natamani niandike urithi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

natamani niandike urithi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by rosemarie, Jul 6, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Kila siku nawaza kuhusu nani atarithi mali zangu, naomba kuuliza kama ndio dalili za mwisho wa maisha yangu kukaribia, lakini naapa sitamwandika mrithi mtoto wangu wa kiume kwa sababu mama yake ni mtu mwenye tamaa ya mali.

  Urithi wangu nitamwandika mama yangu ndio msimamizi mkuu, kwisha.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu wewe ndo mwenye tamaa na mali pamoja na mama yako ambaye utamrithisha...Hivi wewe nani mwenye uchungu na mali zako kama sio Mke wako? mambo ya kizamani hayo mzee...mie nikifa leo Mke wangu ndo mrithi wangu na watoto wake acha wazimalize hizo mali zangu lkn ndugu zangu no even touch my WIFE on any decision abaout my wealth....
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  nikupe mfano hai, nina jirani yangu alimwandika dada yake kama msimamizi, mkewe akapinga akamdunda! Mwanamke akaona isiwe tabu akanunua kiwanja, mwanaume akacomplain na yy aandikishwe kwenye kiwanja cha mke. Baada ya ugomvi wakatengana. Leo hali ya mwanaume inasikitisha.gkwa vile watoto wako kwake mkewe analeta chakula mara kwa mara. Ila mke yupo mbali kimaendeleo ana mali chungumzima!

  Hapo ndo ujue mali uchume na nani then mirathi nani! Kwa nini usigawanye mirath sehemu 3 zenye ujazo tofauti kama mkeo anayekuvumilia kwa shida na raha ana 'tamaa?'
   
 4. Tulizo

  Tulizo JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 849
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Duh! ..hayo mawazo yako ni ya kweli kaka? with all due respect kwa mama.. mke wako na mtoto wako ni part and parcel of yourself.

  Kama humuamini mke wako kwanini unaendelea kuwa nae? Kumbuka tamaa ya mke wako haizidi uchungu kwa mtoto wake.. Think twice kaka!
   
 5. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilifikiri ungewaza mkeo na watoto wataishije baada ya kifo chako.................we unawaza mali zako.......ukifa nenda nazo basi!
  Huyo mama yako ulichuma naye?
  Hata kama mkeo ana tamaa na mali,nafikiri tamaa yake ni positive ndio maana mkaweza kuwa na mali hizo....................acha ulembukeni wa mali!
   
 6. s

  shosti JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mhh hii kali mume wa namna hii ni hatari kuliko nyoka mwenye sumu kali!
   
 7. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  oooh! mama mpe chake na mkeo na mwanao wape chao,haija husu malikupewa mama jee mama kama anawatoto mungu amuweke mpaka mwanao awemkubwa amrithishe jee akifaa mapema mali anapewa nani ndugu yako, yani usicheze na maisha ya mtoto wako na mkeo umechuma nae ana haki ya kutumia chako.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Ulikwisha kufa siku mingi...........ni mzoga tu upo barabarani......................wajua nimejuaje? yeyote ambaye amezama kwenye kifo ujue amezingirwa na upofu wa dhambi na aona mauti yamemsogelea....................................achana na dhambi utafikia mahali utasahau kifo.......................
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Haya mawazo ni ya wapi wakuu
  Mkeo ambaye umepata shida nae anaamka asubuhi anakuwekea maji ya ya kuoga, anakufulia mpaka na nguo nyingione umetoka nazo kwa hawara hajali, anakuvumilia kurudi kwako usiku ukiwa umelewa, sometime hata chakula alichohangaika kupika huli kisa ushakula nyumba ndogo, amekubebea mimba na kukuzalia watoto bado unasema hutaki arithi mali yako unaenda kumrithisha mama
  Mkeo angekuw amtapanya mali hata hapo ulipo usingefika ungekuwa ushafilisika siku nyingi
  Kasome kidogo na sheria ya masuala ya mirathi uelewe inasemaje
   
 10. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mnh! Kaazi kwelikweli!
   
 11. kijana makini

  kijana makini Member

  #11
  Jul 7, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  a walking corpse..we ndo una tamaa kuliko hata huyo mkeo..self-centred organism!!!
   
 12. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Kweli walimwengu wanavituko
   
 13. giningi

  giningi Member

  #13
  Jul 7, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama mimi ndo ningekuwa mkeo na nikasikia upuuzi unaotaka kuufanya nakupa kibuti cha nguvu natambaa coz ntajua nilikuwa nakaa na shetani
   
 14. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mwandike japo apate ako ka pick up ka majan..USIMWADHIBU MTOTO KWA MAKOSA YA MAMAKE
  NI KITU CHA HEKIMA..ANDIKA IFI U fil u wan2..write t

  mkeo ump kitu?
  hauna mtoto wa kike?au ndo walewale so bora umpe mama mali zako?
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  wana vituko si kidogo.Nahisi anatamani azikwe nazo.
   
 16. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  da post zooooooooote umu zmetulia.....nadhan uchoyo utamwisha...
  ..uyu ni wale wanume ata wakinunua juic ..anasema i ya baba..wakat wa kula mezan anakula akimaliza anachukua juic kwenye frij anajimiminia uku watoto/watu wote wanamtumbulia macho ata haya hana..uchoyo/ubnafsi moja kwamoja..

  kila kitu kizuri ..paja .kidari chake ole wake mtu akipakue...atafukuzwa nyumba aende kulala nje skuiyo...

  thou mkeo ajasoma post i ..lakin kwa kuwa umemwazia na kumpangia mipango mibaya hauna budi KWENDA KUMUOMBA SAMAHAN...ta km si direct lakin yakupasa kufanya malipizi..nunua japo kanga mwambie mke wangu nimeipenda i vaa....LASIVYO NAKWAMBIA LAANA YA DHAMBI YA UBNAFSI ITAKUANDAMA NA AITAKUACHA KAMWE..utashangaa unafilisika taratiibu na mkeo anaibuka na kushika mali from nowhere...

  uwez jua mkeo alkuwa anavumilia mangap wakat upo nae..km angekuwa na tamaa angeishi naawe mpk sasa?
  au wadhan pia ANAISHI NA WEWE CZ WEWE UNAMALI?

  u mbinafsi thats y kila unachokiona ni mali tu...na jinsi ya kuztia hila..DO U THK MKEO ANA MCHANGO ATA KIDOGO KWENYE IZO MALI ZAKO?
  THK TWCE BRAZA

  IT SEEMS UNA UGONJWA ULE WATOTO WA KIUME UNAWAPATA.... KUMPENDA MAMAKAE KUPITA KIASI KIAS CHA KUGOMBANA NA WAKE ZAO,ATAKACHOSEMA MAMA NDO ANATAKA KITEKELEZWE KWAKE ATA KM MAMA ANAKOSEA ILI MRAD MAMA KASEMA..NA WENgne wanapitiliza na kuishi na mama zao km wapenz wao...
   
 17. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu nilikuwa nipo porini,asanteni wote mliojibu,lakini tatizo nitalieleza hapa peupe
   
 18. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  rose kuna kitu nataka niweke wazi kabla hujaanza kunilaani,huyu mwanamke sio mke wangu,tumezaa lakini tuliishi pamoja kwa muda fulani tukaachana,mimi namwudumia mtoto tangu anazaliwa mpaka sasa hivi ana miaka 14,sababu kubwa iliyonifanye niwaze vile ni yule mwanamke kumilimiki mali tulizochuma tukiwa pamoja ikiwa ni pamoja ni kibanda kidogo nilichojenga kwenye uwanja wao kimakosa,
  nimegundua yule mwanamke ni mtu mwenye tamaa sana ni ikitokea nikafa sasa hivi ndugu zangu na yeye itakuwa ni vita kali mno,yule mwanamke alishaolewa na anaishi na mume wake,nafikiri nimeeleweka wakuu!
   
 19. s

  shosti JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  weka kwa jina la mtoto wako
   
 20. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0


  okkk ..nw i get u
  niliZan ni mkeo wa ndoa na unaishi nae tangu enziiiii na enzi..
  bas fanya iv;HAINA HAJA YA KUMUHUKUMU NA MUNYIMA MTOTO WAKO STAHIKI YAKE KWA kuhofia mama yake atafaidika na mali izo..mpe mwanao urith wake..kwan ana miaka mingap?ata km ikiwa miwili stl ana hak ya kupewa ..

  ulikosea kujenga kwenye kiwanja cha mkeo/cha kwao...mara nyng uwaga vna matatizo ikwemo kuonekana mwanaume hauna chako pale simply cz kiwanja akikuwa chako...na nadhan hasira zote juu ya mkeo zmetokana na kuchuklua/kumiliki kibanda ulichokijenga kwenye KIWANJA CHAO..SAMEHE NA SAHAU..move on na tenda hak kwa mwwanao..usilalie kwenye kosa ili bas ikawa ndo reference ya kila decision unayotaka kufanya juu ya mal unaangalia kesi iyo ya kuchukuliwa kibanda chako...

  ebu angalia kaka..amekudhulumu kiwanja..je alikukata mikono?
  je aukuweza kujenga kibanda kingne?
  je aukuweza kupata na mali nyngne?


  m sure umepata mali nyngne kibaooo na nyumba nzuriii ukajenga ..so wat n y uwaze /uwe na hasira bado juu ya kibanda kile..sahau bwan..kila kitu kina sababu sweetie..uwez jua mungu alilenga nini...WEWE SHUKURU KWA KILA JAMBO ILI MRAD NGUVU UNAZO ZA KUPATA VTU VNGNE BASI KESI IYO YA KIBANDA SAHAU

  sometimess tunafanya makosa....lakin tusijute na kuyabeba makosa maisha yetu yote..we hav 2 foget na ku move on

  pole sana lakin.
   
Loading...