Natamani Sana kuanza ufugaji wa kuku kibiashara lakini bado sijaamua nifuge aina gani ya kuku kati ya broiler na chotara

dinkush 1691

Member
Apr 12, 2014
13
4
Lengo langu ni kuanza na kuku 1000 lakini bado sijapata taarifa kamili za mradi wenyewe ninaotaka kuuanza mabanda ninayo kuna Mtaalam aliyakagua akayapitisha kuwa yanafaa.

Taarifa ninazoomba mnisaidie kushea ni tofauti ya ulaji wa broiler na Chotara, mtaji kiasi gani Kwa broiler au Chotara na mchanganuo wake, return ya pesa nitakayoweka n.k kadri ya mchangiaji atakavyoona taarifa anayonipa ni muhimu.

Asanteni 🤝
 
Broiler wanaingia sokoni baada ya wiki nne. Chotara baada ya miezi mitatu mpaka minne. Mpaka hapo kwa kigezo cha muda unaruka na yupi?
 
Nakushauri uende na Broiler.

Soko la kuku-chotara gumu sana. Nilifuga kuku-chotara (Kroiler, Sasso) nikiwa na lengo la kufika kuku 800, nilistop kwa kuku 300 baada ya kuwaingiza sokoni na kugundua soko kubwa ni la broiler na kuku-kienyeji pure, chotara walikuwa wanakataliwa. Wakaishia kuoverstay shambani wakanitia hasara kubwa ya chakula.
 
Kuna ambao wanasema broiler wanatakiwa wiki 8. Chini ya hapo unalazimisha tu na hatakuwa na kilo za kutosha. Sijui sahihi ni kipi.
 
Nakushauri uende na Broiler.

Soko la kuku-chotara gumu sana. Nilifuga kuku-chotara (Kroiler, Sasso) nikiwa na lengo la kufika kuku 800, nilistop kwa kuku 300 baada ya kuwaingiza sokoni na kugundua soko kubwa ni la broiler na kuku-kienyeji pure, chotara walikuwa wanakataliwa. Wakaishia kuoverstay shambani wakanitia hasara kubwa ya chakula.
Mkuu kama hutajali naomba muongozo wa ufugaji wa broiler. Mfano kuku 100 gharama zake inakuje yaani kununua vifaranga, chakula, chanjo na kila kitu hadi hapo watakapokomaa kwa kuuzwa.
 
Kuku broiler 100 gharama zake ni polo nne za chakula
Starter 2
Grower 1
Finisher 1

Bei zinalingana na sehemu uliopo
Kma mimi huku nilipo
Bei ya starter ni 93000- 88000
Bei ya grower ni 860000
Bei ya finisher ni 82000

Broiler wanatumia chanjo moja tu ya siku ya saba ambayo ni Newcastle na bei yake ni 5000 tu

Mpaka hapo ni ww tu na jinsi utakavowatunza mpk kuwauza ni ndani ya wiki 4 tu unauza ila ukiwa mfuko upo vizuri unawaongezea ata wiki 3 ili upate bei nzuri Zaidi
 
Thanks.
Polo ni nini?
Na je baada ya wiki nne huko ulipo unauza kuku mmoja kwa bei gani?
Pia hujaniambia bei ya vifaranga.
 
Aisee tunatofautiana Kiswahili tu sisi wazenji tunaita Polo ila nyie mwaita gunia

Sasa apo bei ya soko ya ulipo mimi siijui m nazungumzia kwa mazingira ya zenji apo

Hlf bei ya vifaranga saivi imeshuka sanaa kwa uko kwenu nahisi ni 150,000 up to 140,000
 
Aisee tunatofautiana kiswahili tu sisi wazenji tunaita Polo ila nyie mwaita gunia

Sasa apo bei ya soko ya ulipo mimi siijui m nazungumzia kwa mazingira ya zenji apo
Hlf bei ya vifaranga saivi imeshuka sanaa kwa uko kwenu nahisi ni 150,000 up to 140,000
Nashukuru mkuu umenipa pa kuanzia.

Polo😂😂. Nimepata msamiati mpya
 
Back
Top Bottom