Natamani kuchana vyeti!

Natamani kuchana vyeti!

poor africans kila mtu anamshauri mtoa mada amuombe Mungu! mungu gani mbaguzi huyo
 
Jamani mwenzenu tangu nimegraduate 2011, B.A Community Development, tena nina GPA nzuri tu, na ni mtu wa kujituma, lakini sijawahi pata ajira mahali popote, NGOs ni nyingi lakini sijawahi hata kuitwa kwa interview katika NGOs zote nilizoomba.

Japo naendelea kupambana na maisha ktk nyanja za kilimo na ufugaji lakini duuuh nikiwaona wenzangu wapo makazini (tena wengine nilikua nikiwabeba kwenye group assignments) napata shida nafsini mwangu to the extent that natamani kuchana vyeti vyangu vyoote nikae kama vile sikuwahi kwenda shule kabiiisaaaa.

Kuna wakati nilitembea maofisini katika ofisi ambazo nafahamu fika wanafanya shughuli zinazohusiana na maendeleo ya jamii nikiomba kujitolea buuureeee kabisa, nauli yangu, lunch yangu, wao wanipe kazi tu niwe nazifanya, tena nitazifanya kwa moyo, lakini sikupata hata pahala pamoja!

Nina mapenzi makubwa sana na profession yangu lakini sasa navunjika moyo, najiuliza nini kinasababisha nisikubaliwe hata pale ninapokua tayari kufanya kazi bure (Volunteering), nimefunga na kuomba kwa kila hali, sasa nimebaki kuhangaika na nafsi tu, nawaza kuchana vyeti vyangu vyote, na mabaki niyachome moto, iwe habari yangu ya shule imeishia hapo!
Ukisoma kwa lengo la kuajiriwa utaishia kuwa mtumwa.

Elimu iwe nyenzo ya kukufumbua macho yako utambue fursa zinazokuzunguka na njia bora ya kuyatumia kwa manufaa yako na wengine huku ukitatua changamoto za Jamii inayokuzunguka.

Tumewachoka na mahubiri ya GPA, GPA hazifanyi kazi bila ubunifu maana vyuoni mmefundishwa ku Google tu na kukariri theories which in the practical life are heaven and earth.
 
Huna sababu ya kujiweka mnyonge kwa kukosa ajira.
Una elimu na umesema unajishughulisha na kilimo na ufugaji nayo pia ni ajira unatakiwa uitilie mkazo sana .ulime na kufuga kisasa zaidi.Muulize mama faiza foxy huwa anasema yeye ni mkulima vuna ujuzi kutoka kwake.
 
Mara nyingi sisi Binadamu tumekuwa na Malengo na nia Tofauti na mipango ya Mungu.

Mungu naye amekuwa akitimiza haja za mioyo yetu ili tuu tutambue kuwa hayo tuyatakayo hayatufai kitu bali yale ayatakayo yeye.

Hadi sasa tumuachie yeye atimize kusudio lake kwetu ndipo tupaze sauti zatu na kusema Hakika Mungu Yupo.

Yawezekana kabisa kuwa hukutakiwa kutoka kimaisha kupitia Degree yako!!
 
Chana vyeti sio chochote ukivihitaji baadae unaenda polisi unaandika loss report then unajitangaza katika gazeti la mwananchi huku jitihada zinaendelea.

Muhimu timiza haja ya moyo wako chana vyeti vyote.

Life's too old to cherish what you don't need anymore
 
Wote wanao somaga hii kozi pale Udsm wanapangiwaga vyuo vya grade A au ualimu
 
Aisee ,Wewe chana vyeti,ili akili yako iwaze kujiajiri 100% hata Bilionea Jack Ma wa alipitia uzoefu unaofanana na wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom