Naomba kujua nauli ya kwenda na kurudi Dubai na je kule ni kweli bidhaa za electronics zinapatikana kwa bei rahisi kidogo ukilinganisha na huku kwetu?:shock:
Candid upo sawa kabisa lakini kwa Arabuni nadhani ni tofauti kidogo,kipindi cha summer ni summer kweli ata wafanyakazi wa hotelini wanaombwa kuchukua likizo maana hakuna wageni,sasa kipindi hicho ticket zinakuwa cheap sana,nakumbuka mwaka jana nili invite rafiki kuja kutembea tulitumia Etihad airline Nairobi-Abu dhabi ilikuwa $300 two ways na Visa ya mwezi mzima $80,lakini kwa wazoefu hawanunui mzigo Dubai wananunua Sharjah ambayo ni nje kidogo ya Dubai..Lakini fanya uchunguzi wa nini unachotaka kununua na kodi yake kwa Tz.
Mimi kwa mda mrefu sana huku sijawai kuona wafanyabiashara wa kongo au west afrika wakiwa mmojammoja,siku zote wanaungana na kuwa kundi la watu kama saba na kuendelea,faida yake ni kuwa wananunua mzigo mkubwa kwa pamoja hivyo wanapata punguzo kubwa(factory price)faida nyingine ni kwenye hoteli wanazofikia ambazo ni maalumu kwa wafanyabiashara vyumba vinakuwa cheaper maana wana share,faida nyingine ni pindi wanapotuma mzigo,container la futi 20 kulisafirisha toka Dubai mpaka Tz ni $1700 hawa jamaa uchukua container zima na kuweka vitu vyao sasa utakuta wanachanga kama $300 kila mmoja na mzigo unakuwa safe,faida nyingine ni kwenye ushuru,hasara pekee wanayoipata ni mzigo wao unakuwa unafanana kama wale wafanyabiashara wa nguo kariakoo ila wanapata faida kubwa sana.
Hivyo nakushauri tafuta mtu mwenye biashara kama yako ili muungane biashara ya kusafiri nje kwa peke yako ni nzuri lakini ni nzuri zaidi kama ukiungana...Two heads are better than one...Nikupe mfano mmoja niliwaikukutana na kijana wa ki TZ akaniomba nimwoshe wapi atapata parfume nikampeleka dukani kufika pale akaomba apewe pcs 80 bei aliyopewa haikuwa nzuri lakini angekuwa na vijana wenzake at least watatu wangeitaji pcs 250 wao ndio wangepanga bei ya zile parfume,
Ukiwa peke yako taxi utakodi peke yako na siti zote za nyuma utazilipia,utapanga chumba ambacho mngekaa watatu lakini ukiwa peke yako ni shiiidaaa unless una mtaji mkubwa na uzoefu....
ukifika Dubai nitafute +971504374387