Nataka kusema lakini wa kumwambia simpati

Nataka kusema lakini wa kumwambia simpati

umejuaje wanafanya yote hayo? ni kwa sababu unawafatilia au umeachia wakuendeshee maisha yako. Hawa watu wabinafsi, wasengenyaji na wachoraji wako kila kona. Hata humu wamo. Ndo hulka ya mwanadamu. Unachotakiwa ni kuanzisha mahusiano na nafsi yako. Ujijue wewe ni nani, ujipandishe thamani yako mbele ya macho yako na uwe accountable kwa Muumba wako tu. Unapofanya kitu lenga kujifurahisha wewe mwenyewe na uangalie kama kinamfurahisha Muumba wako. Ukikosea mahali kama ilivyo hulka ya mwanadamu, fanya toba kwa Mungu ' kisha jisamehe na ukubali matokeo ya kosa lako kisha songa mbele.

Kamwe usilenge kuwapendeza binadamu maana hawana asili ya wema. Hata uwe umefanikiwa kiuchumi kama Dangote watakusengenya na kukuchora, hata uwe umefanikiwa kiroho kama Hinnie watakuchora tu.

Cha msingi ni kutokuwaza watu wanasema nini juu yako, na hata ukijua wanasema nini juu yako kama utakuwa umeshatengeneza amani na nafsi yako maoni ya watu hayawezi kukuumiza. Kwa hiyo anza kufanyia kazi imani yako juu yako mwenyewe. Anza kujiamini na kujikubali. Ukijiamini na kujikubali utaanza kuhisi watu wanakuona kama unavyojiona wewe. Kama unajiona mtu mzuri hilo ndo la msingi. Kama unajiona una mapungufu na unahangaika kuyaondoa ili watu wakuone huna mapungufu lazima ujione mpweke maana hutaweza ku-dictate jinsi unataka watu wakuone au kukunenea. Ukijitambua, ukajikubali na kujiamini hata kama watu watasema tofauti na unavyojiona, wewe haitakusumbua kwa sababu utakuwa unajiambia "wanasema hivi kwa sababu hawanifahamu. Mimi ndiye ninayejifahamu na Muumba ndo anayenifahamu na kunielewa zaidi". Baaas, unaendelea na maisha yako.

Nakiri katika shauri zote katika huu uzi hii ni zaidi ya shauri.

endelea na moyo huo huo mkuu.
 
Khaa!! Umekuwa mama huruma ghafla??? Ajabu sana
A%20S%20shade.gif

Kama ajabu peleka jumba la maonesho watu wakashangae
 
Fafanua vizuri Mkuu ili nipate kitu

Mtangulize Mungu kwenye kila jambo lako kwanzaa...
Fanya maamuzi ya akili na usikurupuke,
Tafuta ela kwa bidii..

Vingine vyoooooote ni ziada na vinafuata hayo ya juu
 
Ili uwe mtu wa kupendwa - wewe penda
Ili uwe na marafiki- Wewe kuwa wakwanza kuonyesha urafiki
Ili usalimiwe - wewe salimia, toa tabasamau kwa wenzio
Ili ukubaliwe -Jifunze kukubali, kuheshimu na kuwa karibu na wenzako (marafiki , ndugu)
Ili upendwe (si mapenzi) - wewe kuwa wa kwanza kuonyesha wema, msamaha na upendo

Ni kweli dunia imejaa choyo, husuda na kila ovu na mbaya zaidi faraja imepotea . upendo na usikilizano umepewa thamani ya vitu kama pesa, ngono , nguvu, matabaka nk kumbe nafsi zetu ndani hazishibi kwa uongo huu. Nafsi zinalilia sikio tu linaweza kusikia shida yako, nafsi zetu zinasubiri mdomo usemao ahsante na unaotia moyo . Nafsi zetu zinakiu ya rafiki / ndugu anayesema ni sawa maisha yataenda mbele . Nafsi zetu zina kiu ya kusikia msamaha unatolewa. Nafsi zetu zina kiu ya kuona haki, ustawi na vicheko kwa watoto, wazee , vijana na wasiojiweza .

Basi wewe mtoa mada kuwa wa kwanza kutoa nuru hii kabla hujasubiri kupewa . The Law of attraction inasisitiza- "whatever you give to the universe , you somehow create it to come back to you" . Be the first to make the changes you wish to see. And avoid blaming : people can disappoint you -but it depends on how you react to the disappointment .
 
  • Thanks
Reactions: M45

Asante sana mkuu.
 
huyu kaka hamjamwelewa. He just feels unloved and unappreciated. it has nothing to do with his relationship status. whether single or married, it happens - something to do with self-esteem. by the way, are you living your advice? the sentences before the advice are indicating trouble. sorry ooh

Oooh really,,,,kumbe nimemiss point....sorry nilifikiri single. Huyu kweli inaonyesha ni self esteemed issue. Inabidi afix hiyo kabla kutegemea mtu mwengine akupende. Yes, I walk the talk.......I am enjoy my moments when I am single, siko desperate ya kupendwa unakuta mtu analower standards just to be loved.

Love is never chased or begged is given freely......
 
Tatizo ccm. Ndio imekufikisha hapo. Mwaka huu fanya maamuzi
 
Back
Top Bottom