Mnyama wa kitabu cha Ufunuo
Watu wengi hawafahamu kuwa mnyama ni nani, na wengi wamejihusisha naye bila wao wenyewe kujua kama wanashiriki na mnyama. Lakini Mungu hajatuacha gizani, hivyo, kwa kupitia neno lake (Maadiko Matakatifu) tunaweza kumfahamu mnyama huyu aliyelezwa katika kitabu cha Danieli na Ufunuo. Tunapaswa kuyaacha maandiko yajitafisiri yenyewe; kwa maana “hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.” 2Petro 1:20-21. Hatupaswi kumuacha mtu flani atafsri unabii kwa jinsi yake mwenyewe, badala yake tunapaswa kuiacha Biblia ijitafsiri yenyewe.
Katika Danieli 7 wametajwa “wanyama wanne” ambao wanawakilisha falme nne. Kumbuka mmyama wa 4 aliyetajwa katika Danieli 7 ndiye mnyama aliyetajwa katika kitabu chote cha Ufunuo. Hivyo hapa tutaangalia sifa za mnyama wa nne wa kitabu cha Danieli, na mnyama wa kitabu cha Ufunuo, kisha tutaangalia ni wapi hapa duniani ambapo sifa za mnyama zinatimizwa kikamilifu.
1. Mnyama atakuwa na uwezo wa kisiasa na kidini (kanisa na serikali).
Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona MWANAMKE, AMEKETI JUU YA MNYAMA mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi.”
Mwanamke au bibi-arusi katika unabii huwakilisha kanisa.
Ufunuo 21:2 “…Yerusalemu mpya…umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.”
Ufunuo 21:9 “…Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.”
Mnyama huwakilisha taifa au ufalme
Danieli 7:17 “Wanyama hao…wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani”
Danieli 7:23 “…Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia…”
Kutokana na Ufunuo 17:3, mnyama huyu ana mwanamke aliyeketi juu yake, na kwa sababu unabii unatafisiri mwanamke kama kanisa, na mnyama kama taifa. Je kuna taifa au serikali ambayo imechanganywa pamoja na kanisa kama kitu kimoja? Ndiyo! Vatican, ni serikali au taifa ambalo limechanganywa pamoja na kanisa la Romani Katoliki kama kitu kimoja, na kuongozwa na mtu mmoja ambaye ni Papa.
2. Mnyama atakuwa na kanisa & serikali vimekaa juu ya milima 7.
Ufunuo 17:3 “Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana…mwenye VICHWA SABA na pembe kumi.”
Vichwa saba katika unabii vinawakilisha milima saba.
Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo.”
Je hapa duniani kuna kanisa na serikali vimekaa juu ya milima saba?
“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic Encyclopedia, p 529.
“Je vilima saba vya Roma ni nini?
Roma inajulikana kuwa imejengwa juu ya vilima saba. Roma ilisemwa imepatikana wakati Romulus na Remus, wana mapacha wa Mars, walifika katika futi ya kilima Palatine na wakauanzisha mji, Vilima sita vingine ni Capitoline (kiti cha serikali), Quirinal, Viminal, Esquiline, Caelian, na Aventine.” –Geography.about.com
ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Vilima saba vya Roma
“…kundi la vilima juu au kuhusu ambapo mji wa Roma wa zamani ulijengwa. Mji wa awali wa Romulus ulijegwa juu ya kilima Palatine (#1) (Kilatini: Mons Palatinus). Vilima vingine ni Capitoline, (#2) Quirinal, (#3) Viminal, (#4) Esquiline, (#5) Caelian, (#6) na Aventine (#7) (Vinavyojulikana kimoja kimoja kwa kilatini kama Mons Capitolinus, Mons Quirinalis, Mons Viminalis, Mons Esquilinus, Mons Caelius, na Mons Aventinus).” –
http://www.britannica.com/seo/s /seven-hills-of-rome/
Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali, harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la Romani Katoliki pekee.
TATIZO ni wavivu kusoma