Mkuu, hapa umeniwahi, nimesoma mara mbili nikajiuliza, ni mimi tu naona kama huu ni upupu au?
Kama kawaida...........hawasomi hawa!, hii ameinyofoa kwa document za ba**a wake alizofojiwa na wasaidizi wake kwa ajili ya kampeni.............2+2 = 22,
uu UJUHA ndo tusioutaka..........tandaleone and company = 8 X 8 - 64 = ?? weka jibu mwenyewe!!!
Nakusikitikia sana kwa upofu wa kujitakia ndugu.Ila takwimu zipo wazi na bajo hujajibu swali langu la msingi la post hii.
Amefanya mambo makubwa sana ktk nchi hii kwa kipindi chake cha miaka mitano kama ifuatavyo:-No one knows.Ila niko sawa.Hivi JK miaka mitano hajafanya lolote?Weka unafiki pembeni.Niambie ukweli
Utoaji wa huduma za Afya uliendelea kuboreshwa kwa kiasi kikubwa na kuleta
mafanikio yafuatayo:-
(a) Kutoka mwaka 2005 hadi 2009, jumla ya zahanati 464, vituo vya afya 98
na nyumba za waganga 394 zilijengwa.
(b) Zahanati 1,037, vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
(c) Zahanati zimeongezeka kutoka 4,679 mwaka 2006 hadi 5,422 mwaka
2009.
(d) Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 526 hadi kufikia 663 mwaka 2009.
(e) Idadi ya Madaktari imeongezeka kutoka 3,528 mwaka 2005 hadi 4,502
mwaka 2010. Vile vile idadi ya Madaktari Wasaidizi imeongezeka kutoka
9,028 hadi 14,017 katika kipindi hicho hicho.
(f) Idadi ya Wauguzi na Wakunga imeongezeka kutoka 18,123 mwaka 2005
hadi 23,886 mwaka 2010.
(g) Chanjo ya watoto dhidi ya kifua kikuu, polio, kifaduro, pepopunda, donda
koo na homa ya ini iliongezeka kutoka watoto 1,243,388 mwaka 2005
hadi 1,356,421 mwaka 2009. Aidha, watoto waliopatiwa chanjo ya surua
imeongezeka kutoka 1,267,716 hadi 1,455,100 katika kipindi hicho hicho.
(h) Katika kuzuia na kudhibiti malaria Tanzania Bara vyandarua 9,000,000
vyenye viuatilifu vimegawiwa kwa watoto wenye umri wa miaka 5 mwaka
2009/2010 bila malipo. Aidha, vyandarua 4,200,000 vya hati punguzo
viliuzwa kwa mama wajawazito.
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000
mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.
(j) Aidha, katika kuleta ufanisi wa huduma za afya, mashine za kuchunguza
damu, uwezo wa figo na ini pamoja na mashine za X-Ray zimewekwa
katika kila hospitali ya wilaya na huduma za maabara zimeimarishwa.
(k) Kitengo cha magonjwa ya moyo kimeanzishwa na upasuaji unafanyika
nchini. Aidha, mashine 7 za kusafisha figo zimefungwa na hivyo
kuwezesha usafishaji wa figo kufanyika hapa nchini.
(l) Maambukizi ya UKIMWI yamepungua kutoka asilimia 7 na kufikia asilimia
Kaka hapa hakuna wa kukuunga mkono hata kwa moja. Zaidi utaambiwa ni kampeni za kikwete hizo ila sijaona zikiitwa kampeni za lipuimba au slaa. Tuombe mungu atufikishe fainali hapo kwenye uchaguzi. Nchi ya Tanzania ni ya watanzania. Na watanzania ndo watakaoamua ni nani anafaa kuwaongoza na si vinginevyo bila ya kujali vitisho na migandamizo kutoka pande zozote zile. Hakuna mtanzania atakayedanganyika katika kupiga kura, bali ni utashi wake ndo utamfanya amchague anayeona anafaa.
mtu wa pwani- waandishi wetu wengi wa sasa wanatokana na jamii yenye elimu duni kutokana na serikali ya ccm hivyo uchambuzi wao pia una walakini na pia wana uwezo mdogo sana wa kupambanua mambo. Wengi wanafaa sana kwa magazeti ya udaku tu!!
Send this message to 50 different people thank you
naomba utapatie data zilizokuwa kwenye ilani ya ccm ili tulinganishe bajeti na uhalisia uliopo,
yaani useme ccm waliahidi kujenga zahanati 20 ila wamejenga 50, pia utupatie na gharama halisi iliyotumika
kujenga zahanati hizo na utueleze ni kiasi gani cha pesa tanzania inapoteza kwa ufisadi, hapo tutatoa
uchambuzi makini.....
Amefanya mambo makubwa sana ktk nchi hii kwa kipindi chake cha miaka mitano kama ifuatavyo:-
yapo mengi ndugu yangu nafasi haitoshi
- Kufumbia macho wizi mkubwa wa fedha za umma.
- Matumizi makubwa (yenye hati chafu) nje ya bajeti,
- Kuingiza familia yake ktk mfumo wa dola
- kuridhia waziri wake kuingia mikataba ya kitaifa hotelini ugenini.
- kuwaachia majambazi wa EPA baada ya kurudisha walichoiba walipotishiwa na DOLA
- Kutofanya homework yake vyema kuhusu chanzo cha umaskini wa watanzania.
- Ikulu yake kutumia pesa nyingi kwa ukarabati usioonekana.
Sidhani kama mzee madrassa al sul atajibu hili
Sidhani kama mzee madrassa al sul atajibu hili
naomba utapatie data zilizokuwa kwenye ilani ya ccm ili tulinganishe bajeti na uhalisia uliopo,
yaani useme ccm waliahidi kujenga zahanati 20 ila wamejenga 50, pia utupatie na gharama halisi iliyotumika
kujenga zahanati hizo na utueleze ni kiasi gani cha pesa tanzania inapoteza kwa ufisadi, hapo tutatoa
uchambuzi makini.....