Natamani Niache Kazi

Natamani Niache Kazi

Nina advanced diploma in business management majoring in marketing.Help me wadau.Kama kuna vacancies.Am tired with this captivity of negativity life.

Jiajiri ndugu, hizi kazi hata kama unalipwa Millioni 15 kwa mwezi, bado future ina giza, kujiajiri ndo mpango muzima, hata kama huna capital, start small, kuwa na utamaduni wa kufanya saving, na itese akili yako ifikirie la kufanya na kidogo ukipatacho, waaaallaaahhiiii utatoka
 
Nawakaribisha ktk Entrepreneurial Organization yangu Victorious Youth Enterprises Group-VYEG, ila wavivu hawaruhusiwi uwe mchapa kazi...!! (contact me at: victoriouy@yahoo.com)

Mkuu habari naomba ni PM kuhusiana na hii organization yako nijue shughuli unazoshuglika nazo labda tunaweza kubadilisha uzoefu kidogo,nina kampuni ya Kilimo
 
Jiajiri ndugu, hizi kazi hata kama unalipwa Millioni 15 kwa mwezi, bado future ina giza, kujiajiri ndo mpango muzima, hata kama huna capital, start small, kuwa na utamaduni wa kufanya saving, na itese akili yako ifikirie la kufanya na kidogo ukipatacho, waaaallaaahhiiii utatoka

Ni kweli uyasemayo ST! Ni kweli upo ugumu hakuna anayebisha hilo ila zipo rewards za kutosha in the end ukivumilia na ni sustainable tofauti na kuwa kwenye payroll ya mtu. Actually waajiriwa wengi nikiwemo mm ni modern slaves hata tukatae huo ndio ukweli!
 
Nina advanced diploma in
business management majoring in marketing.Help me wadau.Kama kuna
vacancies.Am tired with this captivity of negativity life.

Mkuu kwa elimu hiyo ya biashara nakushauri uache kazi yako hyo unayofanya na uanze biashara mara moja. ndani ya mwaka utaona mabadiliko makubwa sana.
 
Usiache kazi hata kama mshahara ni mdogo, afu ujue hela huwa haitoshi hata siku moja....
kazini ndo sehemu utakutana na watu watakaokupa channnel zingine
ukikaa home utakuwa dolo tu usiache.
 
Nikiukumbuka msemo wa "acha kazi,uone kazi.........."najihurumia. Kazi mshahara mduchu, pia sio career yangu. Nimetafuta kazi miaka tangu niajiriwe 2011 nikitoka chuo nikajua najishikiza tu. Kumbe dah! miaka inakatika umri unaenda hela haiseviki ingawa nipo single pia pepo wa madeni ananiandama.

Najiona napoelekea ntakuwa tapeli.

God bless me and all who feel the hardships like I do.

mkubwa acha kazi tuje tusugue mabenchi ya kitaa pamoja maana nakuhisi umemisi kitaa ur welcome but mwenzio nikipata hata hiyo ntashukuru mungu.....siku zote mtu anajipanga alipo na ulipo ndio pakuanzia ukitaka kushuka theni kupanda tabu maisha ni kama mbio za marathon mkubwa
 
Kwani unapokea mshahara sh ngapi? Maana mshahara unaweza kuwa mkubwa ila matumizi yako yakawa si mazuri. Weka figure tujue kama kazi unayofanya hailipi!
 
hheri yako wewe uliepata mshahara na kukesha club kuliko huyu anaetafuta kazi bila mafanikio..
kuna mahali amesema amekesha club utajuaje anasomesha nduguze?utajuaje ni familia maskini anasaidia ndugu zake utajuaje amepanga na kodi ni kubwa .acha kuwaza negative mtu akisema yuko singo sio club tu ndugu yangu!!!!
 
Pumba Kuu................mtu yuko serious wewe upo kifeisibuku, pataanzishwa jukwaa lenu la "pampers" mtaendaga huko
Wasio na akili kama wewe hawataki kuambiwa ukweli kwani ni zito wa kufikiri. Hili ni jukwaa la wenye kutumia akili sio vilaza kama wewe mwenye kutuletea upumbavu kujaza ukurasa. wavivu wa kufanya kazi waanzishe jukwaa lao badala ya kuleta miharo hapa. Ni marehemu tu anayeacha kufanya kazi.
 
Sina ajira nina degree yangu ya bcom acc. Najifunza mengi sana toka kwa waajiriwa, mimi tangu nikiwa mdogo kunamaisha ambayo nilikua ninayapenda niishi ila kilasiku zinaposogea naona ni ndoto hasa ninapo waangalia hawa waajiriwa da sioni hata mmoja ambaye aweza kua mode wangu wote shida tu. Sio siri nazama zangu kwa entrepreneurship japokua sina kitu ila ninania na nimeamua. Tuonane miaka SABA IJAYO TUPIME MAFANIKIO YETU. Best of Luck kwakila mtu kwakile anacho kiamini.
 
Usiache kazi hata kama mshahara ni mdogo, afu ujue hela huwa haitoshi hata siku moja....
kazini ndo sehemu utakutana na watu watakaokupa channnel zingine
ukikaa home utakuwa dolo tu usiache.

unapitaga huku kumbe!!!

Nikajua ni kule tu kwa vitu vyako vya kusuuza macho na vichangamsha roho
 
Pole kaka,nimefanya kaz ya kuajiriwa kama mhasibu kwa mwaka m1 hakuna nlichofanikiwa zaid ya kulipa kodi na kununua tv.mwezi wa 1 nimefanya MAAMUZI MAGUMU ya kuacha kazi.nimeachana na utumwa wa kisasa na vyeo vya kijinga ofisini. Nafanya ujasiriamali wangu kwa kutumia mda kdogo then kpato cha kawaida,huku maisha yanaenda
 
Wasio na akili kama wewe hawataki kuambiwa ukweli kwani ni zito wa kufikiri. Hili ni jukwaa la wenye kutumia akili sio vilaza kama wewe mwenye kutuletea upumbavu kujaza ukurasa. wavivu wa kufanya kazi waanzishe jukwaa lao badala ya kuleta miharo hapa. Ni marehemu tu anayeacha kufanya kazi.

Hv biashara au ujasiriamali sio kazi? Kwa maana kwamba kazi ni ile ya kuwa kwenye payroll ya mtu mwingine tu? Ukianzisha biashara ukamake mshahara wako na may be wa wengine wanaokusaidia kwenye hiyo mission haiwi kazi tena?
 
Hilo ni neno umempa. Inaelekea kwake bwana huyo kazi maana yake kupata mshahara kwa mwezi. Hajui walioajiriwa wanatamani sana kufanya kazi ya ziada kujishughulisha kwa akili zao kujikimu sawasawa. Ni jambo la msingi kabisa kulijua hilo kwa mtu yeyote mwenye akili sawasawa. Mara nyingi hapa jukwaani watu wanasumbua macho ya watu kuleta hadithi za kushindwa maisha ati wanaomba msaada kwa kuwa wanatamani kuacha hili na lile......upuzi mtupu. Mtu anaezaje kupata mchumba akapeleka na mahari akapanga na siku ya harusi halafu aje kwetu kuuliza tumshauri namna ya kuoa mke mzuri au kolewa na mwanaume mzuri?? Hali hiyo naiona kama kutoitumia fulsa ya JF kama resource ya mtu kujiendeleza, misuse of opportunities. Ninadhani watu wa namna hiyo ni kuwakatisha tamaa tangu mwanzoni. Tunataka mtu aseme anafikiria kufanya mradi fulani, sasa anauliza ushauri wa namna ya kuufanya mradi huo kwa ufanisi. Kwani skills zinatofautiana kati na baina ya watu na ni vema kuwa wazi ili kutafiti striking the perfect point ili upate mafanikio. Kwa nini mtu aulize ushauri wa maamuzi yake ya kujikata shingo afe? If one desires to die and chooses the procedure that fits him or her, let it go..... kwani mtoto akililia wembe mpe, itakuwa shule nzuri sana kwake na wapumbavu wenzake. Tutumie mitandao kwa faida na sio kupotezeqana muda. Kujaza threads za kipuzi kunafanya hata zile nyuzi za maana zisionwe kwa sababu ya kuboreka kwa kuziona zenye miharo ingawa hizo hushabikiwa zaidi. Nakubali nyuzi zingine ni za burudani ili waliochoka kufanya kazi kwa bidii wakisoma wacheke kidogo na kurelax kupata nguvu ya kufanya kazi zaidi. BURUDANI, ELIMU na HABARISHO ndio msingi wa chombo chochote cha habari kinachotaka kudumu.

Asante kwa kunirudisha duniani, maana nene mvifile hilo na huyo mwagito.
 
Kugaya haja ya kuvipa muvina vanu tulitofauti moli moli tufika hela. Ene uvipe suva na muhango mnofu uliga hela vanu halafu mwitakila bure halafu tutumila ludali kuvapatanisa badala ya kutumila kuvika mihango ja maendeleo. Nyongise kwa kunzelewa na ndilumba sana!
 
pole sana rafiki..hayo bwana hata mimi yaliwahi nikuta nikaamua kufanya uamuzi mgumu nikaacha kazi. lakini jaribu kuongea na mwajiri wako umuelezee hali halisi ya maisha jinsi yalivyoshuka(hayajapanda) na kuwa magumu anaweza kukufikiria akajua namna ya kukusaidia!

ilikuwaje mkuu ulivyoacha kazi, hebu share experience kidogo, ulishasecure nafasi sehemu nyingine, ulikuwa na some savings au familia ilikubust? kila nikitaka kuacha kazi nasita, kauoga falani kananiingia hivi!? though najua kujiajiri ndo kitu yangu.
 
Back
Top Bottom