Kwa vifaa vya ujenzi ni cheap kupita maelezo ila bati zipo juu,ndio maana siku hizi Tz utakuta mtu kajenga nyumba boma tu akaliacha,akaja Dubai kununua finishing material zote mpaka dirisha za aluminium utakalouziwa kwa tsh 300000 huku utalipata likiwa complete kwa tsh 42,000/rangi nyingi tunazotumia Tz zimetengenezwa arabuni very cheap.Tiles,sinks etc Furniture ndio kabisaa kuna kabati nilituma kuzunguka kariakoo nilikuta ni tsh 850,000 sikuamini macho yangu mimi nilinunua chini ya 250,000/,vifaa vya ujenzi havina ushuru mkubwa..isipokuwa cement ndio unatakiwa kukumbuka kuomba cheti cha ubora ili ikifika Tz Tra wasikusumbue,na cement wanaopata faida zaidi ni wafanyabiashara maana wakiweka kwa container kubwa ata wakitozwa ushuru mkubwa na wakauza kila mfuko kwa Tsh 8,500/ bado wana faida.vifaa vya umeme ndio kabisa mwaka jana nilinunua bunda la waya 1.5 kwa tsh 25,000..Kwa biashara ya nguo ni Thailand lakini kwa vifaa vya ujenzi,spare na electronics Dubai ni pazuri zaidi na sio mbali sana hivyo utumaji wa mzigo unachukua siku chache na gharama nafuu,kutuma container la ft 20 ni $1700 na kuna kampuni nyingine ni chini kidogo na ndani ya siku 10 mzigo upo port Dar.na kama utaki container kutuma kwa box CBM ni cheap pia.Cement nyingi inayotengenezwa Dubai sasa ina demand kubwa Qatar maana wana ujenzi mkubwa wa hotels na viwanja kwa ajiri ya world cup sasa bei imepanda wanauza tsh 3,900 kwa mfuko