Nataka kuwa mwana usalama wa Taifa

Nataka kuwa mwana usalama wa Taifa

Habarini wakuu.

Mimi ni memba mpya(kwenye kuanzisha uzi) ila ni memba wa muda kama shabiki wa JF.
Huu ni uzi wangu wa kwanza kuuanzisha(mnisamehe kama kuna mahali nitakosea)

Turudi kwenye maada..

Siku nyingi(kabla sijawa memba wa jf) nimekuwa nikifuatilia sana masuala mazima ya kiusalama kupitia movie na magazeti,na baada ya kupakua app ya JF nilikutana na maada mbal mbal zinazohusu maswala mazima ama story zinazohusu usalama.

Baada ya kuendelea kufuatilia na kusoma kila nnachokutana nacho na kinahusu usalama,niliweza kufunguka kiakili na kimawazo kuhusu swala zima la usalama.

Miongon mwa vitu vilivyonifungua akili ni pamoja ya namna hawa watu(mashushushu) wanavyopatikana,ikiwa ni pamoja na mashulen na kupitia vyombo mbal mbal vya usalama kama JKT n.k

Baada ya kuwa nimefunguka kiakili kuhusu jambo hili ,nilikata tamaa na kuona siwez tena kuwa shushushu kwa sababu sipo shule,na siwez tena kwenda JKT kwa maana umri umeshaenda(nna miaka 27 na elimu yangu ni kidato cha 4).

Lakini nilijipa moyo na sikujidekeza kwa kuendelea kukata tamaa,na badala yake niliendela kufuatilia maada mbali mbali na historia mbali mbali za kijasusi kupitia hapa hapa JF kama maada za mkuu The bold na za watu wengine wengi.

Sasa bas leo nimeamua kuvunja ukimya na kuamua kuja kwenu wana jamvi na kuwaomba msaada wa kimawazo na ushauri wa nn nifanye ama nn nifuate ili niweze kuwa miongoni mwa hawa watu wa usalama(TISS) ama kama kuna kikosi kingine cha kiusalama. Nikimaanisha nitaingia vipi ndani ya 18 ya hawa jamaa ili wanichukue na mm?

Nafahamu kuwa ni ishu ya siri na ni ishu ambayo sio ya kuweka hadharan,kama kuna mambo ya hadharan mtanipatia,na kama kuna ushauri wa sir bas hata PM nitaupokea pia.

Mm ni mzarendo na ninafaham hii kazi inahitaji moyo na unahitaji uzarendo pia,katika hili hakuna shida.

Naipenda nchi yangu TANZANIA na nipo tayal kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwa nguvu zangu zote.



Nawasilisha hoja,naombeni msaada wenu.
Na naomba radhi sehemu yeyote nitakayokuwa nimekosea.
Ungefahamu "usalama wa taifa" ni jukumu lako usingeomba ulichoandika.Hata wewe ni usalama wa taifa kwa kua ni mtaifa ninachoona ni TAMAA
 
Njoo na ID yako ya zamani,,,ili nkushaur vzur
Siikumbuki.maana nlijiunga mwaka 2015,kisha nkapotea humu ndani.baadae mwaka jana nkarudi tena,but nkawa nimesahau pasword naa username. Ndo nkafungua tena hii. Jana ndio nkaanzisha uzi wa kwanza toka niijue JF
 
Ungefahamu "usalama wa taifa" ni jukumu lako usingeomba ulichoandika.Hata wewe ni usalama wa taifa kwa kua ni mtaifa ninachoona ni TAMAA
Tamaa ya nini sasa mkuu?? Kama ni ajira tayali ninayo
 
Hata mim kazi hiyo ya Usalama wa Taifa ninaipenda toka moyoni na nimejaribu kuifuatilia kinoma but sijawahi ona Post zao. Naamin hapa Jf kuna watu wenye Access na hii ishu.. nina miaka 31 na ni graduate wa Bachelor. Plz mwenye information na hizi kazi aniPm if possible
 
Mtafute Yericko Nyerere na Jason Bourne wakupe ABC za Ujasusi.

Kwanini unapenda kujiunga na TISS? Kuna Role Model uliyemuona ukatamani na wewe uwe?

Kwa Maelezo yako umesema una kazi,kwanini uipendi hiyo kazi uliyonayo inayokupa mkate?

Kwahiyo wewe hauwezi kuwa polisi jamii au whistle blower?
Nitawatafuta mkuu.

Ila kuhusu swal lako la kwann napenda kujiunga TISS?
Napenda kujiunga kwa sababu naipenda hii kazi na naipenda nchi yangu pia.
Kuhusi mtu anaenivutia kwa hapa Tz (anaefanya usalama) sina. Ila navutiwa na mshilika humu ndan The bold kutokana na stori zake na maelezo ma ufafanuzi wake kuhusu maswala ya usalama na protokal mbali mbali za mambo hayo.

Kuhusu swal lako la kwann siipend kaz yangu nlionayo na nnataka kuwa TISS?
Nipo tayali kufanya kazi ya usalama hata bila malipo yoyote,ili mladi tu waniruhusu niendelee na mishe zangu ama ajira nilionayo ili nipate mkate wa kila siku
 
Nia unayo lkn hawajama hawavhukia MTU bila kumfanyia uvhunguzi wa khaki ya juu maana issue yenyewe iko very sensitive watu wengi wanapenda lkn wanashindwa so tafuta kitu kingine
 
Kipi kimekuvutia kwenye hii kazi?!
Toka nikiwa mdogo nilikuwa mkakamavu sana ,na nilitaka nifanye kazi ya ukakamavu na ya kujitoa.

Lakini pia watu hawa huwa wananifurahisha kwanza utunzajibwao wa siri na kujitoa kwa ajili ya watu wachache ,napenda sana kujitoa kwa ajili ya wanzangu ilo ili wawe salama.
 
Back
Top Bottom