Nataka nijue kusoma Quaran

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.

Moja ya sababu zilizofanya niipende dini hii ni kwamba lugha inayotumika ni ile halisia iliyotumika kuandika hii quaran, Napenda sana napokua kwenye dini nisome kwa maandiko orijino, kusiwe na kitu ambacho kimeongezewa wala kupunguziwa, wala kutafsiriwa.

Kuna makosa madogo katika tafsiri ya lugha iliyotumika kwenye maandiko ya kihebrania ya biblia mfano biblia zetu zilizotafsiriwa zimeandika mama yake Yesu alikua ni bikra na ndicho wengi huamini ila biblia orijino ya kiebrania imeandika kwamba mama yake yesu alikua ni mwanamke mdogo anayeweza kuzaa,

Kwa vile hapa Tanzania ni nadra sana kukuta madarasa ya kiebrania Ningejaribu mbali kujua kihebrania ila jitihada zingegonga mwamba kwa sababu nilifatilia kwamba kwamba huko israel dini ya ukristo ni asilimia 2 tu wanaoiabudu tangu ilioruhusiwa mwa juzi (2016) ambapo wengi huabudu judaism na uislamu.

Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,

Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.

Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.

NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.
 
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.

Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,

Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.

Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.

NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.
Kuna aya katika quran inasema:Hakika Mungu anamuongoza amtakaye na humpoteza amtakae...!!karibu ndugu yangu soma uislam uelewe itafaa saana kujua kile unacofata !!
 
Msingi wa elimu ya kislam ni kufundishwa, hata kama una vitabu n.k lazma ukae kwa ustadhi/sheikh akufundishe, ungesema upo wap iwe rahic kuelekezwa wap/kwa nan ukasome, hii itakusaidia kuchukua elim sahihi ya uislam, vnginevyo ukijifungia ndan na audio/vidio zako na vitabu kadhaa hautofanikiwa inavyotakiwa
 
Nenda madrasa au mskiti wowote wa karibu yako utapata private tutor.

Mtandao pia una site nyingi sana za kufundisha Qur'an lakini ni vyema ukapata basics face to face.

Ni wepesi sana kusoma Qur'an na Kiarabu. Hususan kwa anaefahamu Kiswahili.
 
Japo Elimu haina mwisho, kujua na kusoma Qur'an inaweza kuchukua muda gani kwa mtu ambaye ni mweupe kabisa kichwani lakini kila siku anaweza kutenga masaa mawili? Binafsi nahitaji kujifunza nahisi kama naweza kusilimu siku zijazo nafsi yangu inaniambia hivyo...
 
madrasa huko si ni watoto tu
 
sitaki ku comment mengi
kikubwa ni nia tu,hakuna kinachoshindikana.

ulianza darasa la kwanza hata kuandika "a"
ulikuwa huwezi lkn leo unasoma mpaka english.

tafuta mwalimu kwenye msikiti uliopo karibu na wewe nina imani utafundishwa bure na hutatoa hata shili.ngi
 
Japo Elimu haina mwisho, kujua na kusoma Qur'an inaweza kuchukua muda gani kwa mtu ambaye ni mweupe kabisa kichwani lakini kila siku anaweza kutenga masaa mawili? Binafsi nahitaji kujifunza nahisi kama naweza kusilimu siku zijazo nafsi yangu inaniambia hivyo...

3 months
 
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.

Moja ya sababu zilizofanya niipende dini hii ni kwamba lugha inayotumika ni ile halisia iliyotumika kuandika hii quaran, Napenda sana napokua kwenye dini nisome kwa maandiko orijino, kusiwe na kitu ambacho kimeongezewa wala kupunguziwa, wala kutafsiriwa. Kuna makosa madogo katika tafsiri ya lugha iliyotumika kwenye maandiko ya kihebrania ya biblia mfano biblia zetu zilizotafsiriwa zimeandika mama yake Yesu alikua ni bikra na ndicho wengi huamini ila biblia orijino ya kihebrania imeandika kwamba mama yake yesu alikua ni mwanamke mdogo anaeweza kuzaa, Kwa vile hapa Tanzania ni nadra sana kukuta madarasa ya kibrania Ningejaribu mbali kujua kihebrania ila jitihada zingegonga mwamba kwa sababu nilifatilia kwamba kwamba huko israel dini ya ukristo ni asilimia 2 tu wanaoiabudu tangu ilioruhusiwa mwa juzi (2016) ambapo wengi huabudu judaism na uislamu.

Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,

Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.

Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.

NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.
Usiwe mnafiki andika hapa yaliyokufanya uhame watu wajue.

Binafsi nakutakia kila kheri huko uendako ila jitahidi sana kupata walimu wa ukweli wanaoijua dini siyo hawa wa humu JF. Mwalimu wa kweli atakusaidia na kukuongoza vizuri kama Faizafoxy alivyokuambia. Ukiingia choo cha wanawake ukakutana na walimu bomu usishangae ukavalishwa mabomu ukaenda kulipua ndugu zako na wasio na makosa.

Walimu wa uongo watakueleza ukawasaidie waislau wenzako Afghanstan na Iraq utadhani hapa Tanzania hakuna waislam. Watakuambia Waisraeli ni wabaya huku wanamtambua Yesu na Musa wakati hao waiwili ni Waisraeli pia.

Mwisho hakuna tofauti ya ulikohama na unakohamia wote ni matapeli tu. Haakuna kitu kinaitwa dini ni cha ukweli zaidi ya utapeli na kudanganyana.

Mchana mwema
 
Heshima kwenu wakuu, mimi ni kijana (miaka 26) mkristo ambaye hivi karibuni nimefatilia kiundani sana dini ya uislamu na nimetokea kuikubali sana.

Moja ya sababu zilizofanya niipende dini hii ni kwamba lugha inayotumika ni ile halisia iliyotumika kuandika hii quaran, Napenda sana napokua kwenye dini nisome kwa maandiko orijino, kusiwe na kitu ambacho kimeongezewa wala kupunguziwa, wala kutafsiriwa. Kuna makosa madogo katika tafsiri ya lugha iliyotumika kwenye maandiko ya kihebrania ya biblia mfano biblia zetu zilizotafsiriwa zimeandika mama yake Yesu alikua ni bikra na ndicho wengi huamini ila biblia orijino ya kihebrania imeandika kwamba mama yake yesu alikua ni mwanamke mdogo anaeweza kuzaa, Kwa vile hapa Tanzania ni nadra sana kukuta madarasa ya kibrania Ningejaribu mbali kujua kihebrania ila jitihada zingegonga mwamba kwa sababu nilifatilia kwamba kwamba huko israel dini ya ukristo ni asilimia 2 tu wanaoiabudu tangu ilioruhusiwa mwa juzi (2016) ambapo wengi huabudu judaism na uislamu.

Ukristo ni dini nzuri tu ambayo imenilea mpaka hapa nilipo na kila napopata tatizo mungu amekuwa msaada sana kwangu nikiwa katika dini ya ukristo, Sitasema kwamba dini ya ukristo sio nzuri, LA HASHAAA!!!,

Zipo sababu nyingi mno zinaonifnya nihamie kwenye uislamu kutoka ukristo ambazo nikiziweka wazi patatokea malumbano yasiyo na mwisho.

Kwa sasa familia na ndugu zangu wote ni wakristo na sitapenda kuhama ghafla, nataka nipate mwanga wa elimu ya kiislamu kwa kusoma kiarabu ili nispate shida kusoma quarani.

NAOMBENI MNISHAURI MAMBO MUHIMU KUHUSU ELIMU YA LUGHA YA KIARABU ITAKAYONISAIDIA KUSOMA QURAN, NI VITU VIPI INABIDI NIJIFUNZE ILI NAPOANZA KUSOMA QUARAN NA KUINGIA RASMU KATIKA DINI YA UISLAMU NISIPATE TAABU.
Mkuu hongera sana kwa hatua yako.

Ila tu nikupe moyo kwamba Qur'ani ni nyepesi sana haaaaaaswa ukishakijua kiarabu chake.

Wengi wanaoisema vibaya wanaitafsiri kwa mujibu wa lugha zao za tafsiri pasi na kurejea katika maana yake ya asili ya kiarabu yenyewe.

Hivyo ni jambo jema sana mkuu.lakini pia lazima utafute mtu sahihi wa kukufundisha vinginevyo utaingia chaka,na hilo hutolipata illaa kwa kusema ulipo kisha tukakuelekeza uende wapi ambako pana usalama.

Kama ilivyo katika mambo ya dunia kuna waalimu feki hawana ujuzi wowote,kuna madaktari feki wakuunga ungaa,kuna watu hawana pesa ila wanaigiza wana pesa,basi jua pia katika dini wapo waigizaji ambao hawana kituuu kichwani lakini wajanja wajanjaa..

Ni jambo rahisi sana,ukisema ulipo kisha tutakupa msaada wa wapi uende ukasome mkuu.
 
Makazi yangu mara nyingi nipo Moshi, Mbeya mjini na Iringa mkuu...nipe ushauri
 
Owkey owkey mkuu.

Inatakiwa uzikimbie fikra chafu chafu na jazba jazba wanazofundisha baadhi ya waislamu kuwaaminisha wengine eti ndiyo sahihi,unatakiwa upate elimu ambayo haitokuyumbisha kutoka kwa watu wapinzani.

Masaa mawili kwako ni mengi sana aisee hongera,kwanza kabisa kabla ya yote nikupe abc tu kwamba.

Mtu ambaye anaenda kujifunza english kozi atapata wakati mgumu sana ikiwa hajui kusoma na kuandika.huwezi kuta mtu anaenda kujifunza kiingereza au kiswahili alafu awe hajui kusoma au kuandika.

Hivyo ni msingi wa lugha yeyote ujifunze kusoma na kuandika kwanza kabla hujajifunza sheria ya lugha hiyo.

Kwa maana hata kiarabu au Qur'an hautakiwi moja kwa moja kuingia kwenye juzuu kabla hujajua kuandika na kusoma japo kwa uchache wake.

Usiingie tu paaap ukaanza kusoma kiarabu ilhali hujajua kuandika na kusoma kiarabu JAPO KWA UCHACHE WAKE.

Natamani ungekuwa karibu ningejitolea muda na mimi lakini haiwezekani.

Nimetumia njia hiyo kuwafundisha wadogo zangu,nilikuwa nawafundisha herufu za kiarabu na namna zinavyosomwa alafu baadaaaeee ndo nikaanza kuwafunza Qur'an ikawa wepesi kwao kujua na kujisomea wenyewe kwa sababu walianza na msingi mzuuuuriiiiii.

Hivyo na wewe weka aibu pembeni,ikiwezekana upate mtu akufundishe peke yako kwa namna ambavyo unatakiwa kuanza,sio akuchanganye na watu wengine ambao wameshajua A B C tayariiiii

Back
Top Bottom