Natangaza kugombea ubunge jimbo la KARATU...

GJHariohay

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2013
Posts
1,041
Reaction score
1,161
Wanabodi amani iwe nanyi na poleni na majukumu ya kutafuta rizki....

Jimbo la Karatu ni jimbo lenye heka heka nyingi sanaa za kisiasa, ni kiini cha mabadiliko katika nchi hii, ni kati ya maeneo yenye historia kwenye medani za kisiasa,, jimbo hili limekuwa chini ya CHADEMA toka mwaka 1995 kipindi hicho mbunge wake akiwa Mh. DR.WILLBROAD PETER SLAA.... nimeamua kujitosa kugombea jimbo la Karatu kupitia chama changu CHADEMA,, sifa zote ninazo, ntafuata taratibu zote ndani ya chama changu ,,nitayasikiliza na kuyahishimu mawazo na maoni ya viongozi wangu wa chama,, umri wangu unaniruhusu,jimbo lile kwa sasa linahitaji kijana ambaye ataweza kuendana na pilika pilika za maendeleo ya haraka kwa jimbo lile,, barabara za mji na stendi ya magari ni changamoto kubwa sanaaa kwa mji wa karatu wenye vyanzo vingi sana vya mapato ikiwemo utalii ambapo Karatu ni center ya hifadhi za NGORONGORO na MANYARA,, mji una hotel nyingi sana kitalii,rasilimali za madini nk....
Maji bado ni changamoto kubwa sana wakati mji wa karatu umezungukwa na rasilimali nyingi sana misitu ambayo ni chanzo kizuri cha maji....

Ndugu zangu wanakaratu mnahitaji kijana atakayeweza kuendana na siasa za speed kubwa kwa maendeleo ya haraka sanaaa...... Kijana wenu kamanda HARIOHAY nahitimu chuo mwaka huu mwezi June,, nakuja kujitosa ili jamii yangu inufaike na elimu yangu na nguvu yangu...

Naomba mnipokee ili tupate maendeleo ya haraka sanaa,, Mimi ni mtoto wenu nimesomea shule yenu ya kata,, sasa naomba muonje matunda ya mtoto wenu ambaye ni zao la shule zenu za kata, nazijua changamoto zilizopo kwenu, maisha yenu nayajua vizuri,, familia yangu ni kimaskini sana, naamini nitawatumikia kwa upendo na unyenyekevu wa hali ya Juu.

Ahsanteni sanaaa Mungu awe kiongozi wetu daima....

Wenu,

Gjhariohay!
 
Weka cv yako hapa sisi ndyo wapiga kura karatu tangia 95.ndyo tunayoibeba cdm karatu.
 
tangu slaa amkabidhi mikoba mchungaji Natse hatujaona kashikashi zozote kutoka kwa mh Natse ni wakati sasa awaachie vijana wenye upeo mkubwa wafanye kazi,mkuu nakuunga mkono
 
Ahsante sana kiongozi .....Mungu atupiganie tuyafikie malengo tunayoyakusudia
 
UNAMALIZA CHUO GANI? au chuo cha kata pia?? unatafuta ubunge au ajira? kwann usianzie chini? kwann Natse hafai wewe unafaa
 
Mkuu ni haki yangu kikatiba kugombea nafasi yeyote ile ya uongozi kama mtanzania ,,Natse unayemzungumzia pia ana haki yake kikatiba, kidemokrasia sasa sioni kinachokupa shida hapo wew hapo....
 
tangu slaa amkabidhi mikoba mchungaji Natse hatujaona kashikashi zozote kutoka kwa mh Natse ni wakati sasa awaachie vijana wenye upeo mkubwa wafanye kazi,mkuu nakuunga mkono

Kumbuka Natse kwenye utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo yuko vizur! Ila pilika za jukwaani ndo kidogo huwezi mwona
 
Hawa ndio waleta fujo,unaanza kwa kusema utagombea ubunge na usipopitishwa na chama utaona unaonewa kwa jinsi ulivyojiaminisha,umeshiriki kujenga chama au unaibuka kwa tamaa ya ubunge,kwanini usingeanzia kwenye serikali za mitaa.
Kuna mwingine namsikia jimbo la Busega wakati kwenye kujenga chama alikuwa anakisaidia ccm
 
Back
Top Bottom