Nataka kusema lakini wa kumwambia simpati

Nataka kusema lakini wa kumwambia simpati

Pole ndugu yangu kwanza amini Mungu hamtupi mja wake hali unayopitia ni ya muda mfupi tu. Mkristo maana yake mfuasi wa kristo yesu. Sasa kama yesu alikubali kutoa uhai wake ili mimi na wewe tukombolewe sembuse mtu wa kukusalimia/kumwambia yanayokusibu? Kwa mujibu wa wataalamu wa saikolojia kumwambia mtu mwingine kile kinachokusibu ni hatua mojawapo ya wewe kuondoa/punguza stress. Please kama hautojali karibu
Mungu akubariki mkuu
 
Niko katika hali ya kusikitisha kila siku mimi hulia machozi maana sina hata mtu wa kunisalimia hata kwa mbali nahisi kufa kufa hata sili maana ninaowahitaji nafikiri hawanihitaji hata kidogo. Sijui mimi nimemkosea nini Mungu.

Naombeni ushauri.

Maskini hadi nmekuonea huruma, ongea na mie mwaya.....(serious)
 
Nielewe mimi sililii mapenzi au ngono ziko kila kona
Khaa!! What's your point???
A%20S%20shade.gif
 
Mkuu kwan hao wa kona bar amekwambia ka wakosa? Ye anacho maanisha wa maishan mwake na sio wa tempo tu! Hao wa bar weng wao n pesa tu na sio kuwekwa ndan
we utakua punga mwanaume hawezi kuja kutangaza huwa analia kwasababu hakuna anayempenda, unataka kusema hata wale wa kona bar nao wanakukataa?
 
Mkuu kwan hao wa kona bar amekwambia ka wakosa? Ye anacho maanisha wa maishan mwake na sio wa tempo tu! Hao wa bar weng wao n pesa tu na sio kuwekwa ndan

Bora umemjibu vyema
Maana yy kakazania madada poa wakati mimi sijasema kuwa nahitaji kwani kama ni kuwahitaj si wako 24hr kila kona.

Ninaowahitaji sio kwa ajili ya ngono
 
Niko katika hali ya kusikitisha kila siku mimi hulia machozi maana sina hata mtu wa kunisalimia hata kwa mbali nahisi kufa kufa hata sili maana ninaowahitaji nafikiri hawanihitaji hata kidogo. Sijui mimi nimemkosea nini Mungu.

Naombeni ushauri.

Eeeeh kumbe hilo tuu.. haya Shikamoo,umeamshwaje?maambo?how are u? umekula jmn leoo? jmani kula hata kidogoo njoo nkulishe hata vjiko viwili... Wengine wanisaidiee popote maana kusaidiana duniani muhimuu
 
Umetisha kamanda big up sana

Nimekaa nikagundua katika hii Dunia watu wengi wanataka kuongea lakini hawapati mahali pa kuyasemea.

Nimegundua katika vitu Muhimu vilivypotea katika hii Dunia basi ni Faraja ama kujaliwa kukubaliwa kutambuliwa. Kitu ambacho wengi hawavifanyi.
 
My point ni kuwa ninaowahitaji siwahitaji kwa ajili ya ngono

That is my point
Khaa!! Hapa naona sina ushauri Zaidi, labda usubiri wataalam wa afya ya ubongo nadhani ndipo tatizo lilipo :glasses-nerdy:

cc mshana jr
 
Pole...karibu kwenye club lol....ndo hivyo kuwa uyaone!!! my advise be happy while you're single, atatokea mtu atakupenda.
 
kazi nafanya sababu ni wajibu wangu.
Lakini jamii yangu ndio inanifanya nahis watu hawa sio sahihi kwangu.

Watu walionizunguka ni wabinafsi

watu walionizunguka ni wasengenyaji

watu walionizunguka ni kwa ujumla ni wachoraji kukuchora, kukukebehi ili waone unajibu nini nimevumilia sana lakini bado.
umejuaje wanafanya yote hayo? ni kwa sababu unawafatilia au umeachia wakuendeshee maisha yako. Hawa watu wabinafsi, wasengenyaji na wachoraji wako kila kona. Hata humu wamo. Ndo hulka ya mwanadamu. Unachotakiwa ni kuanzisha mahusiano na nafsi yako. Ujijue wewe ni nani, ujipandishe thamani yako mbele ya macho yako na uwe accountable kwa Muumba wako tu. Unapofanya kitu lenga kujifurahisha wewe mwenyewe na uangalie kama kinamfurahisha Muumba wako. Ukikosea mahali kama ilivyo hulka ya mwanadamu, fanya toba kwa Mungu ' kisha jisamehe na ukubali matokeo ya kosa lako kisha songa mbele.

Kamwe usilenge kuwapendeza binadamu maana hawana asili ya wema. Hata uwe umefanikiwa kiuchumi kama Dangote watakusengenya na kukuchora, hata uwe umefanikiwa kiroho kama Hinnie watakuchora tu.

Cha msingi ni kutokuwaza watu wanasema nini juu yako, na hata ukijua wanasema nini juu yako kama utakuwa umeshatengeneza amani na nafsi yako maoni ya watu hayawezi kukuumiza. Kwa hiyo anza kufanyia kazi imani yako juu yako mwenyewe. Anza kujiamini na kujikubali. Ukijiamini na kujikubali utaanza kuhisi watu wanakuona kama unavyojiona wewe. Kama unajiona mtu mzuri hilo ndo la msingi. Kama unajiona una mapungufu na unahangaika kuyaondoa ili watu wakuone huna mapungufu lazima ujione mpweke maana hutaweza ku-dictate jinsi unataka watu wakuone au kukunenea. Ukijitambua, ukajikubali na kujiamini hata kama watu watasema tofauti na unavyojiona, wewe haitakusumbua kwa sababu utakuwa unajiambia "wanasema hivi kwa sababu hawanifahamu. Mimi ndiye ninayejifahamu na Muumba ndo anayenifahamu na kunielewa zaidi". Baaas, unaendelea na maisha yako.
 
Pole...karibu kwenye club lol....ndo hivyo kuwa uyaone!!! my advise be happy while you're single, atatokea mtu atakupenda.
huyu kaka hamjamwelewa. He just feels unloved and unappreciated. it has nothing to do with his relationship status. whether single or married, it happens - something to do with self-esteem. by the way, are you living your advice? the sentences before the advice are indicating trouble. sorry ooh
 
Khaa!! Hapa naona sina ushauri Zaidi, labda usubiri wataalam wa afya ya ubongo nadhani ndipo tatizo lilipo :glasses-nerdy:

cc mshana jr
Ntashukuru pia mkuu
 
Back
Top Bottom