Nataka niende mikoa, Dar es Salaam kugumu

October man

JF-Expert Member
Nov 23, 2017
3,635
4,995
Nimeishi Dar es salaam toka nazaliwa nilichoona kuishi Dar bila mtaji wa maana ngumu.

Mikoani huko sinaga ndugu wala connection yoyote Origin yangu ni Dar ila sasa nataka nijilipue mikoa mingine nikazisake pesa nirudi na capital ya kutosha hapa Dar nimegundua kunalemaza vijana wa umri wako wote unaona hawana maisha kabisa sitaki nikae nyumbani kabisa tena.

Kuna mikoa niliyoilenga kwenda kwenda kutokana kidogo nina washkaji niliosoma nao wanaishi huko kwahiyo nakuwa na urahisi na pa kufikia na kujua pa kuanzia.
1) Morogoro
2) Moshi (Same)
3) Dodoma
4) Mbeya
5) Tanga

Naomba kujua mkoa gani utakuwa mzuri zaidi wa kwenda ambao unafursa za kukufanikisha fasta kiuchumi, napenda munipe direction ya mkoa ulio profitable zaidi hapo. Vibarua kama viwanda, mashamba nk.

Pia nataka mkoa ambao rahisi kupata hata Shule ya kufundisha maana nimesoma Education.

Dar competition kubwa sana nataka mkoa ambao sito hustle sana kupata hata kibarua chochote au shule ya kufundisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Manyara au Rukwa au Katavi hivi kwa hiyo digree yako utatoboa hata Tanga pia nako poa tu

DSM nimeshaishi kwa kweli kwa wenye mitaji midogo hawatoboi pale

Mikoani laki tano ni mtaji wa kutokea kabisa which it is vice versa in DSM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom