Natamani kuchana vyeti!

Natamani kuchana vyeti!

Jamani mwenzenu tangu nimegraduate 2011, B.A Community Development, tena nina GPA nzuri tu, na ni mtu wa kujituma, lakini sijawahi pata ajira mahali popote, NGOs ni nyingi lakini sijawahi hata kuitwa kwa interview katika NGOs zote nilizoomba. Japo naendelea kupambana na maisha ktk nyanja za kilimo na ufugaji lakini duuuh nikiwaona wenzangu wapo makazini (tena wengine nilikua nikiwabeba kwenye group assignment) napata shida nafsini mwangu to the extent that natamani kuchana vyeti vyangu vyoote nikae kama vile sikuwahi kwenda shule kabiiisaaaa!
Kuna wakati nilitembea maofisini katika ofisi ambazo nafahamu fika wanafanya shughuli zinazohusiana na maendeleo ya jamii nikiomba kujitolea buuureeee kabisa, nauli yangu,unch yangu, wao wanipe kazi tu niwe nazifanya, tena nitazifanya kwa moyo, lakini sikupata hata pahala pamoja! nina mapenzi makubwa sana na profession yangu lakini sasa navunjika moyo, najiuliza nini kinasababisha nisikubaliwe hata pale ninapokua tayari kufanya kazi bure (Volunteering), nimefunga na kuomba kwa kila hali, sasa nimebaki kuhangaika na nafsi tu, nawaza kuchana vyeti vyangu vyote, na mabaki niyachome moto, iwe habari yangu ya shule imeishia hapo!
Pole sana. Mateso yakizidi ujue neema inakaribia, mshirikishe Mungu.
 
Siku ukipata kazi utakuja hapa usema hujabarikiwa kupata mume. As siku utakua ulishawaza kuwa ukipata elimu ya degree utafurahi. Binadamu hawezi kuridhika kamwe
 
Nenda MUCE kasome Post graduate Diploma
Kwasasa sina uwezo wa kumudu masomo financial wise. Hata hivyo nadhani changamoto itabakia hivi hivi, si yatakua yale yale tu! Au?
 
Siku ukipata kazi utakuja hapa usema hujabarikiwa kupata mume. As siku utakua ulishawaza kuwa ukipata elimu ya degree utafurahi. Binadamu hawezi kuridhika kamwe
Mume ninae, na mtoto mmoja ninae, labda niambie jingine! Ahsante kwa kuchangia la moyoni mwako!
 
Unajishughilisha na kilimo kipi na unafuga nini? Dada sio razima uajiriwe hata hicho kilimo na ufugaji unawexa kukutoa kabisa, sema labda unalima.huku unamawazo makubwa sana labda ya kuwa by pass hao wadogo wako.

Unaweza fanikiwa kwenye kilimo unacho fanya au ufugaji only kuwa commited na confidence.
 
Wakati wa mungu ni wakati sahihi bado muda wako haujafika mungu Hawai wala hachelewi atakujib tu
 
Ahsante kwa kunitia moyo, amini amini nimewahi hadi kufunga siku 40, nimewashirikisha wachungaji na wanawake wenzangu mpaka nimechoka, yaani wadogo zangu wanaanza chuo 'til wanamaliza, wanapata kazi eti mimi nipo tu! Kuna wakati nalalamika mbele za Mungu namwambia mbona umenipa fumbo kubwa sana, najisikia vibaya sana!
Pole sana tatizolako ni kama langu Nina mwaka Niko home kila ninapopeleka siitwii, najitahi najitahidi kufanya ibada ila bado rizk haijafunguka.
 
Pole sana tatizolako ni kama langu Nina mwaka Niko home kila ninapopeleka siitwii, najitahi najitahidi kufanya ibada ila bado rizk haijafunguka.
Mdogoangu mpendwa, usijifananishe na mimi tena utajitia mkosi! Kaa kimya! Mwaka mmoja bado sana, endelea kumuomba Mungu, usianze kujifananisha na case ngumu kama yangu classmates wangu huwa wananishangaa sana wakioniona sina kazi hawaamini ati! Mpaka najikuta natengana nao coz najiona si wa class yao tena! Siwafurahii tena as classmates!
 
Wakati wa mungu ni wakati sahihi bado muda wako haujafika mungu Hawai wala hachelewi atakujib tu
This is too much! Unless God has a special mission with my life! However, let His will be done! I won't stop proclaiming his highness!
 
Unajishughilisha na kilimo kipi na unafuga nini? Dada sio razima uajiriwe hata hicho kilimo na ufugaji unawexa kukutoa kabisa, sema labda unalima.huku unamawazo makubwa sana labda ya kuwa by pass hao wadogo wako.

Unaweza fanikiwa kwenye kilimo unacho fanya au ufugaji only kuwa commited na confidence.
Ukiona mtu hadi anachanganyikiwa hv ujue mambo hayaendi vile mtu anatarajia. Nalima mahindi tu, nahangaika na ufugaji wa kuku chotara lakini changamoto zimekua nyingi kiasi kwamba zinanivuruga kabisa! Kila nikijitahidi naona narudi nyuma tu! Sijui nimekaliwa na kitu gani!
 
Usichane vyeti mkuu!

Vina maana gani sasa......they've lost meaning! I dont see them as something to be proud of anymore, but otherway round! So tearing and smashing them into ashes is just ok with me!
 
You can count years my dear, wadogo zangu wanaanza vyuo wanamaliza, wanapata kazi mimi nipo nawaangalia tu! I really, feel bad to the extent I don't want to set my eyes on my certificates anymore! Over a long period now I am thirsty of tearing my certificates into smallest pieces and I must make sure they remain only ashes!
Don't do that.....viache tu, Usifanye hivyo.....Unaweza Siku kuhitajika sehemu,ukahitajika upeleke vyeti...alafu ikawa sio.

Nasisitiza vihifadhi tu, ni kumbukumbu yako ya ulivyohangaika Masomoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom