Nataka kuwa mchawi anaeujua vyema naomba anifunze

kiraza

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
303
500
*Mimi ni kijana wa umri wa miaka 25, naishi dar es salamm Bado sijaoa.

Dhumuni la kuja hapa jukwaani mbele yenu leo hii ni kuomba msaada wa kuujua Uchawi/Nguvu za kiroho ziliyo na matokeo ya wazi katika maisha haya.
ONYO.
Katika thread hii sitapenda kusikia kabisa habari za Mungu,
Sababu za kutopenda kusikia neno hili ni kwa sababu nimeshaishi sana
maisha ya kumuomba na kumtumaini bila mafanikio, Kwangu mimi Mungu amekuwa kimya
kabisa na hajajibu lolote tangu nilipoanza kumuomba zaidi ya kuzidi kupata
changamoto na mikosi lukuki.
Hivyo kwa kwa mshauri yoyote hapa nitaomba anipe na anifunze habari labda za Mungu mwingine mwenye nguvu za wazi akiombwa kwa dhati., na si hii Miungu iliyo Maarufu katika jamii hizi tunazoishi.

Kwa ufupi mambo fulani yaliyonisukuma kuja kuomba msaada huu na yafuayo ni baadhi.

1. Bila kuwa na nguvu yoyote ya kiroho huwezi kuishi kwa raha na amani maishani mwako
zaidi utakuwa ukiwasindikiza wenye uwezo fulani wa kiroho.
2. Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa wanadamu wengi wenye roho ambazo hazina huruma kirahisirahisi, mazulumati, waonezi wa wanyonge ndio wenye mafanikio makuu kimaisha.
ukilinganisha na watu wa kawaida wanaochakaa kwa dhiki huku wenye ahueni
wakipambana na shida, hasa ya Pesa na magonjwa
3. Watu wengi wenye mafanikio ni watu wasiri ambao hawana pupa kwenye kila jambo na hata kwenye kutoa msaada, watu hawa huwa hawatoi misaada hovyo hovyo, huwa wanatoa misaada kwa sababu maalum, tofauti na mtu wa kawaida anavyopita Kariakoo na kuwagawia ombaomba
hela kidogo aliyonayo.

Hivyo kwa sababu hizo na nyingine lukuki nilizonazo kichwani nimeamua kuchukua Uamuzi huu wa,KUTAFUTA JINSI YA KUPATA ELIMU YA UCHAWI/NGUVU ZA KIROHO.
Maana katika kufikiria nimepata wazo kuwa Nguvu za kiroho ndizo zinazofanya mabadiliko ya mwili.

Hivyo kwa mtu yoyote ambaye anadhani ana uwezo wa kunisaidia kuhusu kunifunza elimu hizi naomba sana msaada wake, nipo radhi hata kupotea kwa miaka na kurudi huku nikiwa nimekamilika kimwili na kiroho ili niweze kuishi na hizi nafsi za wanadamu kwa raha.

NB: Elimu ninayoilenga sio ya kuitoa familia yangu sadaka, maana familia yangu hasa ndiyo lengwa kwenye mafanikio yangu.
Kwa yeyote anayeweza kunisaidia naomba aniPM.
ASANTE
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,641
2,000
Hakuna uchawi kiuhalisia.

Kilichopo ni dhana tu.

Hivyo acha kujilengesha kwa matapeli wataotaka kukutafunia hela na mali zako, kama unazo.
 
Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,260
2,000
Ndugu kiraza. Nitakufunza uchawi ambao utakuletea pesa nyingi mikononi mwako.
Fanya yafuatayo kufikia malengo:
Tafuta kuku mweusi tii halafu umchinje usiku wa manane kwenye sehemu ambapo huwa kuna mkusanyiko mkubwa wa watu kam vile kwenye minada au sehemu za mikutano ya kisiasa.
Ukimchinja ukinge damu yake na uondoke nayo pamoja kichwa cha huyo kuku.
Ukifika nyumbani kwako usizungumze na MTU yeyote na uende moja kwa Moja mpaka chumbani kwako.
Ile damu ihifadhi mahali ambapo haitaguswa na mwanamke. Kile kichwa kichemshe na mchuzi utakaopata(_usizidi 1000mls) uweke kwenye chupa safi halafu uweke uvunguni kwako(asiguse mwanamke) kwa muda wa siku Tatu,siku ya NNE ichungulie(iangalie) na ukikuta kitu chochote kwenye huo mchuzi(nyoka au kitu chochote cha hatari) usikimbie ila mchukue huyo utakayemkuta kama ni nyoka halafu umpike lakini hakikisha unakuwa peke yako na mchuzi utakaopata ufanye kuwa ndo maji yako ya kunywa kila siku asubuh kabla hujala au kupiga mswaki. Usinywe mchuzi mwingi sana,2-4mls zinatosha kwa siku mara Moja tu asubuhi.
Siku ya NNE toka umeanza kunywa huo mchuzi utapigiwa simu na namba inayoanzia 3678.......90. Ipokee hyo namba na utaelekezwa mahali ilipo Mali yako. Ukifika maeneo uliyoelekezwa(_itakuwa sehemu ambapo kuna watu warefu sana ambao hujawshi kuwaona hapa duniani) usiogope na utakabidhiwa mfuko mdogo ambao utakuwa na kiganja cha sokwe aliyeishi miaka 390 iliyopita. Kupitia huo mkono(kiganja) utakuwa unauomba ukupe kila kitu unachotaka.
Ile damu ya kuku itakuwa ni kama mafuta yako ya kupakaa kila siku asubuhi kabla hujaanza kazi zako.
Usipende mke wa MTU
Onyo:_ pesa utakazopata usihonge.
Usinywe pombe.
Hakuna malipo ya awali kutoka kwako kuja kwangu kabla hujafanikiwa.
Ukifanikiwa tafadhar nitafute kwa ajili ya malipo yangu.
Ukishindwa kunitafuta tafadhar usinilaumu
Utekelezaji mwema
 
Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
7,906

Hakuna malipo ya awali kutoka kwako kuja kwangu kabla hujaganikiwa.
Ukifanikiwa tafadhar nitafute kwa ajili ya malipo yangu.
Ukishindwa kunitafuta tafadhar usinilaumu
Utekelezaji mwema
aisee! job true true
 
Los técnicos

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
2,712
2,000
Du hata malaika anaweza kubadilika kuwa shetani. Magufuli wahurumie vijana hawa usipowahurumia taifa litakuwa la waganga na washirkina
 
Rais2020

JF-Expert Member
Jul 14, 2016
3,260
2,000
Mkuu swala la uchawi haliangalii umri. Huo umri wake ni mkubwa saaaana kuwekeza kwenye uchawi. Ukizingatia ushaur wangu hapo juu ww utakuw ni mchawi wa kimataifa
 
Abuu Kauthar

JF-Expert Member
Jul 10, 2011
3,342
2,000
“Na wakafuata yale waliyozua Mashaytwaan kuuzulia ufalme wa Sulaymaan. Na wala Sulaymaan hakukufuru, bali Mashaytwaan ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Allaah. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walichojiuzia nafsi zao laiti wangelijua” (al-Baqarah [2]: 102).
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom