Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
I think those people who counsel him are mad and he himself is mad also..he want to lead grave and dead people as they are the only one who do not ask any question.
 
Uhuru wa habari uko kikatiba na kiukweli unapaswa kulindwa na Mh Raisi pamoja na vyombo vya dola na si vinginevyo. Haki na uhuru wa binadamu hazikutokea mbinguni ila zililetwa na watu. Upatikanwaji wa haki na uhuru wa binadamu ulisababishwa na kutokea kwa matukio yenye historia mbaya zaidi duniani (ni vizuri viongozi wetu wakasoma nakuelewa). Hivyo basi, haki na uhuru wa binadamu unapaswa kuheshimiwa na kupewa hadhi stahiki . Serekali inawajibu wa kulinda haki za watu na siyo kuzivunja. Kwa muktadha huo, ikiwa raisi ameapa kulida na kuitetea katiba hana budi kulinda na kutetea haki zote za kibinadamu zilizoanishwa kwenye katiba. Kama ni kweli muheshimiwa raisi ameyasema hayo uliyoyaanisha hapo juu, basi muheshimiwa raisi anapaswa kuacha kutoa kauli zinazo kinzana na katiba ambayo yeye ameapa kuilinda na kuitetea.

Nakumbuka wakati wa uongozi wa baba wa taifa (mwenye enzi Mungu amrehemu) viongozi walikua wanaandaliwa. Zikuwapo shule mahususi kwaajili ya kuandaa, kukuza na kuimarisha viongozi. Wengi wa wanasiasa waliobahatika kupitia katika mafunzo hayo wameonyesha uhodari katika uongozi na kuongoza kwa kufuata misingi ya katiba, sheria na haki na kuachana na uongozi unaofuata matakwa binafsi. Hali kadhalika, nimeona kwa wenzetu wamarekani, raisi mteule anapewa wasaha wakuelekezwa mambo ya msingi ya kufanaya pamoja na kuwa na mawazo yake ya awali. Hivyo basi, kwa kuwa viongozi wetu hawakuandaliwa katika mifumo rasmi, hizo ndizo changamoto zitokanazo na udhaifu huo. Kwa misingi hii, jitihada za makusudi zipaswa kufanyika ili kuandaa viongozi wetu wa kesho ili kuliepusha taifa letu na mambo amabayo yanaweza kuepukika kwa siku za usoni.
 
Umesahau kuwa kusema mtu wa chombo cha usalama kapokea Rushwa ni jambo Jema kwa mchukia Rushwa lakini ni jambo baya kwa asiyetaka ijulikane
Hoja ijibiwe kwa hoja watu wasifungwe midomo !
Ni kweli ni jambo baya kwa asiyetaka ijulikane, lakin hofu inatoka wapi kama umesema jambo la kweli na una ushahidi nalo??

alaf vyombo vya usalama wapo commited kulinda confidentiality, kama ukisema hapa jf, wakakuhitaji kwa mahojiano zaid ili wapate detail za uhakika, pasipo kumwambia mtuhumiwa juu ya nani aliyetonya, tatizo liko wapi?.

Hakuna aliyefunga mdomo watu, wewe sema tu, lakini uwe na ushahidi na yale unayosema. hata wakikuhitaji kwa mahojiano unakuwa na cha kusema.

Imagine kama mtu aliyesema dangote anahamishia kiwanda Kenya. akiobwa ushahidi wa hoja zake atazitoa wapi??
 
Sasa wewe unadhani kuna haja gani ya kumsaidia vita mtu ambaye hana umuhimu wowote kwenye maisha yangu....sana sana anafanya maisha yangu yanakuwa magumu...ni kweli Kabisa nitaungana na adui yake ili tumshinde na kumvurumishia mbali..
Ha ha ha ha...... mkuu we ni mbinafsi sana. hata madawati yaliyotengenezwa na kupunguza tatizo kwa kiasi kikubwa, bado unaona hajasaidia chochote???

Hata kupunguza PAYE kwa wenzetu wenye mshahara kima cha chini bado unaona hana maana? usiwe selfish sana, eti akusaidie wewe tu ndo uone kuna kitu kafanya.
 
hakuna uhuru usio na mipaka...
nadhani style za uwasilishaji wa hoja zenye kufikisha kisu kwa mfupa....zipunguziwe ukali wa maneno......ili hali kufika kwa ujumbe kuwe pale pale......

hii ya kuuwaslisha ujumbe wa ukweli wa kumuanika mwenye mamlaka na wadhifa wa kiserikali huku umeng'ata meno...ndio iletayo shida....
wanataka information zao za kuwaanika zikija humu ziwe soft kusomeka....
 
Mkuu hayo madawati ni bakuli lilitembezwa kama vile lilivotembezwa kwa ajili ya wahanga wa kagera na pesa kukwibwa




 
Nifikiri baada ya uchaguzi kupita mwaka Jana vyama vyote labda vilikaa chini Na kutafakari wapi vilipo Fanya vzr Na wapi vilifanya vibaya Na kuja Na ufumbuzi mwingine Wa kisera ili kuweza kujipatia mashiko au kupendwa Na wana nchi ili mpk 2020 viwe vzr ktk uchaguzi. Lkn kwa hii Aina ya ccm inavyoenda mmmmmmh sizani km huko 2020 mtafanya vzr..... Naona dalili zote za kukumbana Na changamoto kubwa sn kuliko ya 2015.

[HASHTAG]#FreeMaxiMelo[/HASHTAG]

[HASHTAG]#BringBackBen[/HASHTAG]
 
Ndio maana Nagufuli anaamua kuwabana watu wajinga kama ninyi sasa ishu ya viwanda hapa inatoka wapi? Mpinge Magufuli kwa hoja siyo unakuja hapa kwa vimaneno vyako vya jejeli alaf eti unasema ndio unakisoa

Mie naona hii mada ina fit kabisa kwenye "discourse ya viwanda" inayoendelea kwenye media zetu na baina ya wadau mbalimbali hapa nchini...
 
Thinking outside the box.
Aliyeandika uzi huu ana lengo baya na jamii forums.
Hajauleta kwa bahati mbaya.
Hata wanaochangia kwa matusi bila staha nao ni hivyo hivyo.
Justification inatafutwa.
Very unusual watu kukosa woga na adabu kiwango hiki.
Umeona mbali sana, hongera yako. Nilichagua niwe msomaji lakini post yako imeniingiza uwanjani.
 
I ain't never scared.
Teh nyana bhe okonamala olebocha maboxi okwene neyo ukoyogagusa amanamala Na magikolo ago gakigasha mmanumba ga banamala olo ginyela. Nyanabhe. Neyo olo opuna okono Tz nalekotwala segerea moja kwa moja Na Malya ya shinyanga. [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…