka haraka haina mbaraka.

Lakini huu ni ushauri tu kwako wewe mwanafunzi, unayetarajia kumaliza masomo yako ya chuo.
 
Utuambie kwanza umekisaidiaje chama huko chuoni unakosoma?
Kama umekuwa "passive" chuoni huku upo chadema,itakubidi USUBIRI kwanza.
Tuambie!
 
Umewasaidiaje wanachuo wenzako kwenye matatizo mbalimbali waliyonayo?
 
xayeng aha mas karatu kwaxueeke jimbor ar KILINDI ner HANDENI irqo kar ur kuliko wenyej?has kilindi.s\mitaa slemero irqo
 
Karatu pale kuna magiant wamejipanga sijui km utapenya..kuna lazaro, natse, sisilia,napia sarme yupo usa huyo
 
Kiongozi inabidi utueleze japo kwa kifupi harakati zako kichama yaani umekifanyia nini chama mpaka hapo ulipo.

Na kwanini umeona unaweza kuwasaidia wana karatu kupitia ubunge na wala si ujumbe au uenyekiti?

Kabla ya kuja kutangaza nia hapa JF ulisha tangaza mahali gani pengine?...na mtazamo wao ulikuwaje juu ya suala lako la kutaka kucontest hiyo nafasi ya ubunge?
 
Kila kheri Kamanda ila hakikisha una dhamira njema toka ndani, Pia usikatishwe tamaa na watu wachache kama una uwezo Mungu Isack atakusaidia, Muhimu kuwa mnyenyekevu na usije ukathubutu kujihusisha na siasa chafu.
 
mkuu sio lazima kuanzia serikali za mitaa mbona David Silinde alipomaliza chuo alienda mbozi akagombea na akapata,ni ibara ipi ya katiba inayosema mtu akitaka kuwania au kugombea nafasi ya ubunge ni lazima aanzie kwenye serikali za mitaa

kijana unamfahamu Silinde lakn hadi ujilinganishe naye?
 
Back
Top Bottom