Nataka nikasomee Driving, naombeni ushauri wenu madereva

Saoka

JF-Expert Member
Oct 23, 2018
405
565
Habari za leo ndugu zangu,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 nataka nikasomee udereva hasa lengo likiwa nikusafirisha abiria yaani kuanza na magari kama cruiser na Coaster (Manual) na kupata leseni yake

Je natakiwa kuwa na vigezo vipi au process gani nitazifuata kufikia lengo na ipi shule nzuri kwa Arusha?
 
Nenda chuo Cha veta kilichopo karibu na nawe utapata majibu ya maswali yote uliyouliza hapa jukwaani,Ila kila la kheri mkuu na ukawe dereva mzuri unayefuata taratibu zote za usalama barabarani.
Shukrani boss
 
Habari za leo ndugu zangu,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 nataka nikasomee udereva hasa lengo likiwa nikusafirisha abiria yaani kuanza na magari kama cruiser na Coaster (Manual) na kupata leseni yake

Je natakiwa kuwa na vigezo vipi au process gani nitazifuata kufikia lengo na ipi shule nzuri kwa Arusha?
Vigezo:
  • Afya njema
  • Usiwe na tatizo la kuona/kusikia vizuri
  • Usiwe na ulemavu wa Akili /mikono/Miguu
  • Uwe na Muda pamoja ada ya mafunzo

Chuo Bora:
1) Modern Driving school (karibu na Florida)
2) Veta ( Njiro)

Process:

  • Fika chuoni
  • Chukua form na ulipe ada ya mwezi mmoja
  • Anza mafunzo bila kukosa kipindi hata kimoja

Mengineyo:
  • zingatia sana sheria na Alama za barabarani
  • Weka msisitizo mkubwa kwenye Manual driving
  • Ukiwa mafunzo kwa vitendo kuwa wa kwanza kuendesha ukisubiri kuwa wa mwisho mwalimu anakuwa amechoka

- Jiongeze kwa kulijua gari vizuri hata kwa ku google au Youtube upate uzoefu mkubwa siyo kila kitu mwalimu atakufundisha.

Ukishapata Lesseni yako ya kwanza (Class D) utahitajika kupata uzoefu wa kuendesha gari ndogo kwa miaka mitatu. Baada ya hapo utakuja tena Driving school ili uchukue mafunzo ya kuendesha gari za Mizigo na abiria na upatiwa Lessen (Class C ) endapo utafaulu Test.

Xxxxxxxxxx Thread Closed xxxxxxxxxxX
 
Mkuu umenifungua vya kutosha Ebwana ubarikiwe Sana pia naliskia pale Modern wapo vizuri, Ahsante Sana kwa ushauri mzuri
 
Mkuu umenifungua vya kutosha Ebwana ubarikiwe Sana pia naliskia pale Modern wapo vizuri, Ahsante Sana kwa ushauri mzuri
Yes! Wapo vizuri na Wana magari mengi na ya kisasa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ni wewe tu uweke juhudi za ziada kwenye kujifunza na ukiwa na Confidence itakusaidia sana.

Sifa za dereva mzuri:
1) Awe mvumilivu asiwe na hasira anapokuwa barabarani

2) Awe mwepesi kuchukua hatua kila anapoona jambo linaloweza kuleta madhara;

Zingatia haya kila baada ya dakika chache unapoendesha gari...
- Mara kwa mara unapoendesha angalia SIDE MIRROWS kuona kilicho nyuma yako

- Mara kwa mara angalia DASH BOARD yako kupata taarifa za gari lako kupitia sensor na gauge zilizopo kwenye dashboard(Temperature,Oil ,Mafuta,seat belt,Battery.....)

- Mara kwa mara sikiliza SAUTI ya gari yako (engine,body,tairi....) Ili kama kuna kitu hakiko sawa utagundua mapema

- Mara kwa mara sikilizia HARUFU zinazotoka kwenye gari yako kama kuna harufu ya utofauti utagundua mapema( harufu ya Tyre kuungua,plate clutch, Engine kuchemsha, waya kuungua, Mafuta kuvuja....)

3) Asitumie kilevi kupita kiasi anapoendesha gari na azingatie alama na sheria za barabarani.

Nakutakia Kila la heri.
 
Nisikilize bwana mdogo. Sisi ndio wenye hii fani.

Kama unataka kusima kuendesha gari yako, nenda chuo chochote cha jirani yako.

Kama unasoma udereva kama fani ikupe ugali ww na wanao nenda veta,

Hakikisha unapata leseni ya class D, E, C1, C2, C3 na A, A2

Hakikisha unapiga figisu upate leseni kubwa ili anze kukomaa. ukipata leseni ndogo inakuhitaji muda kuibadilisha kuwa kubwa
 
Vigezo:
--Afya njema
--Usiwe na tatizo la kuona/kusikia vizuri
--Usiwe na ulemavu wa Akili /mikono/Miguu
--Uwe na Muda pamoja ada ya mafunzo...
Mkuu mi mwenyewe navutiwa Sana na udereva wa haya magari makubwa maroli na mabasi ivi dereva wa roli na na Basi nani anapata hela kubwa?
 
Yes! Wapo vizuri na Wana magari mengi na ya kisasa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo ni wewe tu uweke juhudi za ziada kwenye kujifunza na ukiwa na Confidence itakusaidia sana.

Sifa za dereva mzuri:
1) Awe mvumilivu asiwe na hasira anapokuwa barabarani...
Shukrani boss
 
Mkuu ili upate class C1 nilazima veta tu vyuo vingine huwezi pata?? Ahsante Sana

Sirudii kuongea mara mbilimbili.
Kama unasomea udereva kama fani ili upate ajira nenda VETA

Kama unasoma udereva kwa ajili ya kuendesha gari lako na mkeo au gari la baba ako nenda Hivyo vyuo vingine

Full stop
 
Habari za leo ndugu zangu,

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 nataka nikasomee udereva hasa lengo likiwa nikusafirisha abiria yaani kuanza na magari kama cruiser na Coaster (Manual) na kupata leseni yake

Je natakiwa kuwa na vigezo vipi au process gani nitazifuata kufikia lengo na ipi shule nzuri kwa Arusha?
Nenda NIT pale
 
kuhusu udereva vyeti tunavyovitambua serikalini ni vya VETA na NIT kwanza vyeti vyao vina watermark yaan alama ambayo kunakili fake huwezi ila vyuo vya VTC au vyuo vingne vyeti vyao wanaprint stationary tu sasa kama unataka ajira ni vizuri usome VETA au NIT
 
Back
Top Bottom