Nataka Rais Magufuli ashindwe

Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
sawa, lakin si bakuli wametembeza wao! mbona akina lowasa na sumaye walipokuwa mawaziri wakuu yaliwashinda kutembeza hilo bakuli watoto wakapata madawati??


Usimlinganishe Lowassa na mambo ya kijinga..isingekuwa ni huo wizi wenu uliohasisiwa na mstaafu mkamtoa kafara sasa hv Elimu ya Tanzania ungekuwa level ingine Kabisa... Yaani kwa sasa tungekuwa tunawaza jinsi ya kuwawezesha watoto wa chekechea kwa laptop na si madarasa na madawati tena...
 
hapa mkuu anakosea uhuru wa habari una faida nyingi kushinda hasara hasa kwa serikali ambayo imepanga kupigana na uovu na uozo, isingekuwa JF huenda sahizi raisi angekuwa mwingine kabisa.... apige kazi akikosea atakosolewa tuu maana yeye ni mwanadamu na akipatia tutamsifu..

Akiendelea hivi atakuta muda wa kutimiza ahadi zake umeisha kisa kusumbuana na kina melo.
 
Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?

Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji

Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?

Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine

Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu

Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.

Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Kuna Uzi wowote ulioanzishwa na Max? Hivi nini maana ya Uchochezi? Nini Maana ya Matusi? Unaweza Orodhesha matusi yanayotukanwa kwa hao wanaokutuma? Na hayo matusi ni kwa nyie tu ila Watanzania Waliokuwa Malofa na WAPUMBAVU Sheria hizi haziwalindi? Hivi waliomtabiria Lowassa kifo wamewahi kukamatwa na kushtakiwa? Wanaokesha humu JF Wakitunga uongo dhidi ya CDM na CUF huwa wanakamatwa?
Kama story ni za uongo Kanusha, fungua kesi za defamation ili upate fidia!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom