Nataka niende mikoa, Dar es Salaam kugumu

Moro kubwa ila kilombero itakuwa poa same sikushauri,Dodoma pako poa Mbeya sidhani Tanga pako poa ile mijitu mivivu ila matoto kusoma hayapendi jaribu kuangalia fursa
 
Ugumu upo Kwenye fikra zako boss, kwa sababu aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo. Workout on your mentality, otherwise huko unapotaka kwenda yatakuwa yaleyale.
 
1. Nenda katavi.
2. Nenda Morogoro maeneo ya kilimo cha mpunga, pia fanya urafiki na wamasai wakufundishe biashara ya Ng'ombe.
 
Wangari Maathai Nililala Station Moro, Mto bag langu.

Asubuhi nikaondoka, yaani hata kutembea tu nilikuwa natembea kwa shida mpaka nikawa naona watu wananiangalia ( Najua tu walikuwa wanaona kweli jamaa ana shida sana )

Kumbuka, Nimepanda train bila kujua naenda wapi, nafikia wapi na kufanya nini ~ Nilishukia Moro kwasababu ndio ilikuwa mwisho wa nauli yangu.

Nikawaza, Nikaamua kwenda kwa rafiki yangu mmoja ( naye alikuwa anabebwa na mtu tu, siyo ndugu yake ).

Kama ujuavyo ukifika kwa mtu lazima useme unaondoka lini, isije kuonekana kama ndio umehamia.

Siku Nimefika ilikuwa Jumamosi, Na Jumatatu nikatakiwa niondoke. Chuo nilikuwa nimepata ila nilichelewa kuripoti kutokana na kukosa ada, wakasema hawapokei tena.

Basi, Kuna mshkaji wangu alikuwa huko kijijini ( nilikuwa namsaidia kuapply vichuo NACTE ~ Kwa sasa Assist C.O ) Nikamwambia kuna nafasi chuo fulani wametoa watu waapply second selection atume pesa nimfanyie. Lengo akishatuma nijifanyie mwenyewe - huenda majibu yakitoka nitakuwa nimepata ADA.
 
Back
Top Bottom