Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
JINA: TUJISAHIHISHE

MWANDISHI: J.K.Nyerere

MWAKA: 962.

Hiki ni kijitabu alichokiandika Mwl Nyerere pindi alipouacha uwaziri mkuu na kuingia kwenye Uraisi-Jamhuri.

Katika kitabu hiki Mwalimu anajaribu kuelezea mambo kadhaa ambayo--kwa mtazamo wake--aliamini ni makosa na mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza ndani ya TANU--kama si Tanganyika kwa ujumla-- ambayo anaisihi jamii iweze kuyasahihisha..(Kujisahihisha ni njia ya kujitafakari na kuamua kurekebisha unapoona hapako sawa).

Mwalimu anaanza kwanza kwa kuufananisha umoja wa binadamu ndani ya jamii na mfumo mzima wa viuongo vya mwili wa mwanadamu. Viuongo hivi ni lazima vitii kanuni za afya na mwili ili visidhuru utendaji wa mwili(jamii). Anasisitiza kiuongo kimoja kikipata hitilafu, inaweza zuia viungo vingine vyote visifanye kazi i.e jamii nzima ishindwe kutimiza malengo yake.


Makosa ya kusahihisha.

1. Unafsi(ubinafsi).
Hili ni jambo ambalo Mwalimu amelieza zaidi ya mara mbili katika kijitabu hiki. Mwalimu anasema kosa kubwa linalofanyika ndani ya jamii au TANU ni wanachama kuishi kibinafsi kwa kuamini kuwa TANU inapaswa kuwafanyia kazi wao na si jamii nzima. Mwalimu anasema watu wa namna hii malengo yao binafsi--na si ya jamii--- yasipotimia basi kwao chama ni kibaya.

2. Woga.

Mwalimu nasema kosa hili hutokana na kosa la kwanza(unafsi). Hii inapelekea katika jamii , watu kushindwa kukemea maovu. Mkubwa anashindwa kukemewa kosa kisa yeye ni mkubwa, na mdogo anaonewa hata kama hana kosa kisa yeye ni mdogo. Woga huu unapelekea watu kutanyamazia maovu na dhuluma zinazofanywa na watu fulani kwa jamii kwa kuhofia kupoteza vyeo vyetu au maslahi fulani--ubinafsi.


3. Fitina

Mwalimu anaielezea hii kwa kuimulika ahadi ya mwanaTANU kuwa, nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko. Mwalimu anasema uwepo wa fitina ndio unaopelekea mtu kutoambiwa ukweli wa dhahiri. Mtu anafanya kosa lakini haambiwi pale hadharani, badala yake watu wanaenda msengenya pembeni. Fitina pia mwalimu anaioanisha na watu kumuonea mtu mmoja aliyefanya kosa dogo kulikuza kosa lake na kuonekana kubwa kama mlima kilimanjaro, na kosa lingine kubwa la mtu mwingine linaonekana kama si kosa.

Mwalimu anaeleza watu wafitini msingi wa 'Ukweli' kwao si msingi wa ukweli wenyewe bali ni mtu...

Fitina inapelekea , wakati mtu mwingine ni kweli kabisa amekosa lakini hakoselewi kwa sababu ya kosa lake, bali hoja zinazotumika kukosoa ni za unafsi.


4. Uchaguzi wa viongozi.

Mwalimu anasema kosa jingine ni kuchagua viongozi kwa msingi wa unafsi. badala ya kuchagua kiongozi kwa misingi ya TANU ,anachaguliwa kwa misingi ya ubinasfsi. Mwalimu anasema hii ni kuua chama.


5.Kutokujielimisha.

Moja ya ahadi ya mwanatanu ni kujielimisha. Mwalimu anasema ni lazima mwanatanu au mwanadamu azidi kujielimisha kila siki, na kujielimisha si tu kwenda darasani. Bali kuutafuta ukweli.

Mwalimu anasema ni kosa na dhambi kubwa kwa mtu kuamini kuwa anajua kila kitu na haitaji tena kujielimisha


6. Kujitweza sababu ya elimu.

Mwalimu anasema lengo la Elimu ni kuitumia elimu yako kwa manufaa ya jamii nzima na si kuwa na elimu na kisha elimu hiyo ikuwekeee mipaka na watu wengi na kuanza kubagua na kudharau watu sababu hawana elimu.


7. Ubaguzi wa kivyama

Mwalimu anasema ipo dhana katika wanaTANU kujiita 'Wao wanaTANU na wale sio wanaTANU.

Hii mwalimu anaieleza watu wasio wanatanu wanachukuliwa kuwa si wananchi na raia bora. Hata wataumishi wa umma hata wawe bora kiasi gani, kama si wanatanu wanaonekana si lolote


8. Ubinafsi wa mawazo

Mwalimu anasema lipo kosa baya linalojengeka katika jamii kuwa wapo watu mawazo yao wanayaona ndio mawazo ya jamii. Likipingwa jambo lao wanachukulia limepingwa jambo la jamii nzima na kujitafutia uhalali kwa jamii, jambo lao linapopingwa eti, ni la jamii nzima.


9. Kuheshimu mawazo

Mwalimu anasema katika jamii kunankuwa na mawazo ya wengi na ya wachache. Katika mjadala ni lazima wachache wapewe nafasi ya kusikilizwa na kuheshimiwa mawazo yao. Lakini hii haimaanishi kuwa ni lazima watakubaliana na mawazo ya wengi. Hata baada ya maamuzi na wachache kukubaliana na mawazo ya wengi, bado demokrasia inawaruhusu kuendelea na imani yao juu ya suala wanaloliamini.


10. Kusingizia mambo juu ya matatizo yetu.

Mwalimu anasema kutokana na kutotumia akili sawa sawa, mwanadamu anatafuta majawabu mepesi kwa mambo magumi. Kukimbilia kusingizia ukoloni au wazungu juu ya matatizo ya watanganyika ni kukwepa ukweli na kutotafuta njia sahihi za kutatua matatizo. Pia mwanadamu anakimbilia kupiga ramli kwa mganga badala ya kutafuta suluhu halisi ya matatizo


HITIMISHO

Mwalimu anahitimisha kwa kusema kuwa kufanya kosa ni kawaida kwa mwanadamu lakini busara ni kujisahihisha na kuepuka makosa. Anatoa mfano, kipofu akikunyaga ni ubinadamu kumpiga kofi, lakini si busara kujitoboa macho ili na wewe umkanyage.
Pia anasema ni ubinafsi kutaja makosa ya watu na kujifanya wewe huna makosa au kuficha makosa. Hata yeye mwalimu anasema anaweza kuwa nayo makosa, bali muhimu ni kutumka akili zetu wanadamu kwa huru bila kutu(makosa hayo) ili kutimiza lengo letu binafsi na ya jamii nzima.

Kwa lengo la kujihukumu wenyewe ( ambalo ni jambo gumu na busara--asilolipenda mwanadamu) na si kwa lengo la kuwahukumu wengine ( ambalo ni jambo rahisi--na alipendalo mwanadamu), mwalimu ameyataja makosa hayo ya WanaTANU ili TUJISAHIHISHE.


*************Mwisho*****************
 
Haya endelea kuamini hivyo
 

Nimekuelewa sana tatizo mihemko ya kisiasa imetawala sana vichwa vya watu
 
Rais ana nguvu nyingi sana ... Rejea kauli za Mwl JK Nyerere ....

 
Hiyo itakusaidia nini?
Unune, ucheke, hata uafanyeje huyo ndo rais wetu
Rais hafanyi kazi kwa kukupendelea wewe
Cha maana ni kufuta sheria na utaratibu
 
Tulimpenda wenyewe. Tujipime sisi wenyewe kama upendo wetu bado upo kwake? kama haupo basi siku hazigandi kabisa tutunze machungu yetu na hasira zetu mpaka wakati utakapo wadia tujitokeze na kumpinga katika karatasi ya Kura. Hii ndiyo demokrasia wandugu.
 
acha kubwabwaja kama kasuku, njia pekee ya kubishana kwa hoja ni kujibu hoja nothing else, hoja ikiwa dhaifu hapa jf inakua debunked tu so if there is nothing to hide there is nothing to fear about any post.
 
Jpm wewe sio Mungu na kumbuka kuna maisha baada ya kufa
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Umewaza mbali.ila in viongozi wachache sana.wanaokumbuka hayo.wengi ulewa madaraka.angalia godwin gondwe.wakati anasoma taarifa ya habari itv.na sasa hivi alivyo.
 
tunapaswa tuwakumbushe maana nao ni binadamu km sisi pia isipokua Mmungu amewapa vyeo tu hivyo hawapaswi kujisahau na pia hakuna atakayedumu milele

Yuko firauni?Hitler ,nk Mwisho wa siku kila mja atarudi mavumbini
 
Hivi mna u hakika kuwa Rais ndiye kaagiza, kiongozi wetu hapa JF akamatwe?
====
Staha katika kumshauri rais ni muhimu.
Si wanasemaga mtu hasemi kisichokuwa mayoni. Malaika ni muujza. Watu wengine sijui wanatoka wapi. Mkiambiwa someni mnaleta phd fake . Haya sasa ndio matokeo yake.
 
Maneno yako na yakapate kibali, kwa Mungu ili yatimie 2020, Ee Mungu baba tunakuomba ukatuinulie Edward Lowasa awe rais wetu wa Tanzania, tunaomba na kushukuru kwa Jina la Yesu...wote tuseme amen
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…