Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Nahisi kufikia 2019 magereza yatakua yamejaa na pia mamba wa mto ruvu watakua wamenenepa sana!
BTW: naunga mkono hoja 100%
 
Mimi natamani January makamba, nape nnauye na wote walioshadadia sheria ya mitandao wafe tuwazike tumalize shida. By the way nna maono watakufa soon

Na jela siendi na nisharopoka maono ya Lema

Huyu rais nilidhani angekuwa wa maana kumbe bora mpenda safari Kikwete. Huu udikteta angeupeleka kwenye mambo ya msingi angefanya la maana sana. Seems hana shughuli anazi create kama Mjinga mjinga yule taahira Paul Makonda
Badala ya kuwafunga midomo naona sasa wametufunga Nitro, Exhaust inapumua moto tu na flatouts za maana
Sina hata mtoto jamani wengine tukifa tutakufa kama mbwa wacha nijinyamazie huku lengo kuu likiwa kufyatua watoto kwanza
 
Mkuu,huyu kiongozi sio mbaya ila kuna vitu vichache anakosea kama binaadam kwa kuruhusu mihemko yake binafsi iliyopitiliza kwenye mambo ya msingi,anatakiwa ajicontrol sana kwani mara nyingi jambo hili humuaribia,abadilishe mindset yake juu ya wanaomkosoa,naamini kwa uchapakazi wake akisikiliza hoja zao na kupata ushauri wa watu wake wa karibu anaowaamini zaidi,anaweza kutoboa sana,kwani sio wote wanaokukosoa hawana hoja,akilitambua hilo atafanya mambo makubwa sana

Akizipanga vizuri karata zake,anaweza kuwa the best president ever happened in our country
Naunga mkono anakwenda vizuri ila washauri wanamuogopa kumwambia ukweli akiachia uhuru wa mawazo na kusikiliza zaidi anaweza kuwapiku marais wote but one tuzidi kumwombea yy na Viongozi wengine watende HAKI kwa wote hata kwa wapizani wake na MUNGU atamlinda, amen!
 
Nyie nyote mnaompinga JPM ndiyo mtashindwa vibaya sana kwakua mnashindana na mamlaka itokayo kwa Mungu.Huyo aliyekamatwa kakamatwa kwa mujibu wa Sheria na si kwa maagizo ya JPM.Tuache Sheria ichukue Mkondo wake na si kila kitu kumsingizia Rais.
 
Huwa mm nasema kila siku wakosoaji wa Magufuli hawana hoja kabisa, wanajifanya ma griti thinka kumbe ni ujinga mtupu.

Hoja zao mara nyingi zinaegemea kwenye kumkejeli rais na kumbatiza majina ya dhihaka. Na ona mleta mada yeye amajikita kwenye hekima mara kukosea kingereza, sasa nikuulize wewe mleta mada huo ustaarabu ni upi unaotaka?

Kama ni viongozi wastaarabu alikuwepo JK na tulitokwa mapovu hivihivi.

Tujifunze sisi kwanza kuwa na heshima. Haiwezekani unachukua tu kisimu chako unaorodhesha jejeli kibao kwa rais wa nchi alafu unasema eti huo ndio ukosoaji!
 
Nyie nyote mnaompinga JPM ndiyo mtashindwa vibaya sana kwakua mnashindana na mamlaka itokayo kwa Mungu.Huyo aliyekamatwa kakamatwa kwa mujibu wa Sheria na si kwa maagizo ya JPM.Tuache Sheria ichukue Mkondo wake na si kila kitu kumsingizia Rais.
mamlaka itokayo kwa Mungu ipi?

haaahaaaa.....!!!pole sana
 
Upo sahihi kaka kukosolewa ni sehemu ya kujifunza ukiona mtu hataki kukosolewa atakuwa na matatizo binafsi

Kila binadamu tunajifunza kwa kuambiwa na wengine wapi hapafai na wapi tupo sahihi hii ya kujifanya miungu watu anajiaibisha mwenyewe na taifa kwa ujumla
Mimi sipo tayari kuona taifa langu linadharirika kwa ajiri ya mapungufu ya mtu mmoja
Hivi ninyi huwa mnakosoa au mnaponda?
 
Miezi michache iliyopita rais Magufuli alisema anatamani malaika ashuke [sijui ashuke toka wapi] aje kuizima mitandao ya kijamii ambayo tumekuwa tukiitumia kupashana habari na kubadilishana maoni na mawazo kuhusu mambo mbalimbali.

Baadhi yetu tuliyachukulia maneno hayo kama ishara ya mambo yajayo kuhusu uminywaji wa hii mitandao na haki ya watu kuitumia kwa kujieleza, kutoa maoni, na kuikosoa serikali.

Sasa kitendo kilichotokea jana cha kukamatwa kwa Max kimethibitisha kuwa huu utawala wa Magufuli umeazimia kutuziba midomo kwa kutumia mabavu ya dola.

Kwa hilo mimi nataka huyo Magufuli ashindwe na alegee kabisa. Sitaki kabisa afanikiwe hata kidogo na watu wote wenye akili zao timamu hawana budi kumpinga na kuifanya hizo azma yake iwe muhali.

Kupinga udhalimu ni jambo la adhama. Na huyu mtu tayari keshaonyesha dalili zote za udikteta. Hivyo tumpinge kwa pumzi na nguvu zetu zote. Kwanza ni mtumishi wetu na si vinginevyo.

Hizi siyo zama za kupelekeshana kwa vitisho. Haogopwi mtu zama hizi.

Akichemka tutamkosoa tu. Akichapia Kiingereza tutamcheka tu. Kama hana ngozi nene ya kuweza kumudu na kuvumilia kuongelewa kwa namna yoyote ile basi aondoke. Aachie ngazi.

Mtu mwenyewe kwanza hafai kuwa rais. Hana haiba ya urais, hana hekima wala busara zinazotakiwa mtu wa kiwango cha rais kuwa nazo. Kila akifungua mdomo wake mtu unaanza kuombea asiongee maneno ya kuaibisha.

Sikuwahi hata siku moja kudhani kuna mtu angekuja kumpiku JK kwenye ubomu lakini ndani ya mwaka tu huyu jamaa keshamuacha mbali mno JK. Pata picha hiyo miaka minne iliyobaki hali itakuwaje.

Huyu mtu tumdindie. Tukinywea atavimba kichwa na kujiona ana nguvu nyingi ilhali hana. Hana nguvu za kuweza kuzidi nguvu ya umma.

Kwa hiyo mimi nataka ashindwe. Tena ashindwe vibaya. Je wewe mdau wasemaje?
USHINDWE WEWE MWENYEWE . ULIONAO NDIO MOYO WA HUSUDA, NA HASIDI HAFANIKIWI KAMWE.
 
DAH, mkuu umeongea POINT sana ,tatizo watu wanaendeshwa ka mihemko badala ya kuufikirisha ubongo na tafakuri za kina,kweli kuna haja ya uwepo wa uhuru wa maoni tena mpana na usio na mwisho lakini uhuru huo usiwe wa mtu kaamka na mindoto yake anakuja humu anatoa stori za ajabu ajabu za kutunga tunga kisha aachiwe tu,

hata huko kwa wenzetu uhuru hupo ila wanautumia kwa nji ipasavyo,mfano kuna mijitu hapa Jf lazima kila siku iweke uzi ambao hauna kichwa wa miguu mradi tu naye aonekane ameweka uzi,kwa kweli ukifikiria sana unaona sisi wenyewe ndio tunajikosea heshima na kuifanya serikali itafute nji ya kuminya uo uhuru,ikumbukwe haijakatazwa kukosoa,kaa kukosoa tukosoe sana tena bila aibu wala hiyana yeyote lakini katika kosoa hiyo tuzingatia ukweli,staha na madhara ya huo ukosoaji wake,

wakati mwingine unasoma uzi unajiuliza huyu ni mtanania kweliii au ni pandikizi la mataifa jirani? ndugu zanguni machafuko ya Misri,Tunisia Libya na nchi nyingin za kiarabu kwa kaisi kikubwa yalitokana na watu kulishana matango pori juu ya serikali zao na hiyo ilikuwa ni mikakati ya nnchi za ng'ambo kuziharibu nchi za kiarabu,atokeo yake watu wakaamini propaganda na kuamua kujiweka rehani kwa kitu ambacho hakina ukweli wowote ule,leo hii hata hawajielewi .

Leo hii walibya wanalia,wamisri wanalia,watunisia wanalia ,wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa ujinga ,kwa kudanganywa na kuchonganishwa,

Kuhusu suala la mmiliki wa Jf kukamatwa na leo inasemekana atafikiswa mahakamani,nazani watanzania hapa hatuahitaji kuwa kama WEHU,tusio jua nini maana ya mahakama,maadamu imebainika kile kilichosababisha akakamatwa na kuzuiliwa ndani ,vema tukawa watulivu huku tukiacha mahakama kazi yake ,ndio tuanze kuja na hayo malalamiko yetu mara baada ya maamuzi kutoka kwani ukitazama sheria Mmiliki wa JF na polisi wote wako sawa katika madai yao.

Mwisho watanzania nchi hii ni yetu sote,hakuna mwenye kusema hii ni nchi yangu,kama umezaliwa tanzania mkono wako wa kulia unaalama ya ndui,ni wajibu wako kuilinda tanzania dhidi ya wanapropaganda wanaoishi kwa kueneza maneno ya ajabu ajabu juu ya Tanzania,maneno ambayo hayana hata tone la ukweli.

Tukikubali hali hii mwisho wa siku tutajikuta tunalia na kujutia,mifano ya misri,libya na tunusia sio ya kubeza,tunachotakiwa kuzingatia hapa tusikubali yaliyotokea huko yanatokea hata hapa kwetu,japo kweli kuna baadhi ya maeneo ambapo serikali haijafanya vema lakini subra na utulivu ulio na uvumilivu vibaki kuwa mioyoni mwetu, wenzetu wa Ghana walivumilia mwisho akafanya maamuzi ya kistarabu na maisha yanaendelea,so na sisi hatuna budi kufanya hivyo kama tu tumewachoka watawala hawa tulio nao.
Hivi kwani uzush ukipotezewa shida iko wapi si muwaache watu watoe madukuduku yao jamani maana hatufanani .Mangapi yamepotezewa?Maana hata uzushi nao unaeza ukawa na ka ukweli kakifanyiwa kazi.Kusingiziana kupo ktk maisha ya kawaida na hii inatufanya tuish tukiwa makini.Hayo ya machafuko waachieni wenyewe huko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom