Fani ipi kati ya hizi ina fursa za kupiga pesa?

_ID

JF-Expert Member
Aug 15, 2019
5,409
7,399
Salaam wadau,

Moja kwa moja kwenye maada husika

Mimi ni kijana mwny umri wa mid 20’s. Nina mpango wa kwenda VETA ili kujifunza ujuzi niweze kujipatia kipato. Lengo langu nikasomee kimojawapo kati ya udereva au ufundi simu+computer. Udereva nilioulenga ni Basic driving + ADVANCED DRIVERS GRADE II + HEAVY GOODS VEHICLE(HGV).

Mpaka saizi niko njiapanda je nisomee kozi gan kati ya udereva au ufundi simu+computer. Kozi zote hzi mbili nazipenda, nazimudu na nina vigezo vyote vinavyohitajika kuzisomea.

Naombeni kujua ni kozi gani ina hela Zaidi mana lengo langu ni kusomea kozi yenye hela haijalishi ya kujiajiri au kuajiriwa. Kitu kingne, nmeona kozi ya aina moja ukienda veta chang’ombe unaisoma kwa mda mrefu zaid kuliko veta kipawa wakati kozi ni ile ile , je hii ni sababu ya nini? Kwa anaejua naomba anijulishe sababu Mfano,
  • Kozi ya COMPUTER REPAIR & MAINTAINANCE ukienda veta chan’gombe (ada 280,000) unaisoma kwa miezi mitatu, wakati veta kipawa (ada 145,000) unaisoma kwa mwezi mmoja

  • Kozi ya ELECTRONICS ukienda veta chan’gombe (ada 280,000)unaisoma kwa miezi mitatu, wakati veta kipawa (ada 295,000) unaisoma kwa miez miwili
Kiufupi nnaomba mnijuze haya;

1. Ni kozi ipi yenye hela kati ya hzo mbili?

2. Ni kwa nn veta chang’ombe inatoa kozi kwa mda mrefu kuliko kipawa wakati kozi ni ile ile?

Wasalaam!!
 
Japo kwa Dunia ya sasa bora Electronics kwa kuwa ina watu wengi watumiaji kuliko Computers japo malipo pia hutofautiana.

KWANGU MIMI BORA ELECTRONICS.

Kuhusu chuo, bora Chang'ombe kwa kuwa kozi zake ni bei rahisi (280.000 kwa miezi 3
Japo kibongo bongo utaona bora kipawa kwa kuwa unasoma muda mfupi ILA nenda CHANG'OMBE.
 
Hzo kozi electronics na computer hzo Ni short kozi (miezi 3 ) kozi ndefu Ni miaka miwili .
Sema una haraka na life
hapana sina haraka na maisha, labda nina uelewa mdogo kuhusu hz kozi za veta. Kama kuna ushauri zaidi nauomba mkuu
 
Japo kwa Dunia ya sasa bora Electronics kwa kuwa ina watu wengi watumiaji kuliko Computers japo malipo pia hutofautiana.

KWANGU MIMI BORA ELECTRONICS.

Kuhusu chuo, bora Chang'ombe kwa kuwa kozi zake ni bei rahisi (280.000 kwa miezi 3
Japo kibongo bongo utaona bora kipawa kwa kuwa unasoma muda mfupi ILA nenda CHANG'OMBE.
Asante kwa reply yako
naomba kuuliza, je ufundi simu unafundishwa ndan ya kozi ya electronics? Nauliza hv kwa sababu veta kipawa wamezitenganisha hizi kozi yan electronics ni kozi inayojitegemea na ufundi smu ni kozi inayojitegemea
 
Soma electronics
mkuu hv hii course ya electronics ina kava na ufundi smu? Yan ukisoma tronics uoafundishwa na ufundi cmu? Mana veta kipawa wameziweka separate yan tronics inajtegemea na ufund cmu unajitegemea
 
Back
Top Bottom