Massivve
JF-Expert Member
- Jun 4, 2015
- 274
- 368
Tatizo ni double standards.Ingekua sheria zinatumiwa sawa kwa kila upande haina tatizo.Ni Mara ngapi viongozi wa upinzani wanadhalilishwa na kutungiwa stories za uongo halafu hakuna ufuatiliaji kama akifanyiwa hivyo wa upande wa serikali na chama tawala?Kwani mtu ukitoa maoni yako pasipo kutoa matusi au ukianzisha uzi wenye uhalisia na usio wa kichochezi unakuwa na hofu ya nini?
Tatizo lililopo kuna baadhi yetu tumekuwa maarufu kutunga stori za uongo na kuzijengea hoja then tunataka jamii iamini kama ni kweli kumbe ni upotoshaji
Mtu kama umeanzisha mada yako na ushahidi unao kwa nini uogope? Endapo utahitajika polisi si unapeleka ushahidi?
Fikiria mtu anayeanzisha uzi hapa eti Dangote anahamishia kiwanda Kenya na hizo habari zinasambaa dunia nzima kumbe ni uonge pasipo kufikiria negative impacts kwa wawekezeji walioko huko nje. Mtu kama huyu leo hawezi fanywa kitu sababu tu anatumia ID feki sishangai kesho akaibuka na jambo jingine
Watu wa namna hii lazima washughulikiwe hakuna kulea ujinga. Watanzania tumekuwa maarufu sana wa kupika majungu
Ninakubaliana na wewe kabisa uhuru wa kutoa maoni lazima uheshimiwe na watawala kwani ni takwa la kikatiba lakini uhuru huo lazima uzingatie utu na nidhamu.
Leo mtu akimchukia mtu flani sababu za kiitikadi za vyama au jambo lolote, kesho anamtungia tuhuma na kusambaza kwenye mitandao. Vitu vya namna hiyo siyo vya kulea
Haya ningeyaunga mkono kama sheria zingekua zinatumika kwa wote na haki sawa